Utafiti wa Kwanza wa Kina Kuhusu Unyanyasaji wa Watoto Nchini Madagaska Unaonesha Hali Inatisha

Enfants Malgaches par Yves Picq - CC-BY-SA-3.0

picha ya watoto wa Madagaskar na Yves Picq – CC-BY-SA-3.0

[ Habari hii iliandikwa na Andry R. Razafimbahoaka ambaye ni mwandishi aliyealikwa.na baadaye ikahaririwa na Global Voices kwa ufafanuzi na mazingira]

Tangu mkataba wa haki za mtoto ambao ulisainiwa mwaka 1991, Madagaska imeongeza jitihada za kutekeleza sera zinazolinda haki za mtoto na ilianzisha ndani ya nchi zaidi ya vituo vya mtandao 750 vya kuwalinda watoto tangu mwaka 2004. Pamoja na maendeleo haya, unyanyasaji, matumizi ya nguvu, unyanyasaji wa kingono na kazi za lazima bado ndiyo ukweli wa kutisha ambao hufanyika ndani nyumba. Kutokana na taarifa iliiyotolewa na nchi ya Madagaskar na UNICEF, kila sekunde mtoto wa Madagaskar hudai kufanyiwa unyanyasaji shuleni, na watoto tisa kati ya kumi wanakuwa wamepigwa na familia zao.

Ripoti ya kutisha ya UNICEF

Kutokana na ombi la serikali ya Madagaska, UNICEF ilifanya utafiti juu ya unyanyasaji dhidi ya watoto katika nchi hiyo. Matokeo ya utafiti huo yanatisha zaidi:

89% des enfants disent qu’ils ont été violentés physiquement un jour au sein de leur foyer. Et pourtant ils sont 72% à dire qu’ils se sentent en sécurité chez eux.

Asilimia 89 ya watoto wanadai kuwahi kuteswa nyumbani kwa kunyanyaswa kimwili angalau mara moja. Katika hao, asilimia 72 wanasema hawajisikii amani wakiwa nyumbani.

Ripoti inaonesha unyanyasaji duniani umejikita katika mila za jadi ambazo ni vigumu kuzihoji. Rajae Sbihi, ambaye ni mtaalamu wa saikolojia ya watoto alishiriki katika utafiti, alieleza:

La violence est considérée comme une méthode éducative, que ce soit dans le milieu familial ou à l’école

Unyanyasaji unachukuliwa kama njia ya kuwaelimisha wakiwa shuleni au nyumbani.

Jeunes filles malgaches par Hery Zo Rakotondramana on FlickR - CC BY-SA 2.0

Picha ya wasichana vijana wa mMadagaskar iliyopigwa na Hery Zo Rakotondramana on FlickR – CC BY-SA 2.0

Kutokana na Sbihi, watoto katika jamii za vijijini wapo katika hatari zaidi ya kunyanyaswa, alisema kwamba karibu asimilia 20 ya watoto wa madagaska hawakusajiliwa wakati wamezaliwa – hasa wanaoishi wilaya zilizopo mbali– hiyo huongeza unyanyasaji wao. Nguvu ya umma kiukweli ndiyo mara nyingi ni moja ya walinzi wa watoto waathirika wa unyanyasaji, na hasa inapotokea nyumbani. Aina hii ya unyanyasaji hupelekea vidonda vya kudumu, kiwewe, matatizo ya ukuaji wa mwili na kifikra, tabia hatarishi au kuacha kwenda shule pia.

Aina mbalimbali za unyanyasaji

Pamoja na unyanyasaji wa kutumia nguvu, kuna matukio mengi ambayo huzuia maendeleo ya watoto. Kwa kweli, 40% ya ripoti za vijana wa Madagaskar hufanya kazi kabla ya miaka 18. Laureate Rasolofoniainarison ambaye ni kiongozi wa kitaifa wa miradi katika ofisi ya OIT (kwa kiingereza ILO: Shirika la kazi la Umoja wa Mataifa)mjini Antananarivo,anaeleza namna unyanyasaji huu unavyoendeleza mzunguko wa umaskini :

les parents disent souvent qu’ils les envoient travailler au lieu d’aller à l’école parce qu’ils sont pauvres. En réalité c’est le fait de faire travailler leurs enfants qui les rend pauvres, en perpétuant un cycle dans lequel l’éducation et la possibilité de s’élever socialement n’ont aucune place.

Mara nyingi wazazi husema kuwa wanawatuma kufanya kazi badala ya kwenda shule kwa sababu wao ni maskini. Kiukweli, kuwafanya watoto wao kufanya kazi ndicho kinachowafanya kuwa maskini kwa kuendeleza mzunguko ambao elimu na kukua kijamii havina nafasi.

Vijana wa kike wapo katika hatari zaidi kwa unyanyasaji huu. Ndoa za utotoni ni sehemu ya mila za jamii za Madagaskar, na ni tatizo kwa watoto. Zaidi ya theluthi ya wasichana kati ya miaka 15 na 19 tayari wameolewa au wana mahusiano. Mabinti wachache hutumia njia za kuzuia mimba (ambao ni chini ya 8%) ambazo zinafikiriwa kuongeza idadi ya mimba zisizohitajika. Hakika, 30% ya mabinti katika kisiwa wana watoto. , kama ilivyoripotiwa na tathmini ya World Atlas ya mwaka 2015. Idadi hii imefikia hadi 50% katika baadhi ya sehemu za mji mkuu. Takwimu nyingine ya kutisha ni kuongezeka kiasi cha unyanyasaji wa ngono kwa wasichana kwa madhumuni ya biashara, hasa karibu na vituo vya mafuta na machimbo .

Zana mpya katika mapambano dhidi ya unyanyasaji

Kabla ya ripoti hii, mahitaji na haki za watoto vilikuwa havijuliakani katika Madagaskar. Hii ni ripoti mpya ambayo inaonekana kama zana ambayo inaruhusu uwakili wa kueleweka vizuri kulinda watoto , kuzuia, na kujibu hali hizi hatarishi. Pia, ni hatua ya kwanza kuelekea uundwaji makini wa sera ya taifa inayolenga kupunguza unyanyasaji. Pia, baadhi wanaona habari hii kama njia ya kushawishi baadhi ya watu. Inaweza pia kutumiwa kama zana ya kurejea katika kutoa hoja ili kuwashawishi watu kuacha mila na desturi ambazo zinaharibu watoto. Kwa ujumla, UNICEF imeajiri wanajamii wakujitolea 240 katika kisiwa kutoa msaada wa saikoljia, mazungumzo na uhamasishaji wa jamii.

Pia, UNICEF imeanzisha ushirikiano ili kuanzisha kanuni za maadili kwa ajili waajiriwa migodini na wakandarasi wadogo nchini Madagaskar katika jitihada za kumaliza unyanyasaji wa ngono kwa vijana wa kike. Hii mbinu ya utendaji inategemewa kuwa na matokeo endelevu kwa ajili ya ulinzi wao miaka michache ijayo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.