Mghosya · Disemba, 2012

makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mghosya kutoka Disemba, 2012

Habari za Upotoshaji Kuhusu Afrika Katika Vyombo vya Habari vya Kimataifa

 Kampeni ya kumkamata #Kony2012 ilibeba mambo yaliyorahisishwa mno kuhusu Afrika. Vyombo vya habari vya Afrika vyenyewe, hata hivyo, kwa sasa havina kinga dhidi ya ukosoaji wa aina hii. Hapa ni muhtasari wa watu maarufu, makosa na kutokuwepo umakini katika habari zinazopewa nafasi katika vyombo vya habari vya dunia kuhusu Afrika na katika vyombo vya habari vya Afrika vyenyewe

31 Disemba 2012

Mwandishi wa Guinea Atoweka Kiajabu nchini Angola

Yuko wapi Milocas Pereira? Swali hili linarudiwa rudiwa kupitia blogu mbalimbali kwa majuma kadhaa sasa, lakini majibu yamekuwa vigumu kupatikana. Katika mitandao ya kijamii harakati zililipuka kuzishinikiza mamlaka za nchi ya Guinea kuchunguza mazingira ya kupotea kwa mwandishi huyo na mhadhiri wa Chuo Kikuu miezi sita liyopita katika jiji la Luanda, alikokuwa akiishi tangu mwaka 2004.

31 Disemba 2012

Chama cha Upinzani NPP Chapinga Matokeo ya Urais Ghana Mahakamani

Chama Kikuu cha Upinzani nchini Ghana, NPP, kimegoma kuyakubali matokeo ya uchaguzi wa Rais. Mnamo tarehe 9 Desemba 2012, Tume ya Uchaguzi ilimtangaza Rais Mahama kuwa mshindi kwa asilimia 50.70 ya kura, akimshinda mshindani wake wa maribu Nana Akufo-Addo wa NPP. Chama cha NPP hapo awali kilifungua mashitaka katika Mahakama Kuu tarehe 28 Desemba, 2012.

30 Disemba 2012

China Inaelekea Wapi kwa Mwaka 2013?

Kadri mwaka wa 2012 unavyosogea karibu, jarida la CHINA DIGITAL TIMES limetoa muhtasari wa mabadiliko na changamoto zinazoikabili China mwaka 2013 kwa kutumia taarifa na bashiri mbalimbali za vyombo vya...

29 Disemba 2012

Assad atumia Ndege ya Kivita Kuwaua Raia Wake

Serikali ya Syria imefanya shambulizi kubwa la angani dhidi ya raia wa nchi hiyo -waliokuwa wamesimama kwenye foleni waisubiri mikate kwenye kiwanda cha kuokea miakte huko Halfaya, Hama. Inakadiriwa kwamba watu waliouawa katika shambulio hilo mjini humo ni kati ya 90 na 300, waasi wakisema kuwa watu hao walikuwa wamejitenga na vikosi vya Assad. Mtandaoni, wanaharakati wanashangazwa inakuwaje dunia inaendelea kutazama tu maisha ya watu wasio na hatia wakiuawa kwa mamia.

28 Disemba 2012