Habari kuhusu Kuwait
Siku ya Wajinga: Waislamu Hawaruhusiwi Kudanganya Kamwe
Pamoja na maonyo, kwamba kufuata mkumbo wa Siku ya Wajinga Duniani kidini adhabu yake ni moto wa milele, watumiaji wa mitandao Uarabuni, waliitumia siku hii kuzikosoa serikali zao.
Misri: Ushauri kwa Waandamanaji wa Kuwait
Wakati watu wa Kuwait walipoanzisha maandamano makubwa ambayo hayakuwahi kutokea ya kuonesha waziwazi kutokukubaliana na mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yaliyopitishwa chini ya mtawala wa kurithi kufuatia kuvunjwa kwa bunge, watu wa Misri wametumia muda wao mwingi katika Twita wakitoa ushauri kwa watu wa Kuwait kuhusiana na yapi ya kufanya na yapi ya kutokufanya.
Kuwait: Nampenda Osama Bin Laden
Mwandishi wa makala wa Kuwait Khulood Al-Khamisametangaza mapenzi yake ya dhati kwa kiongozi wa ugaidi Osama Bin Laden, anasema kuwa anasubiri kuungana naye ahera ili aweze kutimiza ndoto yake. Kwenye Twita watu wa Kuwait wanaeleza kustushwa kwao na makala hiyo pamoja na hisia za moyoni za Al-Khamis.