TAZAMA/SIKILIZA: Kupambana na miiko inayozuia utoaji mimba

Mwezi Desemba mwaka jana, dunia yote ilijielekeza nchini Argentina ambako utoaji mimba uliruhusiwa rasmi kisheria nchini humo. Lakini je, ni kwa kiwango gani wasichana na wanawake wanalazimishwa kuwa wazazi katika sehemu nyingine duniani?

Tazama au sikiliza kipindi hiki cha Global Voices Insights (kilichoruka hewani mubashara tarehe 7 Aprili), ambapo mhariri wetu wa Amerika Kusini Melissa Vida anafanya mazungumzo kuhusu haki za uzazi na wataalam na wanaharakati wafuatao:

    • Debora Diniz (Brazil): mtaalam wa stadi za utamaduni anayeendesha miradi ya kiutafiti katika masuala ya maadili ya kibaolojia, haki za wanawake, haki za binadamu na afya. Anafundisha Chuo Kikuu cha Brasilia, lakini pia akitafiti katika Chuo Kikuu cha Brown, na ni mwanaharakati wa haki za uzazi. Dokumentari zake kuhusu utoaji mimba, usawa katika ndoa, kutenganishwa kwa serikali na masuala ya dini na utafiti kuhusu seli mundu zimepata tuzo mbalimbali za kitaifa na kimataifa na zimeshindanishwa kwenye mashindano mbalimbali.
    • Joy Asasira (Uganda): mtetezi mbobezi wa Afya ya Uzazi barani Afrika, Haki za Binadamu, na masuala la Jinsia na mwanamikakati wa masuala ya utetezi duniani, msuka kampeni, na harakati na gwiji wa uratibu na mipango. Joy alitunukiwa tuzo ya Chama cha Wanasheria nchini Uganda (ULS) ya Mwanasheria Mwanamke Bora wa Haki za Binadamu kwa 2018/2019 na akatambuliwa kama kiongozi mwanamke chipukizi katika Afya ya Dunia kwenye Mkutano wa Wanawake Viongozi duniani uliofanyika Chuo Kikuu cha Stanford mwaka 2017.  
    • Emilie Palamy Pradichit (Thailand): mwanzilishi na mkurugenzi wa Shirika la Manushya, alilolianzisha mwaka 2017 (Manushya ni neno la Sanskrit lenye maana ya ‘Mtu”), akiwa na lengo la kuhamasisha nguvu ya jamii za watu wa maeneo mahususi, hususani wanawake watetezi wa haki za binadamu, ili waweze kupigania haki zao, usawa na haki za kijamii. Emilie ni mwanasheria wa kimataifa wa haki za binadamu aliyebobea kwenye haki za jamii zilizotengwa. 
    • R Umaima Ahmed (Pakistan): mwandishi wa kujitegemea. Mwanzoni alikuwa Mhariri Msaidizi wa tovuti ya The News on Sunday na gazeti la The Nation. R Umaima ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 wa maudhui ya mtandaoni na magazetini. Amejikita kwenye masuala ya usalama wa kidijitali, wanawake na haki za wanyama. Pia ni mwandishi wa Global Voices.
    • Dominika Lasota (Poland): mwanaharakati wa haki za tabia nchi mwenye umri wa miaka 19 ambaye pia ni sehemu ya harakati za Fridays For Future na Women's Strike.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.