Habari Kuu kuhusu Habari za wenyeji
Habari kuhusu Habari za wenyeji
Ujerumani yakiri kuhusika na mauaji ya kimbari nchini Namibia enzi za ukoloni, lakini wahanga wasema haitoshi
Miaka zaidi ya 100 baada ya mauaji ya kimbari ya watu wa kabila la Ovaherero na Nama nchini Namibia, Ujerumani inakiri kuhusika kwake na itatoa fedha kufadhili miradi nchini Namibia kwa kipindi cha miaka thelathini.
Kwa nini Wakolombia Wazawa Wanaandamana Dhidi ya Rais Ivan Duque?
Wazawa Kolombia wameratibu maandamano ya kitaifa kupinga mpango mpya wa maendeleo wa Rais Duque wakiunganisha nguvu na Wakolombia weusi, wakulima, wafanyakazi na wanafunzi .
Wanaharakati Nchini Colombia Wawasilisha Barua Kuhusu Mauaji ya Viongozi wa Kijamii Huko ICC
Zaidi ya viongozi 163 wa kijamii na wanaharakati wameuawa kwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita nchini Colombia.
Kutana na Vijana wa Ecuado Wanaoendesha Kipindi cha Kwanza cha Lugha ya ki-Chwa Radioni Nchini Marekani
“Kipindi hiki kinahusu kujieleza na bila kuogopa kufanya hivyo.”
Michoro Yaonesha Harakati za Raia wa Ufilipino Wakipambana na Ukandamizaji
Nchi ya Ufilipino ina idadi ya raia wazawa wanaokadiriwa kufikia milioni 14. Wengi wa raia hawa wanaoishi maeneo ya vijijini wapo katika hatari kubwa ya kuathiriwa na uharibifu unaotokana na shughuli za uchimbaji madini, harakati za utafutaji maendeleo pamoja na matumizi ya nguvu za kijeshi.
Wanaharakati Waomba Ulinzi kwa Makabila Yanayopinga Uchimbaji Madini Nchini Ufilipino
"Wao ndio waasisi wa tamaduni zetu za kipekee za sanaa. Mauji dhidi yao ni mauji ya utu wa watu wetu."
Mradi wa Video Waelezea Mapambano ya Kimaisha ya Watu wa Papua ya Magharibi
"Hizi ni habari tofauti na zile za mgogoro uliopo: Harakati za kupata elimu, mazingira, usawa na utu."
Shiriki Zoezi la Kujifunza Lugha za Asili Mtandaoni
Badala ya zoezi la kuweka mabonge ya barafu vichwani mwao, watetezi hawa wa lugha wamekubali kushiriki zoezi la lugha za asili kwa njia ya video
Filamu Yaonesha Namna Kabila Dogo Linavyojaribu Kuwazuia Wakata Misitu Kuharibu Mazingira
Sunset Over Selungo ni filamu ya dakika 30 inayoonesha namna kabila la wenyeji la Penan linavyopigania kutunzwa kwa misitu ya asili kwenye kisiwa cha Borneo nchini Malaysia. Borneo ni kisiwa kikubwa zaidi barani Asia. Filamu hiyo imetengenezwa na mtayarishaji huru wa filamu wa Kiingereza, Ross Harrison
Maktaba ya Digitali ya Tiba Asilia Nchini Ufilipino
Ikiwa imeanzishwa na mamlaka kadhaa za kiserikali, Maktaba Dijitali ya Elimu ya Tiba za Jadi Ufilipino (TKDL-Health) inalenga kuweka kumbukumbu na kufanya masuala ya tiba za jadi kuwa za kidijitali nchini humo. Jamii, ambazo nyingi ni zile za miliamni au majirani zao, zimekuwa zikitegemea miti na mazao mengine ya asili...