Mghosya · Aprili, 2011

makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mghosya kutoka Aprili, 2011

Misri: Basboussa kwa Urais!

Mtangazaji habari wa zamani wa televisheni ya Misri na mwanaharakati Bothaina Kamel alitangaza kwenye twita kwamba ana mipango ya kugombea urais. Yafuatayo ni maoni ya kumuunga mkono na kupinga hiyo mipango yake .

28 Aprili 2011

Côte d'Ivoire: Gbagbo agoma, Waafrika waandamana

Wakati Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Rais Laurent Gbagbo akiwa bado amejichimbia ndani ya handaki nchini humo, akigoma kukamatwa kwa kuendelea kukataa kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, ushiriki wa Ufaransa katika harakati za kumng’oa zinasababisha miitikio miongoni mwa wanasiasa na raia wa Ufaransa, pamoja na jamii ya Waafrika waishio Ufaransa.

12 Aprili 2011

Côte d'Ivoire: Abijani kwenye masaa ya kudhoofu kwa utawala wa Gbagbo

Siku mbili zilizopita zimekuwa na utajiri katika misuguano na mivutano nchini Côte d'Ivoire. Vikosi vinavyomtii Ouattara, vilianza mashambulizi kuelekea Kusini na Magharibi mwa nchi hiyo. Katika siku zisizozidi tatu, walifanikiwa kuikamata miji ya Douékoué na kufika Yamoussoukro tarehe 30 Machi. Wa-Ivory wanatoa maoni yao kuhusu wafungwa kutoroka, kufungwa kwa televisheni ya taifa na sehemu aliyo Gbagbo:

12 Aprili 2011

Naijeria: Je, Teknolojia itaathiri uchaguzi wa mwaka 2011?

Wanaijeria wanaingia kwenye uchaguzi tarehe 16 Aprili 2011 kumchagua rais wao mpya. Uchaguzi uliahirishwa kutoka siku iliyokuwa imepangwa awali ya Aprili 9 kwa sababu ya kasoro za kimuundo. Katika makala hii tunatazama namna Wanaijeria wanavyotumia teknolojia kuwezesha uwazi katika uchaguzi, ushirikishwaji wa kisiasa na utawala bora.

11 Aprili 2011

Japani: Iambieni Dunia isaidie

Picha zilizotafutwa na kuwekwa kwenye twita zinaweza kuleta mambo ya kushangaza. Tafuta herufi hizi “宮城” (Miyagi) na picha chache zitatokea kutoka kwenye wilaya hiyo, moja ya maeneno yaliyoharibiwa sana nchini Japani baada ya tsunami. Nenda chini, na picha moja inaonekana, yenye rangi ya kahawia na bluu mpaka utakapoibofya…

10 Aprili 2011