· Septemba, 2013

Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Septemba, 2013

Boko Haram Waua Wanafunzi 50 wa Chuo Kikuu Nchini Naijeria

  30 Septemba 2013

Kikundi cha kigaidi cha Naijeria Boko Haram kimewawasha moto bwenini na kuwaua wanafunzi wasiopungua 50 wa Chuo Kikuu cha Kilimo kilichopo kwenye Jimbo la Yobe, wakiwa usingizini. Rais Goodluck Jonathan alitangaza hali ya hatari katika eneo hilo kufuatia mfululizo wa vitendo vya kigaidi.

Timu ya wanawake ya Mpira wa Kikapu ya Msumbiji Yafika Mbali

  29 Septemba 2013

Kufuatia ushindi wa kishindo kwenye mashindano ya robo fainali (tazama habari zetu ), yaliyofanyika usiku wa jana timu ya mpira wa kikapu ya Msumbiji, wanawake, ilishinda nafasi ya kuingia kwenye Fainali za Mashindano ya Afrobasket usiku wa leo dhidi ya washindi watetezi Angola. Kwa staili nyingine ya kurudi kwa ushindi...

Serikali ya Tanzania Yafunga Magazeti Mawili

  28 Septemba 2013

Serikali jana (terehe 27 Septemba, 2013) ilitangaza kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania kutokana na kuandika habari na makala zilizoelezwa zina nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola na kuhatarisha amani. Taarifa ya kufungiwa magazeti hayo ilisema; Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14)...

Picha Nyeusi: Waafrika Nchini Italia

  27 Septemba 2013

Picha Nyeusi ni kazi za wapiga picha watatu – Marco Ambrosi, Matteo Danesin na Aldo Sodoma – Kituo cha Stadi za Uhamiaji mjini Verona, Majiji ya Verona na Padua, Chuo Kikuu cha Padua Idara ya Sosholojia ikiwaonyesha Waafrika nchini Italia.

Daktari wa Peru ni Miongoni mwa Waathirika Waliopeza Maisha Westgate

  27 Septemba 2013

Shirika la Habari la Andina limearifu [es] siku ya Jumamosi, Septemba 21, 2013, kwamba daktari wa ki-Peru Juan Jesús Ortiz ni mmoja wa watu waliuawa katika shambulizi la kigaidi lililotokea katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, lilisababisha idadi ya vifo vya watu 59 na wengine 175 wakijeruhiwa. Hivi ndivyo Periodismo...