makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mghosya kutoka Agosti, 2009
Iangazeni Naijeria: Imetosha Sasa Basi
Pamoja na kuwa nchi yenye utajiri wa mafuta, hali ya ugavi wa umeme nchini Naijeria hairidhishi. “Katika sehemu nyingi za nchi, giza linatawala na majenereta yamechukua nafasi kama vyanzo vya nishati ya umeme” Inasema blogu ya Adebayo. Sasa Wanaijeria wameanzisha kampeni kubwa ya mtandao wa intaneti inayopinga hali hii inayogharikisha kwa kutumia tovuti za kijamii, hasa kwenye Twita kwa kutumia anwani ya #lightupnigeria (#iangazenaijeria).