· Januari, 2010

Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Januari, 2010

Rais wa Malawi kutangaza rasmi penzi lake siku ya Valentine

Wamalawi wanatafakari taarifa kuwa mnamo tarehe 1 Mei, rais wa nchi Dkt. Bingu wa Mutharika anatarajiwa kumuoa waziri wa zamani wa utalii Callister Moyo. Harusi hiyo itatanguliwa na sherehe za kitamaduni za uchumba wakati wa siku ya wapendanao ya Valentino tarehe 14 Februari. Wanabloga wachache wamemtakia heri rais katika mapenzi mapya aliyoyapata baada ya kifo cha mkewe Ethel miaka mitatu iliyopita.

30 Januari 2010

Marekani: Dkt. Martin Luther King, Jr. Akumbukwa

Martin Luther King Jr. alizaliwa tarehe 15 Januari, 1929 na akawa mmoja wa wasemaji na watetezi wakuu wa Harakati za Haki za Kiraia huko Marekani. Nchini Marekani, anaenziwa kwa sikukuu ya taifa, inayoadhimishwa kila mwaka siku ya Jumatatu ya tatu ya mwezi Januari. Leo, wanablogu wengi nchini Marekani wanaadhimisha kumbukumbu yake kwa kuandika makala za kumuenzi, huku wakiungalisha urithi wake wa masuala ya haki za jamii na masuala ya leo, wakionyesha wazi kuwa miaka 42 baada ya kuuwawa kwa King, maneno yake bado yana maana.

22 Januari 2010

Togo Yaondolewa Kwenye Mashindano ya Kombe la Afrika baada ya Shambulizi Baya

Timu ya Taifa ya Togo sasa imeondolewa rasmi kutoka kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kufuatia shambulizi lililoelekezwa kwa msafara wa timu hiyo Ijumaa iliyopita katika eneo la Kabinda lililo nchini Angola na ambalo liko kwenye ukanda wa mapigano baina ya vikosi vya serikali na vile vya waasi wanaotaka kujitenga. Huku kukiwa na shutuma nyingi kutoka kwenye serikali ya Angola na maafisa wanaosimamia soka barani Afrika, wanablogu wa Ki-Togo wanauliza maswali magumu kuhusu msiba huo.

13 Januari 2010