Janga la COVID-19 limeathiri kwa kiwango kikubwa haki za wanawake huko Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika; kutoka kuongezeka kwa ukatili majumbani mpaka kupoteza ajira zao. Lakini kuna eneo moja lililowazi ambapo wanawake wameathirika ambalo mi ukeketaji, na hii ni baada ya kulipuka kwa janga la Korona na heka heka za kukabiliana nalo.
Mwezi April, Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa “kutokama ma vizuizi vilivyotokana na juhudi za kupambana na janga la korona, kuna visa milioni 2 vya ukeketaji ambavyo vinakisiwa kutokea kwa muongo ujao ambapo ingewekana kuzuia kama uzuiaji wa korona usingetibua mpango na juhudi za kupambama na ukeketaji”
Ukeketaji unajumuisha “shughuli za kukata kwa sehemu au kuondoa kabisa sehemu ya nje ya uke, au kuumiza sehemu za uke bila uhusiano au dhana yoyote ya kutabibu,” kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).
Kitendo hiki ni utamaduni wa kimila na kidini ulioota mizizi kote barani Afrika, Mashariki ya Kati na Asia , na hufanywa na wakunga wa jadi, waganga kwa kutumia visu, nyembe au vipande vya chupa.
Ukeketaji pia unafahamika kama ukataji wa sehemu za siri inaaminika kwa upana kuwa ni ” moja ya ukatili uliopitiliza dhidi ya wasichana na wanawake,” na bado unaripotiwa kwa uchache sana hasa huko Mashariki ya Kati. Inakadiriwa kuwa angalau wanawake milioni 200 wameathiriwa nao.
Jambo hili limeelezewa vyema na UNICEF katika video:
In the MENA region, Female Genital Mutilation (FGM) is a problem that primarily concerns Egypt, Sudan, Yemen, Iraq and Djibouti.
Carlos Javier Aguilar, Regional Adviser Child Protection, explains more.
Watch and share?help #EndFGM ? pic.twitter.com/OrjJvIQl8R
— UNICEF MENA – يونيسف الشرق الأوسط وشمال إفريقيا (@UNICEFmena) February 7, 2020
Katika ukanda wa Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, ukeketaji ni tatizo ambalo kimsingi linazitatiza nchi za Misri, Sudan, Yemen, Iraq na Djibouti.
Carlos Javier Aguilar, Mshauri wa Masuala ya Ulinzi wa Mtoto anaelezea zaidi,
Angalia na shirikisha?msaada #EndFGM ? pic.twitter.com/OrjJvIQl8R
Somalia inadhaniwa kuwa na idadi kubwa ya wahanga wa ukeketaji ambapo asilimia 98 ya wanawake wenye miaka kati ya 15 mpaka 49 wamekeketwa. Huko Djibouti, inakadiriwa asilimia 93 wameathirika, Misri asilimia 92, Sudan asilimia 88, Mauritania asilimia 69, Yemen asilimia 19 na Iraki asilimia 7 kulingana na takwimu zilizoachiliwa Juni na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Idadi ya watu (UNFPA).
Kitendo hiki hutofautiana kulingana na tabaka la kijamii, kabila na hata kiwango cha elimu katika kila nchi na katika maeneo ya mijini au vijijini. Ukeketaji mara nyingi hutokea baina ya watu maskini zaidi au katika familia ambazo hazijaelimika katika maeneo ya vijijini. Huko Yemen, ukeketaji umeota mizizi katika ukanda wa Pwani lakini unafanyika kidogo katika maeneo ya Kaskazini. Nchini Iraq, kitendo hiki kimesambaa sana katika upande wa Kaskazini mwa jimbo la Kurdi. Huko Misri unafanyika zaidi kwa wasichana wanaoishi ukanda wa Juu wa Misri.
Nchini Mauritania, zaidi ya asilimia 90 ya wanawake kutoka katika familia maskini zaidi wamefanyiwa ukeketaji ukilinganisha na asilimia 37 ya wanawake kutoka katika familia zenye kipato cha juu.
UKEKETAJI: Ukatili Unaoripotiwa Kidogo Zaidi
Ukubwa na upana wa ukeketaji utakuwa umedharauliwa kwa sababu ya “ulimwengu kutokuwa na picha halisi ya ukeketaji iliyokamilika,” kulingana na ripoti ya pamoja kuanzia Machi, imeidhinishwa na Usawa sasa, Mtandao kutoka Ulaya wa Kutokomeza Ukeketaji na Mtandao wa kutokomeza ukeketaji kutoka Marekani. Taarifa hiyo ilidhihirisha “kuwa utamaduni huu unaongezeka na pia unafanyika hata Mashariki ya Kati na Asia,” na “dunia kwa hakika imeupuuzia ukeketaji.”
Tafiti ndogo zilizo fanyika hivi karibuni zinaonesha kuwa ukeketaji pia unafanyika huko Iran, pamoja na nchi zote za Ghuba kama vile Kuwait, Falme za Kiarabu, Omani na Saudi Arabia. Divya Srinivasan kutoka Usawa Sasa aliiambia Reuters kwamba “alishangazwa sana na matokeo ya utafiti huo mdogo kutoka maeneo kama vile Omani na Saudi Arabia ambapo kwa kawaida sio maeneo ambayo yanaweza kukujia akilini unapoliwazia suala la Ukeketaji”
Taarifa hii ilichapishwa wakati janga la COVID-19 likiwa limeshika kasi huko Mashariki ya Kati na haikuchapishwa wala kutafsiriwa hata kidogo na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ya Kiarabu. Jamii kukosa uelewa kuhusu ukeketaji inaweza kuthibitisha dhana ya kuwa ukeketaji sio jambo la kutilia maanani kabisa.
Miiko ya Kijamii
Huko Mashariki ya Kati, kuna miiko inayoizingira miili ya wanawake ambapo ni marufuku kujadili hadharani mambo ya siri kama vile ukeketaji ambapo umefungamanishwa na imani za kimila, dini na utamaduni.
Kwa mfano, nchini Misri Wakristo na Waislamu kwa pamoja “wanaamini kwamba ukeketaji wa wasichana unawafanya wavutie zaidi waume zao watarajiwa na unawakinga na mabaya, pia wamama huhofia kwamba mabinti zao hawataolewa kama hawatakeketwa,” kulingana na ripoti ya Tokomeza Ukeketaji Mashariki ya Kati, kampeni ambayo iliandaliwa mwaka 2013 kuipa jamii uelewa Kuhusu ukeketaji na pia kuuambia ulimwengu kuwa ukeketaji haupo Afrika pekee bali pia katika nchi nyingi za Mashariki ya Kati na Asia”. Taasisi hii inaendelea kukusanya taarifa zaidi za ukeketaji na imetengeneza njia ya kukusanya taarifa itakayosaidia mtu mmoja mmoja au vikundi vya watu kufanya tafiti ndogo juu ya ukeketaji.
Watu hupendelea kuepuka mazungumzo na mada za ukeketaji labda tu litokee tukio litakalogusa vichwa vya habari kama tukio la kifo cha binti wa miaka 12 alifariki baada ya kukeketwa huko Kusini mwa Misri mwezi Februari, ndipo watu huzungumza.
Ghida Hussein, mwanafunzi wa Kimisri aliiambia Global Voices kwamba:
As we don’t talk about it, it is as if the problem doesn’t exist. FGM is often practiced silently behind closed doors. It is happening far from the more educated urban centers of power where activists and politicians are seated. FGM is a controversial sensitive issue and unless there is international attention and funding, it is not seen locally as a priority by an overwhelming male political class.
Kwa kuwa hatuzungumzi kuhusu jambo hili, ni kama vile tatizo hili halipo kabisa. Ukeketaji unafanyika kimya kimya nyuma ya milango iliyofungwa. Inatokea huko mbali na watu walioelimika mijini ambapo ndipo wanaharakati na wanasiasa wanakaa. Ukeketaji ni jambo tata na labda jumuiya ya kimataifa zitoe msaada wa fedha na uhamasishaji, lah sivyo hutaona jamii inayotawaliwa na tabaka la wanaume wakilipa jambo hili kipaumbele.
Kuvunja miiko na kuongea kuhusu ukeketaji huwafanya watetea haki za Binadamu kushambuliwa kwa lugha za matusi na chuki.
Nchini Oman, mwanaharakati wa haki za wanawake Habiba al Hinai, mwanzilishi wa Taasisi ya Haki za Binadamu – Omani alifanya utafiti mdogo mwaka 2017 huko Omani na akagundua kuwa asilimia 78 ya wanawake wamekeketwa.
Baada ya kuchapisha matokeo ya utafiti wake mtandaoni, Habiba alipokea mashambulizi na vitisho:
I posted my results online and the response was huge. I was attacked by religious conservatives who say female circumcision is a form of Islamic worship.
Niliweka matokeo ya utafiti wanhu mtandaoni na mwitikio ulikuwa mkubwa. Nimeshambuliwa na waafidhina wa kidini ambao walisema kuwa ukeketaji ni sehemu ya ibada ya Waislam.
Huko Omani, ambapo ukeketaji hautambuliki rasmi, hakuna ulinzi kwa wahanga. Habiba aliongeza haya katika taarifa yake:
How can you ask a survivor to speak out against FGM and then face all the consequences —criticism and online defamation, her family and her tribe may disown her, maybe her husband will divorce her — without proper support. I don’t expect these women to speak out and face society.
Ni jinsi gani unaweza kumwambia manusura aongee kuhusu ukeketaji na kisha akumbane na madhara yote haya ikiwamo kukosolewa, kutukanwana hata familia au ukoo wame unaweza kumtenga kabisa, pengine hata mumewe anaweza kumtaliki- kama hakuna namna rasmi ya kuunga mkono. Sitarajii wanawake hawa kusimama na kuzungumza lwa ujasiri na kuikabili jamii.
Kutokomeza Ukeketaji: Iko Taratibu sana, Haijitoshelezi
Nchini Yemen na Umoja wa Nchi za Kiarabu, ukeketaji umezuiwa kufanyika katika Taasisi za afya pekee, lakini sio majumbani. Nchini Mauritania, kuna kizuizi cha kisheria lakini sio kukatazwa moja kwa moja. Nchini Iraq, ukeketaji umekatazwa huko kwenye jimbo la kidini la Kurdi, lakini bado ni halali katika ukanda wa kati wa Iraq.
Kumekuwepo na dalili za kutokomeza ukeketaji. Miaka iliyofuata baada ya kuanzishwa kwa taasisi ya haki za wanawakee, Misri imekataza ukeketaji mwaka 2008. Sudani ikiwa katika kipindi cha mpito kisiasa baada ya miaka 30 ya udikteta, imekuwa ya kwanza kukataza ukeketaji hapo April.
Lakini utekelezaji wa sheria ni changamoto kubwa kwa sababu ukeketaji bado uko kwa kiwango cha juu na unakubalika pia umesambaa kwa sehemu kubwa .
Ingawa sheria sio silaha muhimu sana lakini bado hazijitoshelezi. Nchi zinahitaji mpango na mkakati wa kitaifa unaotekelezeka ukihusisha polisi, mahakama, watoa huduma za afya, makarani na kutoa elimu kwa jumuiya ya kijamii.
Mfululizo wa majanga ya kikanda na mamlaka za kidikteta imechelewesha mabadiliko yakizuia kampeni na rasilimali za kupambama na uvunjifu wa hali za wanawake.
Sasa macho yote ya ulimwengu yameelekezwa kwenye kupambana na COVID-19 na madhara yake katika uchumi na programu nyingi ambazo zinahusika moja kwa moja na haki za wanawake walio katika mazingira hatarishi na kutoa huduma za kijamii zimeahirishwa kwa au pengine sio kipaumbele tena. Kukiwa na familia nyingi maskini na wasichana wengi wanaoachishwa shule au ndoa utotoni, ukeketaji ni kama vile unaendelea kupata nafasi bila kujulikana katika ukanda huu.