· Disemba, 2011

Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Disemba, 2011

Global Voices: Changia Leo

2011 umekuwa mwaka usio wa kawaida katika maudhui ya mtandaoni. Global Voices imekuwepo pale wakati mapinduzi yalipotokea, wakati tawala za kidikteta zikianguka, na matokeo ya matumizi ya mtandao yaliposambaa katika miji na mitaa ya wachangiaji wetu wanaoripoti kutoka duniani kote.

28 Disemba 2011

Zimbambwe: Hasira wakati Mzee Mugabe Anapowania Uchaguzi wa 2012

Chama cha ZANU –PF (Zimbabwe African National Union - Patriotic Front) kimempitisha Robert Mugabe kuwa mgombea wake kwa ajili ya uchaguzi wa rais unaotazamiwa kufanyika mwaka ujao. Kama uchaguzi utafanyika mwakani, Mugabe atakuwa na umri wa miaka 88 na atakuwa Mwafrika wa pili mzee zaidi kugombea katika uchaguzi wa rais. Kupitia Twita na Facebook wa-Zimbabwe wameonyesha hasira na kutokuamini kilichotokea.

15 Disemba 2011

Madagaska: Wajadili Uhalali wa Uwekezaji wa Kigeni wa Moja kwa Moja

Wakati Madagaska ikijaribu kutafuta suluhisho la matatizo ya muda mrefu ya kiasa, Wanablogu wa ki-Malagasi wanajadili thamani ya Uwekezaji unaofanywa Moja kwa Moja na raia wa Kigeni. Wa-Malagarasi wanaamini kwamba Madagaska, kama nchi nyingine za Kiafrika inao utajiri mkubwa wa rasili mali lakini tatizo likiwa ardhi yenyewe kupokonywa kwa sababu ya utawala mbovu na biashara zisizoangalia maslahi ya wananchi.

14 Disemba 2011

Zambia: Rais Sata Aituhumu Benki Kuu Kuchapisha Noti Bandia

Rais Michael Sata ameweka wazi kwamba Benki Kuu ya Zambia kwa maelekezo ya kilichokuwa chama cha Upinzani nchini humo MMD, ilichapisha “noti bandia” ambazo inasemekana ziko kwenye mzunguko wa fedha. Hata hivyo, Chama cha MMD kwa kupitia Waziri wake wa zamani wa Fedha Situmbeko Musokotwane, kimekana tuhuma hizo kikisema Benki Kuu inayo uhuru wa kuchapisha noti mpya za ziada bila kuwasiliana na Waziri wa Fedha ama Rais kwa sababu ina mamlaka kamili ya kufanya hivyo.

13 Disemba 2011

Afrika Kusini: Malema Ameng’oka, Nini Kinafuata?

Mwanasiasa na mtu ambaye husababisha utata zaidi ya wote nchini Afrika Kusini Julius Malema amesimamishwa uanachama wa chama cha ANC kwa miaka mitano. Malema anachukuliwa na mashabiki wake kama sauti ya dhati ya watu masikini wa Afrika Kusini hususani kwa wito wake kuhusu utaifishwaji wa migodi ya Afrika Kusini.

12 Disemba 2011