Habari Kuu kuhusu Madagaska
Habari kuhusu Madagaska
Utafiti wa Kwanza wa Kina Kuhusu Unyanyasaji wa Watoto Nchini Madagaska Unaonesha Hali Inatisha
Ripoti inasema asilimia 89 ya watoto wanadai kuathiriwa na unyanyasaji majumbani angalau mara moja wakati asilimia 30 ya vijana kinda wa kike katika Kisiwa cha Madagaska tayari wana mtoto.
Kwa nini Kila Mtu Nchini Madagaska Anafanyia Mzaha Mananasi
Mjadala wa Mananasi nchini Madagaska ni zaidi ya ujuavyo.
Huduma za Afya nchini Madagaska Zinaweza Kukabiliana na Mlipuko wa Ebola?
Nchi kumi na tano za Afrika ikiwemo Madagaska ziko kwenye hatari zaidi ya maambukizi ya Ebola kwa sababu zina mazingira yanayofanana na yale ya nchi zilizoathirika. Waziri Mkuu anasema Madagaska imejiandaa lakini wengine wana wasiwasi
Nzige Wavamia Mji Mkuu wa Madagaska
#valala pic.twitter.com/YHzOx5Q8QU — Vaintche Rahouli (@vincraholi) Agosti 28, 2014 Watumiaji-mtandao wa Twita na Facebook kutoka mji mkuu wa Madagaska, Antananarivo, wamepachika picha kadhaa za nzige wakivamia mji. Uvamizi wa nzige sio tukio la ajabu nchini Madagaska, hasa baada ya dhoruba za kitropiki, lakini sio kawaida katika miji mikubwa. Nzige wanaweza...
Mapigano ya Wanakijiji Kugombea Ardhi Yasababisha Maafa Nchini Madagaska
Blogu ya L'Express Mada ilitoa taarifa kwamba kijiji kizima cha Andranondambo kilichoko Kusini mwa Madagascar kiliharibiwa [fr] kufuatia mapigano ya wanakijiji yaliyosababishwa na mzozo wa kumiliki ardhi. Vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambayo ilidumu kwa siku tatu kati ya Mei 20-22, ilipoteza maisha ya wanakijiji wote. Akikumbuka tukio hilo, mmoja...
Serikali Mpya ya Waziri Mkuu Roger Kolo Yatangazwa Nchini Madagaska
Mtandao wa Tananews nchini Madagascar umechapisha orodha kamili ya mawaziri 31 wa serikali mpya ya Madagaska [fr]. Mitsangana Madagascar anasema kwamba orodha hiyo ina wanawake 6 na kuwa mawaziri 7 walikuwa kwenye baraza[fr] la serikali iliyopita ya mpito. Waziri mkuu wa zamani Beriziky aliitakia serikali kila la heri kwenye mtandao...
Kwa Nini Rais wa Madagaska Hajatangaza Uteuzi wa Waziri Mkuu
Rais mpya wa Madagaska Hery Rajaonarimampianina alichaguliwa kuwa raia mnamo Desemba 20, 2013. Miezi michache baadae, bado hajatangaza uteuzi wa waziri mkuu wa serikali yake mpya. Wachunguzi wengi wanashangaa kwa nini imechukua muda mrefu. Mwanablogu wa Kimalagasi Michael Rakotoarison ana maoni tofauti kuhusiana na hali hiyo; hoja yake ni kuwa huenda...
Twiti ya kwanza kutoka kwa Rais wa Madagaska
Rais mteule wa Madagaska Hery Rajaonarimampianina amefungua akaunti yake ya mtandao wa twita mnamo tarehe 23 Machi, 2014. Hii ndiyo twiti yake ya kwanza : Kuna uwezekano mkubwa kuwa hiyo ndiyo twiti maarufu kutoka kwa mkuu wa nchi. Ni Rupert Murdoch anaweza kuwa na wasiwasi na kiwango cha “ukubwa/umaarufu” wa...
Msichana Nchini Madagaska Ajiua Baada ya Picha Zake Kusambazwa Facebook
Koolsaina anaandika kwamba msichana mmoja wa ki-Malagasi alijiua [fr] baada ya picha zake kusambazwa kwenye ukurasa wa Facebook unaoonyesha picha za wasichana wa Madagaska bila ruhusa yao. Wito ulitolewa kwa utawala wa Facebook ulitolewa ili kuufunga ukursa huo. Mpaka leo (Machi 16, 2014), Koolsaina anasema ukurasa huo bado unapatikana.
Madagaska Bado Inasubiri Waziri Mkuu, Serikali Mpya
Mwezi mzima tangu Rais mteule Hery Rajaonarimampianina achaguliwe kuwa mkuu wa nchi nchini Madagaska, bado hakuna dalili nani atakuwa waziri mkuu na akina nani wataunda serikali. Ma-Laza anahoji kuwa suala kuu si hasa nani atakuwa waziri mkuu bali atakuwa ana ajenda gani akikabidhiwa ofisi [fr]: Un technicien hors pair, rassembleur,...