Global Voices ni jamii ya wanablogu zaidi ya 200 waliopo duniani kote ambao wanafanya kazi kwa pamoja kukuletea tafsiri na ripoti za yanayojiri kwenye ulimwengu wa blogu na uandishi wa kiraia, Global voices ina paaza sauti ambazo kwa kawaida huwa hazisikiki katika vyombo vya habari vya kimataifa.
Global Voices inakusanya, inapanga, na kurusha hewani mazungumzo ya kwenye mtandao wa intaneti – inaangazia sehemu na watu ambao mara nyingi vyombo vya habari huwapuuzia. Tunafanya kazi kuendeleza zana, asasi na mahusiano ambayo yanasaidia sauti zote, kutokea kila mahali, kusikika.
Mamilioni ya watu wanablogu, wanatangaza kwa kutumia mtandao wa intaneti, na wanaweka picha, filamu za video na habari, bila ya kujua ni wapi pa kuzipata habari hizo, inaweza ikakuwia vigumu kuzisikia sauti zenye kuheshimika kati ya hizo. Timu yetu ya kimataifa ya waandishi wa kujitolea na wahariri ni washiriki hai katika ulimwengu wa blogu wanaouwakilisha.
Global Voices imesajiliwa nchini Uholanzi kwa jina la Stitching Global Voices, kama asasi isiyo ya kibiashara. Hatuna ofisi, lakini tunafanya kazi kama jamii ya kwenye mtandao, na hukutana pale tu nafasi inapojitokeza (kwa kawaida wakati wa mikutano mikubwa). Tunategemea ufadhili, kazi mbalimbali za kulipwa na michango ili kulipia gharama zetu.
Miradi Yetu
Global Voice inatafsiriwa na wafasiri wa kujitolea katika lugha zaidi ya 15 ambao wameunda mradi wa Lingua. Kadhalika Global voices inayo tovuti ya Utetezi na mtandao unaosaidia watu ambao sauti zao huchujwa kuongea wazi mtandaoni. Pia tunao mradi wa Rising Voices unaosaidia watu au jamii zilizotengwa kutumia uandishi wa kiraia ili kusikika, mradi huu unatilia mkazo nchi zinazoendelea.
Soma zaidi kuhusu miradi yetu.