Michoro Yaonesha Harakati za Raia wa Ufilipino Wakipambana na Ukandamizaji

'Land Grab'. Federico Boyd Sulapas Dominguez uploaded this painting in time for the Asia-Pacific Economic Cooperation Summit which will be held in the Philippines.  Reposted with permission

“Ukwapuaji wa Ardhi”. Federico Boyd Sulapas Dominguez alipakia mchoro huu wakati wa kuelelekea kwenye kongamano la Ushirika wa Kiuchumi la Asia-Pacific linalotarajiwa kufanyika nchini Ufilipino. Imerudiwa kuchapishwa kwa ruhusa

Kwa kipindi cha miaka 40 iliyopita, msanii wa Kifilipino Federico Boyd Sulapas Dominguez amekuwa akiandaa picha zinazoonesha harakati za wazawa katika kukomesha uchimbaji madini wa uharibifu, utafutaji maendeleo usiojali haki, pamoja na matumizi ya nguvu za kijeshi. Lengo lake ni kuifahamisha jamii kuhususiana na masaibu yaikumbayo jamii ya watu waishio Ufilipino pamoja na harakati zao za kulinda ardhi waliyorithishwa na mababu zao.

Ufilipino ina zaidi ya wakazi wazawa milioni 14 ambao huzungumza lugha zaidi ya 110 za kikabila. Hata hivyo, urithi huu wa aina yake unahatarishwa na ongezeko la haraka la miji, harakati za kibiashara pamoja na uporaji wa ardhi yao kupitia shughuli zinazopewa baraka zote na serikali zikiwamo zile za kilimo, uvunaji miti na uchimbaji wa madini.

Katika kisiwa cha Mindanao, kilichopo kaskazini mwa Ufilipino, jamii ya watu wa huko hujulikana kwa jina la lumad. Makundi anuai ya Lumad ambayo yanapinga kuingiliwa na makampuni ya uchimbaji madini yamejitokeza kwenye vyombo vya habari kati ya miezi ya Septemba na Oktoba 2015 mara baada ya kushambuliwa na makundi ya watu mithili ya wanajeshi. Takribani watu 700 wa jamii ya Lumad wameweka kambi jijini Manila, mji mkuu wa Ufilipino, kwa ajili ya kushinikiza kuondolewa kwa wanajeshi kwenye makazi yao.

Malalamiko ya Lumad yanaonekana sana kwenye kazi nyingi za Federico. Amekuwa pia akipakia nakala ya kazi zake za zamani katika ukurasa wake wa Facebook ambazo anaziona kama bado zina manufaa kufuatia kuvamiwa kwa jamii ya Lumad na matukio ya mfululizo ya kurubuni mali asili zilizopo kwenye maeneo ya urithi ya makabila haya. Baadhi ya michoro yake tayari imeshasambazwa kwa kiasi kikubwa kwenye mitandao ya kijamii na wanaharakati, wanazuoni pamoja na watetezi wa masuala ya urithi ambao wanalenga kuhamasisha jamii kusaidia jamii ya lumad kupata haki yao.

Federico, ambaye ni wa kabila la Mandaya (Jamii ya wazawa wa lumad kutoka Mashariki ya Mindanao), anawahamashisha wasanii wachanga kuongeza maaarifa yao kuhusu utamaduni wa Ufilipino kwa kujumuika na jamii za wazawa.

Ifuatayo ni baadhi ya michoro ya Federico:

"Talabok" is a Lumad Matigsalog term for social gathering or market day. Artwork by Federico Boyd Sulapas Dominguez reposted with permission

“Talabok” ni neno la Lumad Matigsalog linaloashiria kusanyiko la kijamii au siku ya gulio. Mchoro na Federico Boyd Sulapas Dominguez. Imerudiwa kuchapishwa kwa ruhusa

This artwork by Federico Boyd Sulapas Dominguez depicts the impact of militarization in the hinterlands. Reposted with permission

Mchoro huu ulioandaliwa na Federico Boyd Sulapas Dominguez waonesha madhara ya matumizi ya nguvu ya kijeshi katika ardhi ya wazawa wa maeneo ya vijijini. Imerudiwa kuchapishwa kwa ruhusa

Aside from exposing the negative impact of militarization, the painting also shows how government laws unfairly discriminate against the Philippines' ethnic communities. Painting by Federico Boyd Sulapas Dominguez, reposted with permission

Mbali na kuweka bayana athari za matumizi ya nguvu za kijeshi, michoro yake pia inaonesha namna ambavyo sheria za nchi zinavyobagua jamii za makabila ya nchini Ufilipino. Imechorwa na Federico Boyd Sulapas Dominguez. Imerudiwa kuchapishwa kwa ruhusa

"Lupa ay Buhay" means "Land is Life". "Kapayapaan" means Peace. The text at the borders of the painting reads: Respect the rights of indigenous peoples and their right to self-determination. Painting by  Federico Boyd Sulapas Dominguez, reposted with permission.

“Lupa ay Buhay” inamaanisha “ardhi ni maisha”. “Kapayapaan” inamaanisha amani. Maandishi chini ya mchoro yanasomeka: Heshimu haki za raia wazawa na haki yao ya kusimamia mambo yao. Imechorwa na Federico Boyd Sulapas Dominguez. Imerudiwa kuchapishwa kwa ruhusa.

'Tagaynop' is a lumad Mandaya term for nightmare. Artwork by  Federico Boyd Sulapas Dominguez, reposted with permission

“Tagaynop” ni neno la lumad Mandaya likiwa na maana ya jinamizini. Imechorwa na Federico Boyd Sulapas Dominguez. Imerudiwa kuchapishwa kwa ruhusa

'Yalingkawas' is a lumad Mandaya term for freedom or freed. Artwork by  Federico Boyd Sulapas Dominguez, reposted with permission

“Yalingkawas” ni neno la lumad Mandaya likiwa na maana ya uhuru. Imechorwa na Federico Boyd Sulapas Dominguez. Imerudiwa kuchapishwa kwa ruhusa

'Mandayuman' is a lumad Mandaya term for where people live. A mini mural showing two major rituals of two different groups. Right part are the Lumad Mandaya (Balilig) and on the left are the Lumad Matigsalog (Panubad tubad). Artwork by  Federico Boyd Sulapas Dominguez, reposted with permission

“Mandayuman” ni neno la lumad Mandaya lenye maana ya mahali watu wanapoishi. Mchoro mdogo ukionesha aina mbili za matambiko ya jamii mbili tofauti. Upande wa kulia ni Lumad Mandaya (Balilig) na kushoto ni Lumad Matigsalog (Panubad tubad). Imechorwa na Federico Boyd Sulapas Dominguez. Imerudiwa kuchapishwa kwa ruhusa

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.