- Picha na: Max Pixel, chini ya CC0 Public Domain leseni.
Hapo Agosti 17, kundi la wadukuaji wasiojulikana lilishambulia maktaba ya wizara ya Afya ya Nicaragua. Mafaili 400 yaliyowekwa wazi yalionesha kwamba kuna ongezeko la visa 6,245 vya wagonjwa wa COVID-19 nchini Nicaragua ambavyo hapo awali havikuwa vinafahamika kwa umma. Tangazo hili lilitolewa huko Twitter na mtu aliyejulikana kama Lorian Syrano, mwanachama wa kundi la wasiojulikana.
Wanicaragua waliopo Twitter walijibu kwa shauku kubwa udukuaji kwa hashitagi ya #OpNicaragua. Tangu mwanzo wa janga hili mamlaka za Nicaragua ziliamua kuficha taarifa za COVID-19 na pia walikataa kufungia watu ndani.
Mtu asiyejulikana alidhihirisha kwamba mpaka mwezi Mei idadi ya watu waliopimwa na kukutwa na COVID-19 ilikuwa ni kwa asilimia 98.80 zaidi ya idadi ile maofisa wa Wizara wanatangaza: visa 1332 badala ya 16. Namna hiyo imeendelea kwa miezi iliyofuata. Mpaka Julai 24, ilionekana kwamba jumla ya visa 6,245 vya maambukizi havikuripotiwa kwa umma.
Pia imeonekana kwamba kasi ya ongezeko la idadi ya maambukizi kwa kila kipimo ni kubwa sana duniani, ambapo karibu asilimia 56 ya vipimo inarudi ikionesha wana maambukizi ya COVID-19. Mkurugenzi wa zamani wa Kitengo cha magonjwa ya mlipuko katika wizara ya afya Álvaro Ramírez, alifafanua wakati akihojiwa na Usiri kwamba ni kwa sababu vipimo vinafanyika kwa watu waliolazwa mahospitalini au wale wenye dalili za maambukizi.
Tayari kabla ya udukuaji huo, mashaka juu ya uhakika wa taarifa rasmi ya takwimu za maambukizi ya COVID-19 yalikuwa yameongezeka. Kwa mfano uchunguzi wa kujitolea ulifanywa na wataalamu wa afya, watafiti, wahandisi, wataalamu wa sayansi ya kompyuta na mawasiliano iliripotiwa kwamba idadi ya vifo vinavyohusishwa na COVID-19 ni mara ishirini zaidi ya taarifa zilizotolewa na Wizara ya Afya.
Kwa mujibu wa Álvaro Ramírez, taarifa zilizovujishwa zinathibitisha kwamba serikali ilikuwa ikificha taarifa kwa makusudi. Alisema:
…el hecho de que esta información estaba ahí, que llegaba todos los días a la presidencia, y que por cualquier razón, que no la vamos a entender fácilmente, ellos (Daniel Ortega y Rosario Murillo) decidieron mentir a la población, y cambiar los datos, y poner datos diferentes.
… ukweli ni kwamba taarifa hizi zilikuwepo pale na zilikuwa zikiifikia ofisi ya Rais kila siku na kwa sababu yoyote ile ambayo hatutaielewa kirahisi, wao (Daniel Ortega na Rosario Murillo) wameamua kuudanganya umma na kubadilisha takwimu na kuweka takwimu za uongo.
Serikali inayoongozwa na Rais Daniel Ortega na mkewe na Makamu wa Rais Rosario Murillo, ilithibitisha hapo Mei kwamba watu walikuwa wakiugua nimonia badala ya COVID-19. Mwezi Mei na Juni taarifa ya kutahadharisha kuhusu maziko ya siri yaliyokuwa yanafanyika ilisambaa. Mwanahabari Lucydalia Baca Castellón alitumaini kwamba masharti ya mikopo ya Kimataifa ingeilazimisha serikali ya Nicaragua “kuchukua hatua za haraka na za uwazi” kuhusu janga la COVID-19.
Mnamo Agosti 16, Mtu asiyejulikana alifanya mzaha kuhusu taarifa zilizovujishwa:
#Anonymous #OpNicaragua #SOSNicaragua #Nicaragua
Salamu kwa uongozi wa kidikteta wa Ortega. Tunaweza kuwa nje ya rada kwa muda kidogo lakini mapambano dhidi ya uhuru wetu hayajakoma.
Wizara ya Afya ya Nicaragua #Imevamiwa! Taarifa zilizodukuliwa zinakujia hivi karibuni pic.twitter.com/jjlOPDQySj
— CyberWare – Anonymous (@LiteMods) August 16, 2020
Asiyejulikana, kama mpinzani wa serikali, wachambuzi na vyombo vya habari vya Nicaragua, vimekuwa vikiita serikali ya Ortega kama “serikali ya kidikteta” kwa sababu ya tabia za mabavu, ufinywaji wa haki na rushwa. Kulingana na taarifa ya kikundi cha wataalamu kutoka kada mbalimbali Ortega amefanya uhalifu mwingi dhidi ya utu, dhidi ya mahasimu wake wa kisiasa hasa wakati wa vuguvugu la kuipinga serikali hapo 2018.
Hapo Agosti 21, Lorian Synaro alishirikisha wavuti ambayo ilisema kwamba taarifa zote za wizara ya Afya ya Nicaragua na mafaili mengine 400 yanaweza kupakuliwa hapo:
#Anonymous #OpNicaragua #SOSNicaragua #Nicaragua
Wizara ya Afya ya Nicaragua imeshambuliwa!! Taarifa lukuki za siri, nyaraka na mfumo mzima umewekwa wazi. Uongo wa serikali hautabaki kuwa siri tena.
Pakua —> https://t.co/e5knY4mw0y
*Soma bandiko hapo chini pic.twitter.com/SSxTWK9Qll
— Lorian Synaro ? (@LorianSynaro) August 21, 2020
#Anonymous #OpNicaragua #Nicaragua #SOSNicaragua
Benki Kuu ya Nicaragua, wizara ya uchumi na tovuti ya serikali ya UAF zote zilifumuliwa. #Offline!https://t.co/EbKGPTs3qMhttps://t.co/dBiIKebLawhttps://t.co/tomII3AMat pic.twitter.com/n8OOZqnjaC
— Lorian Synaro ? (@LorianSynaro) May 14, 2020
Chombo kikuu cha habari El 19 Digital, ambacho kina mahusiano ya karibu na serikali hakijaripoti chochote kuhusu matukio haya pamoja na kuwepo kwa habari zinazohusiana na Wizara ya afya. Pia Wizara ya afya nayo haikusema chochote kuhusu mashambulizi hayo.