Rajisi ya Usajili wa Watumiaji wa Simu za Mkononi Nchini Mexico Yazua Hofu Kuhusu Haki ya Faragha

Mexico imepitisha mpango wa kusajili taarifa za kinasaba, majina, na anuani za watumiaji wa simu za mkononi katika kanzidata, huku wanaharakati wakionesha mashaka yao kufuatia uamuzi huu. Katika nyakati tofauti, serikali ya Mexico ilishaonesha kushindwa kutunza taarifa binafsi za watu.

Seneti ya Jamhuri ya Mexico iliidhinisha na kisha, mapema Aprili 16 kuchapisha sheria ya maboresho ya Sheria ya Mawasiliano na Utangazaji ya nchini Mexico inayoruhusu kuanzishwa kwa Rajisi ya Kitaifa ya Watumiaji wa Simu za Mkononi (Padrón Nacional de Usuarios de Telefonía Móvil, PANAUT, kwa Kispaniola).

Rajisi hii ni kanzidata inayojumuisha taarifa kuhusu watumiaji wa huduma za simu zinazotolewa na makampuni ya simu. Sheria hii inaeleza:

Usajili wa namba za simu katika rajisi ya Kitaifa ya Usajili wa Watumiaji wa Simu za Mkononi itakuwa ni jambo la lazima kwa watumiaji wote, na watalazimika kutoa taarifa za utambulisho rasmi, mahali wanapoishi, na taarifa za vinasaba kabla huduma za simu kuwezeshwa kwa mtumiaji husika. (…)

Hii inamaanisha, watumiaji wa simu za mkononi nchini Mexico wanapaswa kusajili laini zao za simu sambamba na kuweka wazi taarifa zao binafsi na taarifa za vinasaba kama vile alama za vidole na sura. Mitandao ya simu ndio itakayokuwa na wajibu wa kukusanya na kuhifadhi taarifa hizi. Inakadiriwa kuwa, uandaaji wa rajisi hii utagharimu kiasi cha Pesos milioni 700 , au & dola za Kimarekani milioni 35.4.
Kwa mujibu wa Bunge la mexico, uhalali wa mabadiliko haya ya sharia unatokana na “mashauriano baina ya mamlaka zenye weledi wa masuala ya usalama na haki katika masuala yenye mrengo wa makosa ya jinai.” Kwa mujibu wa taarifa za serikali, hadi kufikia mwaka 2019, inakadiriwa kuwa watu milioni 22.3 walikuwa wahanga wa makosa mbalimbali. Uimarishaji wa Achieving “ amani na ulinzi“ilikuwa ni moja ya ahadi kuu za Rais wa Mexico, Andrés Manuel Lopez Obrador, mara baada ya kuchaguliwa mwaka 2018.

Upingwaji wa sheria hii ulianza wakati wa taratibu za bungeni hadi ilipoidhinishwa. Mtandao wa Asasi za Kiraia unaojihusisha na utetezi wa haki za kidigitali, au kwa kifupi R3D, ulitoa tahadhari katika hatua za awali kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuwa mchakato huu unachangia katika kupunguza makosa ya mtandaoni. Pia, walieleza kuwa mchakato huu ni raisi kukwepwa na baadhi ya watu. Wakati huohuo, kanzidata hii inadhaniwa kuwa inaweza kupelekea ufunjifu wa haki za msingi kama vile haki ya faragha na pia kuweza kuhatarisha usalama wa raia kutokana na uwezekano wa watu wasiohusika kupata taaarifa binafsi za watu au kuwepo kwa hatari ya kuvuja kwa taarifa hizi. Pia, asasi hii iliweka bayana kuwa, sharia hii itaathiri hali ya watu kuwa wakweli kwani “mabadiliko haya ya sharia yanaweka bayana kuwa taratibu zote za kisheria zinazofanyika kupitia namba za simu [yatahusishwa] na mtu aliyesajiliwa kwenye rajisi hii,” ikimaanisha kuwa, kwa mfano, itawalazimu watu wathibitishe kuwa hawatashitakiwa kwa tukio lolote la wizi au la matumizi ya taarifa binafsi za mtu bila idhini yake.

Sekta moja ya inayojihusisha na masuala ya mawasiliano ya kielekroniki inayojumuisha makampuni 1,000 , iliwataka watunga sheria kuachana na mswada huo wa sheria. Wanahoji kuwa, itakuwa vigumu kuwa na kanzidata katika mazingira ambayo kila mtoa huduma za simu anatumia teknolojia yake binafsi, na kwamba utaratibu huu unaathiri uwekezaji katika siku zijazo, hii ni pamoja na kile kinachosemwa kuwa sharia hii haitapunguza idadi ya makosa ya uhalifu.

Nchini Mexico, pamoja na kuwa kuna hali ya kuwa na Imani na serikali ya shirikisho kwa mujibu wa takwimu rasmi , asilimia 7.5 ya raia wa Mexico walisema kuwa wahanga wa matukio ya rushwa yaliongezeka, hii ni kwa mujibu wa Utafiki wa Kitaifa wa Ubora wa Huduma za Serikali . Taasisi mbalimbali zina hofu kuwa, taarifa binafsi za watu zinaweza kuvuja na kuangukia kwa watu wabaya na hivyo kuwaweka watu katika hali ya sintofahamu.

Matukio kadhaa yameripotiwa ya taasisi kadhaa za serikali nchini Mexico kushindwa kuhifadhi kikamilifu taarifa binafsi za watu , hii ni kwa mujibu wa wakala anayehusika na uhifadhi wa taarifa binafsi za watu. Moja ya mifano hai ya hivi karibuni ni Wizara ya Kazi, ambayo iliweka wazi taarifa za wafanyakazi wa serikali kuu wapatao 830,000 .

Tukio jingine la aina hii lilitokea kwenye sekta ya afya. Mwaka 2018, taarifa za kitabibu milioni 2.3 zilivuja katika jimbo la Michoacán. Mamlaka za serikali zilidai kuwa “wajibu wa msingi” unabaki kwa kampuni husika ya teknolojia ambayo ni Hova Health. Katika sekta hiyohiyo, mwaka 2020, uchunguzi ulibaini taarifa binafsi za wagonjwa ambao ni watumishi wa serikali zilionekana kupitia vivinjari vya intaneti .

Jaribio la kuanzishwa kwa kanzidata kama hii iliyojulikana kama Kanzidata ya Kitaifa ya Usajili wa Watumiaji wa Simu za Mkononi (Registro Nacional de Usuarios de Telefonía Móvil, or RENAUT, kwa kihispaniola) lilifanyika mwaka 2009. Ilidumu kwa miezi miwili tu kabla ya kusitishwa mara baada ya kuripotiwa kuwa kanzidata hii ilikuwa inauzwa. Mwaka 2013, rajisi ya uchaguzi ilitangazwa mtandaoni kuwa inauzwa.

Raia wamechukua hatuza za kisheria dhidi ya uanzishwaji wa rajisi ya namba za simu, hata hivyo, nyingi ya hatua hizi zilitupiliwa mbali na mahakimu. Kwa upande wake, Taasisi ya Taifa ya Uwazi, Upatikanaji wa Taarifa na Ulinzi wa Taarifa binafsi za Raia (Instituto Nacional de Transparencia, Acceso a la Información y Protección de Datos Personales in Spanish) ilifungua madai ya ukiukwaji wa katiba kwa kuwa inaamini kuwa rajisi hii inakiuka taratibu za uhifadhi wa taarifa binafsi za watu pamoja na haki ya uhuru wa kupata taarifa. Taasisi ya Taifa ya Mawasiliano (Instituto Federal de Telecomunicaciones, au IFT, kwa kispaniola) iliafiki juhudi hizi, kwa hoja kuwa haikutenga fedha zozote kwa ajili ya uandaaji na shughuli nyingine zozote za rajisi hii, kwa kuwa hakukuwa na bajeti yoyote iliyopitishwa, na kwamba rajisi hii inaminya uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa huduma za mawasiliano.

Kwa upande wake , mkakati wa #NoALPadrón (#NoToTheRegistry), unaoundwa nan a asasi 10 za kijamii, iliitaka Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu (Comisión Nacional de Derechos Humanos, au CNDH, kwa kispaniola), shirika la serikali linalojitegemea, lilifungua shitaka la kupinga rajisi hii ambayo haipo kikatiba. Hata hivyo, tume ilitoa taarifa kuwa isingeweza kushirikiana na shirika hili, bali ingefanya ufuatiliaji.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.