Nani Jansen Reventlow na Rasha Abdulla waungia kwenye bodi ya Global Voices

Nani Jansen Reventlow (Kushoto), Dk. Rasha Abdulla (Kulia). Picha ya Nani Jansen Reventlow iliyopigwa na Testuro Miyazaki, imetumika kwa ruhusa. Picha ya Dk. Rasha Abdulla haki miliki ya Rasha Abdulla.

Global Voices inayofuraha kutangaza kujiunga kwa wanachama wawili mahiri wapya kwenye  bodi yetu ya wakurugenzi.

Nani Jansen Reventlow ni mwanasheria wa kimataifa mwenye mafanikio makubwa na pia mtaalam kushughulikia masuala ya haki za binadamu kwa kuweka vigezo vya uhuru wa kujieleza kwenye mataifa mbalimbali duniani. Ni Mkurugenzi mwanzilishi wa Mfuko wa Haki za Kidijitali, unaowasaidia washirika wake barani Ulaya kukuza haki za kidijitali kupitia hatua za kimkakati. Nani ni Mhadhiri wa Sheria katika Shule Kuu ya Sheria ya Columbia na ni Profesa wa Shule Kuu ya Utawala ya Chuo Kikuu cha Oxford. 

Dr. Rasha Abdulla ni Profesa wa Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma katika Chuo Kikuu cha Kimarekani Cairo. Tafiti zake zimejikita kwenye mitandao ya kijamii na uhamasishwaji, tofauti zilizopo kwenye vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza, na uhariri wa maudhui. Ni mwanachama wa zamani wa Timu ya Ushauri wenza ya Umoja wa Mataifa kuhusu Jukwaa la Utawala wa Intaneti  (IGF MAG) na mwandishi wa vitabu nane ikiwamo, “Intaneti kwenye Nchi za Kiarabu: Misri na kwingineko,” pamoja na makala za kitafiti, ripoti na sura alizochangia kwenye vitabu. Tafiti zake kuhusu mitandao ya kijamii na harakati za kisiasa zilizopelekea mapinduzi ya Misri zimemletea ushindi wa tuzo kadhaa za kitafiti, ikiwa ni pamoja na ile inayofahamika kama AUC Excellence in Research Award [Tuzo ya Ubora kwenye Utafiti ya AUC]. 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.