makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mghosya
‘Mnao uwezo mkubwa na kuzidi’
"Siwezi kunyamazia mfumo wa elimu unaozidisha matarajio yanayoadhibu na kufedhehesha watoto wa taifa hili."
Nanjala Nyabola ajiunga na Global Voices kuwa Mkurugenzi wa Advox
Kama mkurugenzi wa mradi wa utetezi (Advox), Nanjala ataongoza uhariri wa uandishi wa habari za Global Voices, utafiti, uanaharakati na utetezi wa uhuru wa kujieleza na haki za kidijitali na teknolojia.
Nani Jansen Reventlow na Rasha Abdulla waungia kwenye bodi ya Global Voices
Tunafurahi kutangaza kuongezeka kwa wanachama wawili makini waliojiunga na bodi yetu ya wakurugenzi
Mwanamke wa tano auawa nchini Azerbaijan katika kipindi cha siku 10
Mwanawake aliyenyongwa hadi kufa nchini Azerbaijan ni wa tano kuuawa kwa sababu ya mgogoro binafsi na mwuuaji ndani ya siku 10.
TAZAMA/SIKILIZA: “Kwenda zaidi ya Maandamano,” mazungumzo na Tanya Lokot
Ulikosa matangazo mubashara ya Juni 17 kuhusu "Mazungumzo ya Global Voices" yaliyomshirikisha msomi wa masuala ya habari Tanya Lokot kuhusu kitabu chake cha "Beyond the Protest Square"? Tazama hapa video na sauti ya marudio ya matangazo hayo.
Ujerumani yakiri kuhusika na mauaji ya kimbari nchini Namibia enzi za ukoloni, lakini wahanga wasema haitoshi
Miaka zaidi ya 100 baada ya mauaji ya kimbari ya watu wa kabila la Ovaherero na Nama nchini Namibia, Ujerumani inakiri kuhusika kwake na itatoa fedha kufadhili miradi nchini Namibia kwa kipindi cha miaka thelathini.
Serikali ya Nijeria yaifungia Twita baada ya mkanganyiko wa twiti ya rais iliyotishia matumizi ya nguvu kufutwa
Watumiaji wa twita nchini Naijeria kutoka kwenye makabila mbalimbali yalitumia majina ya Kiigbo kukuza alama habari ya #IamIgboToo kuonesha mshikamano wao na watu wa kabila la Igbo waliotishiwa na twiti ya Rais Buhari.
Trinidad na Tobago yakaribia kurekebisha Sheria ya Fursa Sawa kutambua ushoga
Mijadala kuhusu hitaji la kubadili Sheria ya Fursa Sawa nchini Trinidad na Tobago imepamba moto baada ya benki kubwa nchini humo kuchukua hatua kubwa za kutambua haki za makundi mbalimbali.
MUBASHARA mnamo Mei 20: Tunachojifunza kuhusu Ulaya kupitia Shindano ya Eurovision
Shindano la Uimbaji la Eurovision linatuambia nini kuhusu siasa, taswira na maadili ya Ulaya? Ungana nasi mnamo Mei 20 kufahamu zaidi. Kipindi hiki kitaonesha mahojiano na washiriki wawili wa mwaka huu!
Mpango wa kutoa chanjo ya UVIKO-19 nchini Kenya waibua matabaka ya maskini na wasiojiweza
Wafanyabiashara na wanasiasa wanapata chanjo mapema wakati Wakenya masikini na wazee wakisimama kwenye foleni ndefu.