Fomu ya Kuomba Kuwa Mtafsiri

Mradi wa Lingua wa Global Voices unakuza habari zinazoandikwa duniani kote na waandishi wa kujitolea wakishirikiana na wafasiri. Mradi huu unafungua mlango wa mawasiliano kati ya wanablogu na wasomaji wa mtandao wa Global Voices wasiozungumza Kiingereza kwa kutafsiri maudhui hayo katika lugha 40+.

Tunakaribisha watu wanaoweza kujitolea kutafsiri maudhui haya kuwa moja wapo ya lugha zetu, au hata kushirikiana na waandishi wetu kuandika habari, Kama wewe si mtafsiri, kuna namna nyingi zaidi unazoweza kusaidia!

Tuna jamii ya watu wanaojitolea zaidi ya 500 duniani kote. Ili kujiunga na timu yetu, unachohitaji kufanya ni kujaza fomu hii ya maombi. Mhariri anayehusika anawasiliana na wewe kwa hatua zinazofuata.

Kama lugha yako haionekani kwenye fomu hii hapa chini, tumia lugha/tafsiri husika kulia mwa makala haya.

Tunasikitika kuwa kwa sasa hatupokei watafsiri wa Kiingereza. Tunakaribisha wachangiaji wanaoweza kufanya vyote viwili kwa pamoja, kutafsiri na kuandika makala zinazotoa habari kwa nchi wanazozipenda wao au wana kiwango kizuri cha utaalamu. Kama hilo linawezekana kwako, tafadhali tumia fomu hii ya maombi badala yake.