Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Aprili, 2015
VIDEO: Dunia Inasema #WanabloguZone9WaachiweHuru
Global Voices inakumbuka mwaka mmoja tangu kuwekwa kizuizini kwa wanablogu wa Ethiopia wa Zone9 kwa kutengeneza video hii ya kuwaunga mkono. Sema pamoja nasi: #WanabloguZone9WaachiweHuru!
Maisha ya Wakenya Yana Thamani, Wanafunzi wa Kiafrika Wasema Kwenye Ibada ya Kuwaombea Wahanga wa Garissa Jijini Beijing
Kikundi cha wanafunzi wa Kiafrika jijini Beijing waliandaa ibada ya kuwakumbuka wahanga 147 wa shambulio la Garissa pamoja na china kutokuwa na uvumilivu kwa watu wanaoomboleza hadharani
Filamu ya Malawi Yawasaidia Wakulima Kujikinga na Mabadiliko ya Tabia Nchi
Filamu ya “Mbeu Yosintha” ilitengenezwa kuwasaidia wakulima na wanavijiji kujikinga na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, hususani kubadilika kwa majira ya mvua kwenye ukanda wa Afrika Kusini Mashariki. Filamu...
Muswada wa Uhalifu wa Mtandaoni Unawapa Mamlaka Zaidi Polisi, Kuliko Wananchi
Wapinzani wakuu wa muswada huo kutoka kwenye asasi za kiraia wanasema wataipeleka serikali mahakamani kama rais ataidhinisha muswada huo kuwa sheria.
Afrika Kusini Imejitenga na Waafrika Wengine?
Mashambulizi ya hivi karibuni huko Afrika Kusini yanahusisha wahamiaji kupigwa, kuuawa, kuchomwa moto, wizi madukani pamoja na wizi wa mali zao. Watu watano wameshauawa, miongoni mwao akiwamo mvulana wa miaka 14 aliyeuawa siku ya jumatatu.
Je, Waganda Wameridhika na Utendaji wa Serikali Yao Kama Matokeo ya Utafiti Yanavyoonesha?
"Historia inatuambia kwamba watu HAWAKUI ili kuupenda na kuuenzi udikteta bali kinyume chake."
Mpigania Amani wa Uganda awa Miongoni mwa Watakaoshindania Tuzo ya Amani ya Nobeli
This is Uganda (ThisIs256) ni jukwaa la waandishi waliobobea kutoka Uganda walio na utayari wa kuandika habari makini za kuihusu nchi yao, wakilenga kutokomeza uanahabari uchwara, njaa, Ebola, ukabila, pamoja...
Namna ya Kuwafanya Wagonjwa wa Ebola Waone Nyuso za Wahudumu Wao Nchini Liberia
Fikiria kuwa hospitalini ukiugua maradhi yanayochukua maisha ya watu wnegi na huwezi kuona nyuso za wale wanaokuhudumia. Hicho ndicho kile ambacho Mary Beth Heffernan alijaribu kukibadili.
Upigaji Kura Unaendelea Tuzo za Blogu Nchini Kenya 2015
Sehemu ya kupiga kura kwenye Tuzo za Blogu Nchini Kenya inaendelea mpaka Aprili 30, 2015: Tuzo za Blogu Nchini Kenya hutafuta kuwatuza wanablogu wanaoandika mara kwa mara, wanaoandika madhui yanayosaidia,...
Mbali na Kusikia Habari za Boko Haram Nchini Niger, Fahamu Jangwa la Ténéré
Niger ipo katika vita na Boko Haram. Tusilisahau hili, hata hivyo, Niger ni mahali palipo na miradi mingi na pia ni eneo lililosheheni utajiri mwingi wa asili pamoja na ushairi.