Côte d'Ivoire: Abijani kwenye masaa ya kudhoofu kwa utawala wa Gbagbo

Makala hii ni miongoni mwa makala zetu maalumu kuhusu Vurugu za mwaka 2011 nchini Ivory Coast.

Siku mbili zilizopita zimekuwa na utajiri wa misuguano na mivutano nchini Côte d'Ivoire.

Vikosi vinavyomtii Alassane Dramane Ouattara, Rais wa nchi hiyo anayetambulika kimataifa, na Guillaume Soro, Waziri Mkuu wa Ouattara, vilianza mashambulizi kuelekea Kusini na Magharibi mwa nchi hiyo. Katika siku zisizozidi tatu, walifanikiwa kuikamata miji ya Douékoué na kufika Yamoussoukro tarehe 30 Machi. Forces Républicaine de Côte d'Ivoire (Jeshi la Jamhuri ya Côte d'Ivoire) liliingia Abijani, mji mkuu wa nchi hiyo ambako Rais aliyepo madarakani Laurent Gbagbo, aliyegoma kuachia madaraka tangu Desemba mwaka jana (2010) baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa Rais, anaweza kuwa huko.

Jamii ya mtandaoni ya Côte d'Ivoire inayo maoni katika matukio hayo, na ifuatayo ni picha ya haraka ya majadiliano machache:

Hofu ya wafungwa wa gereza la MACA

Maison d'Arrêt et de Correction d'Abidjan (MACA) nigereza la Abijani. Kufuatia habari kwamba wafungwa wameachiliwa huru, Léon Guéré (@Cocoloposo) aliandika kwenye twita tarehe 31 Machi:

@cocoloposo: #civ2010 URGENT: MACA ouverte tous les prisonniers sont dehors.(police)

Habari za hivi punde: Gereza la MACA limefunguliwa, wafungwa wametoroka

Kufuatia tangazo hili, watumiaji wa mtandao walianza kuhofia kwamba wafungwa hawa wanaweza wakapewa silaha:

@Abidjannais225, akimjibu @Cocoloposo, alisema:

@Abidjannais225: Confirmez SVP !!! P…. mais c grave, LMP veut creer la chienlit au pays

Thibitisha tafadhali! Hii ni hatari. Chama cha Laurent Gbagbo kinataka kutuletea balaa katika nchi hii

Mwanaharakati wa mtandoni “K” (@Sanders225) alithibitisha siku hiyo hiyo kwamba wafungwa wa gereza la MACA, na wengine wa kutoka kwenye magereza mengine mawili wameachiwa. Baada ya muda, taarifa ya habari kwenye Shirika la Habari la Reuters ikasema wafungwa wanaofikia 5000 wameachiwa mjini Abijani.

Yuko Wapi Laurent Gbagbo?

Guillaume Soro, waziri mkuu alitangaza kwamba Laurent Gbagbo alikuwa amepewa mpaka saa 1 usiku (saa za GMT) tarehe 31 Machi, 2011 awe amejiuzulu. Hii ilisababisha miitikio mikali kwenye alama ya twita ya habari kuhusu Côte d'Ivoire ambayo ni, #civ2010:

Dakika kumi na tano kabla ya kukamilika kwa saa aliyopewa Gbagbo kujiuzulu, @Malko7 alianza kuhesabu dakika zilizobaki kwa njia ya twita:

@Malko7: Heure H-15 minutes

Saa 1- bado dakika 15

Na muda ulipofika, Marie L'Ange (@Attou_225) alitoa maoni:

@Attou_225: c'est l'heuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuure!!!!

Muda umeeeeeeeefikaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!

Nnenna akatuma twita:

@Nnenna: Il est 19h ici chez moi. On dit koi?

Hapa ni saa 1 usiku. Nini kinaendelea?

Wakati huo huo, mapambano makali yalianza kupigwa Radio Télévision Ivoirienne. Kituo hicho kilikuwa bado kinadhibitiwa na wafuasi wa Gbagbo mpaka jana yake.

Kati ya saa 3 usiku (GMT) na saa 4:40 (GMT), picha moja ya video ilirushwa kwa kurudia rudia: Laurent Gbagbo na mkewe Simone, wamezungukwa na walinzi wao wa karibu wakiwa na majadiliano katika bustani ya Makazi ya Rais mtaa wa Cocody. Laurent Gbagbo anaonekana amesongwa na mambo, na Simone haonekani kuelewa hali ya mambo ilivyo mjini Abijani, kama ilivyooneshwa kwenye video hii iliyowekwa na abidjannetTV, anuani ya You Tube ya wavuti ya habari ya nchi hiyo:

Matangazo ya RTI mwishowe yalikatika saa 4:40 usiku (saa za GMT) kama ilivyooneshwa kwenye picha hii iliyowekwa na Olivier Vauluisant (@batelier59):

Mwisho wa matangazo ya Luninga ya Taifa (RTI) picha iliyowekwa na Batelier59

Kwa mujibu wa Senam Beheton (@SenamBeheton) kwenye twita, picha hizi zilionyeshwa wakati vikosi vya Ouattara vikichukua udhibiti luninga hiyo ya Taifa:

@SenamBeheton : Les propriétaires sont peut-être arrivés. La recréation est terminée?

Mabwana wakubwa huenda wamefika. Muda wa mchezo umeisha?

Kituo cha Sky News kiliripoti tarehe 1 Aprili kwamba Laurent Gbagbo na mke wake wanaweza kuwa bado wako kwenye kasri lao la Cocody, huku wamezungukwa na vikosi vya Ouattara. Baadaye siku hiyo hiyo toleo jingine lilitoka likibainisha kwamba Laurent Gbagbo na mkewe Simone wameondoka kwenye makazi ya Rais kuelekea kwenye kasri la rais lililoko eneo la uwanda wa juu [Fr], Abidjan. EdithBrou aliandika kwenye twita:

makazi ya rais na redio, huko uwanda wa juu na makazi binafsi ndivyo vimebaki tegemeo pekee la Gbagbo kwa mujibu wa mwanadiplomasia aliyezungumza na #AFP

Côte d'Ivoire ni mada inayoongoza kwenye twita

Matukio ya hivi karibuni nchini Côte d'Ivoire yalifuatiliwa kwa karibu kwenye twita, ambako #civ2010 na Laurent Gbagbo ndizo zilikuwa mada zinazoongoza nchini Ufaransa:

Makala hii ni miongoni mwa makala zetu maalumu kuhusu Vurugu za mwaka 2011 nchini Ivory Coast.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.