Mpango wa kutoa chanjo ya UVIKO-19 nchini Kenya waibua matabaka ya maskini na wasiojiweza

"Information and awareness is important to prevent the spread of COVID-19. Here in Kenya, Clinical Health care workers are sensitising the community on COVID-19. Photo : Victoria Nthenge" by Trocaire is licensed under CC BY 2.0

“Taarifa na uelewa ni muhimu katika kujikinga na maambukizi ya UVIKO-19. Picha inawaonesha wafanyakazi wa afya nchini Kenya wakielimisha jamii kuhusu maambukizi ya UVIKO-19. Picha: Victoria Nthenge” na Trocaire ina leseni ya CC BY 2.0

Kuanza kutolewa kwa chanjo ya UVIKO-19 nchini Kenya kumegubikwa na tuhuma za vitendo vya rushwa, upendeleo na ufisadi ambavyo vimewaacha wananchi wengi masikini na wazee wakisubiri kwenye mistari mirefu nje ya hospitali za umma wakati huu ambao nchi hiyo inakabiliwa na mlipuko wa tatu wa maambukizi na vifo vinavyotokana na UVIKO-19.

Wakati huo huo, mamia ya Wakenya wanalipa kiasi cha hadi dola 100 ili waweze kuitwa mapema, kama ilivyoelezwa kwenye akaunti kadhaa za Wakenya mtandaoni sambamba na vyombo vya habari vya Kenya na vile vya kimataifa.

Mapema mwezi Machi, Kenya ilinunua zaidi ya dozi milioni 1 za chanjo ya Oxford-AstraZeneca kupitia mpango wa Upatikanaji wa Chanjo ya UVIKO-19 Duniani, inayoratibiwa na Shirika la Afya Duniani kupitia utaratibu unaoitwa COVAX. Kupokelewa kwa chanjo hizo kulianzisha kampeni ya kutoa chanjo bure katika hospitali teule za umma na binafsi.

Kutolewa kwa dawa hizo kuligawanywa katika hatua tatu: watumishi wa afya na maafisa usalama na uhamiaji, wananchi wenye umri zaidi ya miaka 58 na watu wazima wenye changamoto mbalimbali za afya, na wananchi wengine wanaoishi kwenye mazingira hatarishi kama wale wanaoishi kwenye makazi yasiyo rasmi. Nchi hiyo inategemea kupokea dozi milioni 24 kupitia utaratibu wa  COVAX. Kwa mujibu wa jarida la The Washington Post, Kenya inalenga kuchanja asimilia 50 ya wananchi wake ifikapo Juni 2022 kwa ushirikiano kati ya mradi wa COVAX na misaada kutoka mataifa mengine.  

Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mwakilishi wa UNICEF nchini Kenya Maniza Zaman alipongeza kuwasili kwa chanjo za kwanza nchini Kenya. “Kufuatilia kuwasili kwa chanjo hizi, UNICEF na washirika wake wanapongeza ahadi ya COVAX kuhakikisha kuwa watu wanaotoka kwenye nchi zisizo na uwezo mkubwa kiuchumi hawaachwi nyuma kwenye mpango huu wa kimataifa wa kuokoa maisha ya watu kwa chanjo,” alisema.

Hata hivyo, mpango huu wa tatu ulivurugika mara baada ya zoezi kuanza kwa sababu ya uamuzi wa dakika za mwisho wa kuharakisha awamu ya pili ya mpango huyo kama namna ya kukabiliana na wimbi la tatu la maambukizi, maslahi ya kisiasa yanayokinzana, na serikali kushindwa kuwasiliana na kuwajulisha wananchi.

Katika makala yake inayohoji kile kinachoendelea kwenye mpango wa chanjo ya UVIKO-19 nchini Kenya, Patrick Gathara, mwandishi anayeishi Kenya na mchoraji wa katuni za siasa aliyepata tuzo mbali mbali alisema:

Politicians loudly and self-servingly argued that they should be given priority to inspire confidence among the population, even though the Ministry of Health was reporting encountering little resistance. Because the state had ignored the need to explain its plan to the population, there was widespread confusion about where and when people were expected to be in line.

Kwa sauti kubwa na ubinafsi, wanasiasa walidai kwamba wao ndio wanaopaswa kupewa kipaumbele ili kuwajengea imani wananchi, ingawa Wizara ya Afya tayari ilisharipoti kutokuwepo kwa upinzani mkubwa wa chanjo hiyo. Kwa kuwa serikali imepuuza takwa la kueleza mpango wake kwa wananchi, kulikuwa na mkanganyiko mkubwa kuhusu wapi na lini watu wanatarajiwa kusimama kwenye mstari.

Pamoja na maelekezo ya serikali  kuwapa kipaumbele wananchi wenye umri wa zaidi ya miaka 58,  vyombo vya habari nchini Kenya viliripoti kwamba wafanyabiashara na wanasiasa wasio kwenye kundi la umri huu wamekuwa wakipata huduma kinyume na utaratibu, hali inayoonesha ubaguzi mkubwa wa masikini unaofanywa na wenye fedha.

Wakati huo huo, wazee wanaostahili na Wakenya maskini, ambao hawana mtandao wa watu wa kuwasaidia na wasio na fedha za kuhonga,  huonekana wakingoja kwenye mstari siku zote kuanzia saa 11 alfajiri, na kuishia kuombwa warudi siku nyingine kwa sababu dawa zimeisha, kwa mujibu wa habari iliyoandikwa na jarida la The Washington Post.

“They have another door for their friends,” Mary Njoroge, 58, one of the teachers, told The Washington Post. “Without a godfather to help you through this process, what are you supposed to do?”

“Wana mlango mwingine kwa marafiki zao,” Mary Njoroge, 58, mmoja wa walimu, aliliambia The Washngton Post. “Bila kuwa na mtu wa kukusaidia kukamilisha mchakato wote, utafanya nini?”

Tukio kama hilo liliripotiwa kwenye hospitali nyingine ya serikali na @_Sativa, mtumiaji wa Twita anayeishi Nairobi, ambaye pia ni Mkenya. Kwenye uzi huo wa Twita, alielezea kile ambacho shangazi yake alikutana nacho, mwalimu mstaafu mwenye zaidi ya miaka 60. Wakati wazee wakisubiri mstarini, muuguzi aliita majina na vijana walikuja mbele na wakatangulia kupata chanjo. Shangazi yake alipouliza nini kinaendelea, muuguzi alimpa namba [ya simu] ambayo angeweza kutumia fedha, alisema kwenye uzi huo wa Twitter.

Kufuatia taarifa za kuongezeka kwa hamasa ya watu kwa kampeni hiyo ya chanjo, Waziri wa Afya wa Kenya, Mutahi Kagwe aliviambia vyombo vya habari:

I think somewhere along the line we seem to have developed some confusion that anybody can walk into a vaccination centre and get vaccines. I want to make it very clear, those carrying out vaccination will have to account for every dose that they have used and that dose that they have used must be matched against an eligible person.

Nadhani tumefika mahali tumetengeneza hali ya sintofahamu kwamba mtu yeyote anaweza kwenda kwenye kituo cha kutolea chanjo na kupata huduma. Ninataka kuliweka suala hili vizuri, wale wanaotoa huduma ya chanjo watatoa hesabu ya kila dawa waliyoitumia na kwamba dawa zilizotumika lazima zioanishwe na mtu anayestahili huduma hiyo.

Rais wa Chama cha Taifa cha Wauguzi nchini Kenya Alfred Obengo aliwaomba Wakenya wasio kwenye orodha ya kipaumbele kuepuka kusimama kwenye foleni ya chanjo.

Akifafanua namna serikali ya Kenya ingeweza kuepuka mkanganyiko huo katika kutekeleza mpango huo,  Gathara anahitimisha makala yake kwa kusema:

Much of this could have been avoided if the Kenyan government and its global partners, including the World Health Organization and Western governments, treated Kenyans as partners in the rollout rather than colonial subjects to be brutalised and exploited. Sadly for Kenyans, their colonial state does not know how to act any differently.

Tungeweza kuepuka kadhia hii kama serikali ya Kenya na washirika wake duniani, ikiwa ni pamoja na Shirika la Afya Duniani na serikali za nchi za magharibi, zingefanya kazi na Kenya kama mbia wa mpango huu na sio koloni linalotendewa ukatili na kunyonywa. Inasikitisha sana kwa Wakenya, nchi yao ambayo ni koloni haifahamu namna nyingine ya kufanya.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.