Mwanamke wa tano auawa nchini Azerbaijan katika kipindi cha siku 10

Picha iliyopigwa kwenye video ya Meydan TV report kuhusu mauaji ya wanawake nchini Azerbaijan.

Makala haya yalichapishwa awali kwenye OC Media. Toleo lililohaririwa linachapishwa Global Voices chini ya makubaliano ya ushirikiano wa kimaudhui .

Nargiz Mustafayeva, mkazi wa Wilaya ya Barda, alinyongwa hadi kufa siku ya Jumapili, Julai 25. Mume wake, Agil Mustafayev, alizaliwa mwaka 1983, alikamatwa. Kwa mujibu wa Ofisi ya Mwendesha Mashitaka, Mustafayev alimwuua mke wake kwa sababu za ugomvi wa kifamilia.

Mustafayeva ni mwanamke wa tano kuuawa nchini Azerbaijan ndani ya siku 10.

Mnamo Julai 24, Meykhosh Jafarov alidaiwa kumpiga mke wake, Khatira Farajova, hadi kufa. Kwa mujibu wa waendesha mashtaka, Farajova na watoto wake walidhalilishwa mara kwa mara na Jafarov.

Mnamo Julai 23, Zarbali Guliyev alidaiwa kumpiga na kumwuua mke wake Lyudmila Tatachenko kufuatia mzozo, kisha kujiua na yeye.

Mnamo Julai 22, sajenti wa polisi Aliaga Soltanov alidaiwa kumwuua Mubarak Agayeva kwa kisu pia kufuatia majibizano.

Mnamo Julai 16, mwimbaji Aygun Mirzayeva alipigwa mara 23 akiwa hotelini mjini Baku. Ali Mammadov, aliyekamatwa kwa mauaji hayo, alisema wawili hao walikuwa wapenzi na alikiri kufanya mauaji hayo.

Kwa mujibu wa mwanaharakati wa haki za wanawake Gulnara Mehdiyeva, wanawake wa Azerbaijan hawana uhakika wa hata ule usalama wa kawaida. “Ninadhani mauaji ya wanawake ni ushahidi wa namna wanawake walivyo hatarini nchini hapa. Kwa sababu, katika mengi ya matukio hayo, mauaji sio hatua ya kwanza ya udhalilishaji, bali hatua ya mwisho kabisa,” Mehdiyeva aliiambia OC Media. Aliongeza:

Murderers are often known for their violence against their spouses or lovers beforehand. For example, a husband who kills his wife who is trying to get a divorce and has abused her and her three children. That was the reason for the divorce.

Wauaji mara nyingi wanafahamika kwa vitendo vya uonevu kwa wenzi au wapenzi wao. Kwa mfano, mume anayemwuua mke wake kwa kujaribu kupata talaka na amemdhalilisha na watoto watatu. Hiyo ndio sababu ya talaka ya kutafuta talaka.

Mehdiyeva alisema kwamba mashirika ya kusimamia utekelezaji wa sheria “yamefanya kila kinachowezekana isipokuwa kile wanachotakiwa kukifanya.”

The country’s policies and the current legislation do nothing to protect women in the period before they are murdered. Police does not like to open criminal cases, especially for domestic violence. When applying to the police, applicants are encouraged to withdraw their complaints in order to reduce the number of cases. They [the police] do everything except their job.

Sera za nchi hiyo na sheria zilizopo hazifanyi chochote kuwalinda wanawake kabla hawajauawa. Polisi hawapendi kufungua kesi za jinai, hususani kwa vitendo vya udhalilishaji majumbani. Wanapoenda polisi, mara nyingi wanawake huombwa kutoa malalamiko yao ili kupunguza idadi ya kesi. Polisi hufanya vyote isipokuwa kazi wanayotakiwa kufanya.

Mehdiyeva aliiambia OC Media kwamba kukosekana kwa uwajibikaji pia kunahusisha mfumo wa mahakama ya nchi hiyo. “Mahakama hazitendi haki; mashirika ya hifadhi ya jamii hayawezi kutoa msaada wa kijamii kwa wanawake wenye watoto wasio na kazi. Matokeo yake, wanawake wanalazimika kuendelea kupambana na uonevu. Hali hii huishia kwa mauaji.”

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.