Makala hii ni sehemu ya habari maalumu tunazowaletea kuhusu Mapinduzi ya Misri ya Mwaka 2011.
” “Mtangazaji habari wa zamani wa televisheni ya Misri na mwanaharakati Bothaina Kamel alitangaza kwenye ukurasa wake wa twita usiku wa Ijumaa [ar] saa za Cairo kwamba ana mipango ya kugombea urais kwenye duru inayofuata ya uchaguzi, na kumfanya awe mwanamke wa kwanza kutangaza nia ya kutaka kuingia kwenye ofisi kuu nchini Misri”, Manar Ammar
Hivi ndivyo Manar Ammar alivyoripoti habari za Bothaina Kamel kugombea kwenye uchaguzi wa Urais wa Misri. Kamel (@basboussa1) amepokea miitikio mchanganyiko kutoka kwa watumiaji wa twita.
Mtumiaji wa Twita @FaresADLhakuweza kuamini habari hiyo, kwa hiyo akamwandikia Kamel akishangaa kama habari hizo zilikuwa zimethibitishwa ama zilikuwa ni uvumi tu:
Fatma Eman, ambaye ni mtetezi wa usawa wa mwanamke aliandika kuhusu habari hizo:

Picha iliyochukuliwa kwenye ukurasa wa facebook wa Bothaina Kamel; akishiriki maandamano wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vita Dhidi ya Rushwa duniani
Lara (@FarawlaLawra) aliiona habari hiyo kuwa nzuri, bila kujali ikiwa ameshawishika kumpigia kura ama la:
Mahmoud Salem, anayefahamika pia kama @Sandmonkey, pia aliandika kumuunga mkono:
Katika video hii iliyopandishwa kwenye YouTube na mtumiaji moushebl1 tarehe 3 Aprili, 2011, Kamel anatangaza mipango yake ya kugombea Urais [ar].
Watu kadhaa walitoa maoni juu ya video hiyo hapo juu kupingana na nia yake ya kugombea Urais.
Radwa El-Shami alihoji sababu zilizo nyuma ya idadi kubwa ya wagombea wanaoutaka Urais nchini Misri:
Ninahoji kwa nini Bw. Shafiq anagombea urais (wakati kiasi cha wa-Misri milioni 10 kati ya milioni 45 wenye sifa na haki ya kupiga kura walimkataa kama waziri mkuu!); kwa nini Dk. Amr Khaled anafikiria kugombea urais (bado haijathibitishwa); Jema gani Sheikh Hassan anafikiria kuwa itaifanyia Misri kama rais (kuna uvumi kuwa naye anawania urais); kwa nini Bw. Martada Mansour anajidhania kuwa anaweza kuwa rais (je atatutawala kwa vitisho na kupayuka?); kwa nini Bi. Bothaina Kamel anataka kuwa rais (ni harakati za usawa wa mwanawake?); kwa nini wapo watu wanamshawishi Bw. Naguib Sawiris kuwa sehemu ya harakati za uraisi (habari kutoka hapa na pale, lakini yeye mwenyewe alisema Baradei ni mtu anayempenda); na ninauliza pia ni upi msimamo wa Dk. AlBaradei baada ya umma kukubali mabadiliko yenye kilema ya katiba ambapo yeye aligoma kuwa rais?
Halafu Radwa aliendelea:
Makala hii ni sehemu ya habari maalumu tunazowaletea kuhusu Mapinduzi ya Misri ya Mwaka 2011..