Wanaharakati Nchini Colombia Wawasilisha Barua Kuhusu Mauaji ya Viongozi wa Kijamii Huko ICC

Picha za skrini za video iliyochukuliwa wakati wa maandamano ya Paris Machi 28. Mwandamanaji akiwa amebeba bango linalosema “wamemuua rafiki yangu” na akiandamana  pembeni ya orodha ya majina ya wahanga. Video imeshirikishwa huko YouTube na Agence France Press kwa Kihispania.

Aprili 5, kikundi cha WaColombia wapatao 20 na umoja wa wanaharakati umewasilisha ombi rasmi kwa mahakama ya Kimataifa ya makosa ya jinai (ICC) kupeleleza uhalifu kuhusu mauaji makubwa ya viongozi wa kijamii nchini mwao.

Umoja huo na wanaowaunga mkono wamewasilisha barua wenyewe huko The Hague baada ya kuandamana kwa juma moja huko Paris huku wakisimama katika miji tofauti tofauti ya Ufaransa na Ubelgiji katika njia zote walizokuwa wakiandamana.

Picha inayofuata ni ya kusanyiko lililofanyika huko Paris:

Heshima kwa ajili ya viongozi wa kijamii 472 waliouawa nchini Colombia, watembeaji kuelekea The Hague wametengeneza bango la kitambaa lenye majina yao wote. Tunaamini serikali ina mambo ya kutosha kuhusu sera yao ya ulinzi na idadi hii haitaendelea kuongezeka.

Maandamano yalianzishwa na Umoja wa Wacolombia walio Uholanzi  na vikundi vingine kuunga mkono baadaye.

Washiriki walitumia hashitagi #MarchamosALaHaya (Kuandamana kuelekea The Hague) na #MarchamosALaHaya5abril (Kuandamana kuelekea The Hague Aprili 5) kueneza taarifa kuhusu mpango huo.

Wanasiasa wa Colombia Gustavo Bolívar na Antonio Sanguino wameonesha kuunga mkono maandamano hayo. Seneta Gustavo Petro, ambaye alipoteza kinyang'anyiro cha urais 2010 na 2018 pia alishiriki maandamano hayo kupitia taasisi yake ya “Colombia Humana” (Binadamu wa Colombia).

Video ya Adriaan Alsema, mwanzilishi wa chanzo cha habari mtandaoni Colombia Reports, ikionesha baadhi ya picha za maandamano yaliyopita ambayo yalifanyika ndani na nje ya Colombia dhidi ya mauaji ya viongozi wa kijamii. Pia ilihusisha maelezo mafupi kuhusu tatizo hili.

Zaidi ya viongozi wa kijamii 163 na wanaharakati — wanaofahamika kama líderes sociales nchini Colombia — wameuawa kwa kipindi cha miaka mitatu na hii ni kulingana na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu – Umoja wa Mataifa.   Mpelelezi wa serikali ya Columbia ana idadi kubwa zaidi ya mauaji 460 tangu mwaka 2016.

Kwa namna yeyote idadi ya vifo vya kikatili imepaa tangu 2016 ulipofanyika mkataba wa amani ambao kwa sehemu kubwa ukimaliza mgogoro uliodumu nchini kwa kipindi kirefu baina ya serikali na kikundi cha waasi cha FARC.

Moja kati ya maelekezo yaliyowekwa na Mkataba wa amani ni kuwa FARC watakabidhi mali zao zote huku wakipewa nafasi za ushiriki katika taasisi za kisiasa.

Lakini FARC wameacha ombwe la mamlaka tangu waachie maeneo yao ya zamani ambayo kwa sasa yanashikiliwa aidha na vikundi vya wanamgambo na waasi ambao hawakubaliani na mchakato wa amani.

Viongozi wa kijamii wanalengwa kwa sababu wanatetea jamii zao dhidi ya vikundi hivyo ambavyo mara nyingi huongozwa na wauza dawa za kulevya au wachimbaji haramu wa madini katika maeneo wanayoyashikilia.

Kulingana na Carlos Guevara, ambaye anaongoza taasisi ya “Somos Defensores” (sisi ni walinzi),  mara nyingi viongozi wa kijamii huuawa wakiwa majumbani mwao, mbele ya familia zao na mara zote hukosa msaada kutoka kwa mamlaka wanapotafuta haki:

…las agresiones contra personas que se dedican a defender de los derechos humanos en Colombia [está al nivel de] una crisis humanitaria […] los están matando porque están impulsando quitar una economía considerada ilegal y que beneficia a los narcotraficantes y grupos armados. Y el Gobierno no está tomando medidas para proteger a esos líderes…

Ukatili dhidi ya watu waliojitolea kutetea haki za binadamu nchini Colombia umefikia viwango vya janga la kibinadamu, wamekuwa wakiuawa kwa sababu ya kupambana katoka katika uchumi ambao ni haramu na unaowanufaisha wauzaji wa dawa za kulevya na vikundi vya wanamgambo wenye silaha. Serikali haichukui hatua yoyote kuwalinda viongozi hao…

Wakati huo huo, Kongamano la kitaifa la taasisi za Kicolombia ilionesha jambo la msingi kuhusu mauaji hayo ambalo limekuwa likiwekwa pembeni: ukweli kwamba viongozi wengi wa kijamii wanatoka katika jamii zisizo na watu wengi.

Kwa kuongezea, viongozi wanawake wanateseka zaidi kwa kuwepo kwa tabaka lingine la ukatili, kwa sababu wanahusishwa na aina nyingine za ukatili unaolenga jinsia.

Mtandao wa twita nchini Colombia mara zote hutumia hashitagi ya #NosEstánMatando (wanatuua) kwa sababu ya kuzungumzia mauaji ya viongozi wa kijamii. Kwa maandamano ya kwenda ICC wanaharakati wanatarajia kuamsha mtazamo wa kimataifa kuhusu hatma yao.

Wakati huo huo, idadi inaendelea kuongezeja tangu kuanza kwa mwaka 2019, viongozi 73 wameshatishiwa katika eneo la idara ya Boyacá pekee.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.