Kwa Nini Rais wa Madagaska Hajatangaza Uteuzi wa Waziri Mkuu

Rais mpya wa Madagaska Hery Rajaonarimampianina alichaguliwa kuwa raia mnamo Desemba 20, 2013. Miezi michache baadae,  bado hajatangaza uteuzi wa waziri mkuu wa serikali yake mpya. Wachunguzi wengi wanashangaa kwa nini imechukua muda mrefu. Mwanablogu wa Kimalagasi Michael Rakotoarison ana maoni tofauti kuhusiana na hali hiyo; hoja yake ni kuwa huenda rais kutulia si jambo baya sana [fr]: 

J’étais dans l’attitude ambiante de celui qui doute, moi qui de base n’ai jamais soutenu le Président [..]. De source sûr, le président missionne à l’étranger une poignée d’hommes discrets chargés de débusquer des compétences. Le pari est donc de dégager la politique, pour ne se soucier que de l’économie. 

 Nilikuwa mmoja wapo wa wale waliokuwa na mashaka hasa kwa sababu sijawahi kumwunga mkono Rais huyu […]. Hata hivyo taarifa za kuaminika ziliniambia kuwa Rais kwa sasa ametoa kazi hiyo kwa  kikundi kidogo cha watu kusaili kwa siri na kubaini watu ambao wanazo sifa zinazostahili. Changamoto ni namna ya kuachana na ushabiki wa kisiasa na kujikita kwenye masuala ya kiuchumi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.