Linapokuja suala la mzaha mtandaoni, basi nanasi limekuwa kama chungwa jipya, angalau kwa nchi ya Madagaska.
Mitandao ya kijamii nchini Madagaska imejawa na mzaha wenye kibwagizo cha nanasi kwa siku kadhaa sasa. Kwa nini tunda hili lenye miiba miiba limekuwa na umaarufu wa haraka hivyo? Hii ni sehemu tu ya hali halisi katika jamii hiyo iliyo ndani ya kisiwa hicho Chekundu.
Madagaska inaonekana kuwa kati ya nchi masikini zaidi duniani baada ya Benki ya Dunia kuchapisha takwimu zake na (kuripotiwa na vyombo vya habari kama vile Radio France Internationale). Ukosoaji juu ya hali ya uchumi wa nchi haukumpendeza sana Rais wa Madagaska. Aliwaomba wachambuzi, vyombo vya habari na wananchi “ kutoa ushahidi unaoonesha kuwa nchi hiyo inaendelea kuwa masikini zaidi.”
Watumiaji wa mitandao ya kijamii wa ki-Malagasiharaka walilitazama suala hilo kwa namna rahisi:
Mbola tsy porofo ihany ve izao ry filoha #Madagascar #WASH https://t.co/7RzRNRO9vk
— Touti Rakotonirina (@strakotonirina) May 28, 2016
Je takwimu hizi si ushahidi unaojitosheleza Mheshimiwa Rais? #Madagascar #WASH
Koolsaina, Blogu ya kijamii ya Malagasi ilibandika picha ifuatayokatika tovuti yake:
Kufuatia majibizano makali yaliyotokea baina ya Rais na mitandao ya kijamii ya Malagasi, tovuti nyingine ya kijamii, Tananews, ilibandika picha ya mke wa Rais Voahangy Rajaonarimampianina akiwa amevaa nguo ya kijani ikiwa na urembo wenye picha ya nanasi kwa mbele:
Tananews waliweka ukurasa mwingine ukiwa na maneno ya mzaha yaliyosema, “Hakika, sio kila mtu ni maskini hapa Madagaska.” Katika ukurasa huo walionesha gauni alilovaa mke wa Rais lililobuniwa na kampuni kubwa ya ubunifu wa mavazi ya Dolce & Gabana na linauzwa dola $7,745 katika tovuti ya idara ya mauzo Nieman Marcus (hakuna uhakika kama hiyo ndio bei halisi ya gauni hilo alilovaa mke wa Rais).
Kulitokea ghadhabu ya ghafla katika mitandao wa intaneti nchini humo. Mafuriko ya utani huo wenye alama ishara ya #mananasi yameendelea kwa siku kadhaa ndani ya tovuti mbalimbali na mitandao ya kijamii ya Malagasi. Hii ni baadhi tu ya mizaha iliyotumiwa na kuenezwa kwa wingi:
Kwa bahati mbaya, mizaha yote iliyohusu nanasi ilikuja baada kutokea tukio la kutisha katika sherehe za siku ya Uhuru wa nchi hiyo; ambapo, bomu la kurushwa kwa mkono lililipuka wakati wananchi wakiangalia gwaride la kijeshi katika uwanja wa Taifa,na kuua watu watatu na wengine 91 walijeruhiwa. Hii ni video ya tukio hilo
Majadiliano yote ndani ya “Pineapple-Gate” yamekuja katika kipindi muhimu ambapo muswada wa sheria ya uhuru wa kujieleza na maadili mtandaoni unaandaliwa na mamlaka za Malagasi. Wakizungumzia hilo vyanzo vya ndani vinatonya na kuzungumzia jinsi muswada huu utakavyobana uhuru wa kujieleza mtandaoni na utakuwa na faini kubwa kwa makala au taarifa zozote zitakazoonekana kuwa ni za uongo. Muswada huo utakabidhiwa bungeni wiki chache zijazo kwa ajili ya kupitishwa.