Habari kuhusu Bahrain
Uandishi wa Habari ni Kosa la Jinai Nchini Bahrain
Mwandishi wa habari wa Marekani, Anna Therese Day pamoja na wenzake walishikiliwa nchini Bahrain, na kisha kurudishwa nchini mwao wakati wa kumbukumbu ya miaka mitano ya maandamano ya kuipinga serikali ya nchini Bahrain.
Zaidi ya Habari za Kombe la Dunia: Machozi Brazil, Mabomu Bahrain na Majanga Qatar
Unapaswa kujua zaidi ya kandanda kuelewa mashindano ya Kombe la Dunia. Deji Olukotun anachambua kwa kina masuala ya uhuru wa maoni na haki za binadamu.
Mwanablogu wa Kibahraini Takrooz Akamatwa
Mtumiaji wa mitandao ya kijamii wa Kibahraini Takrooz amekamatwa kwa madai ya "kuchochea chuki dhidi ya utawala" kwenye mtandao wa Twita.
Siku ya Wajinga: Waislamu Hawaruhusiwi Kudanganya Kamwe
Pamoja na maonyo, kwamba kufuata mkumbo wa Siku ya Wajinga Duniani kidini adhabu yake ni moto wa milele, watumiaji wa mitandao Uarabuni, waliitumia siku hii kuzikosoa serikali zao.
Rafiki Yangu Anateswa kwa Ku-blogu
Safy ni mtu wa kawaida aliyewahi kufanya kazi kama afisa wa Teknohama mpaka aliposhuhudia rafiki yake akipigwa risasi na polisi wa kutuliza ghasia wakati wa majuma ya mwanzo ya mapinduzi. Hakuweza kuendelea kuwa "mtu wa kawaida" baada ya tukio hilo.
Bahrain: ‘Kususia michezo ya Olimpiki’
Wa-Bahraini wengi wanatoa mwito wa kususuia michezo ya Olympics. Kwanza, mwana wa mfalme, ambaye amekuwa akituhumiwa kwa kujihusisha na utesaji wa wanariadha, anahudhuria michezo hiyo. Pili, sehemu kubwa ya timu ya nchi hiyo imetengenezwa na wanariadha wa ki-Afrika.
Mwaka Mpya na Mienendo ya Zamani Nchini Bahrain
Wakati nchi mbalimbali ulimwenguni kote zikiukaribisha mwaka mpya kwa fataki na shamrashamra, serikali ya Bahraini iliandaa utaratibu wa aina yake kwa waandamanaji nchini humo. kwa bahati, watumiaji wa mtandao wa intaneti walikuwa tayari, kuonesha na kuweka kumbukumbu ya baadhi ya matukio kwa ajili ya kushuhudiwa na sehemu nyingine yote ya ulimwengu.
Hakuna Usalama kwa Waandishi wa Kiraia Nchini Bahrain
Baada ya video ya "kibao" cha polisi wa Bahrain kusambaa sana mtandaoni, Waziri wa Mambo ya Ndani alitoa tamko akiomba kuwa yeyote aliyepiga picha tukio hilo aliripoti haraka kwa mamlaka zinazohusika. Siku mbili baadae, na kinyume na kauli hiyo, watu wengi walishangazwa na kukamatwa kwa mpiga picha.
Uarabuni: Sera ya Romney kwa Mashariki ya Kati Yaibua Mjadala
Hotuba ya Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Bw. Mitt Romney iliyoelezea sera yake ya nje imeibua mjadala mzito miongoni mwa raia wa mtandaoni leo hasa wale watokao katika nchi za ki-Arabuni. Twiti zinazohoji sera ya mambo ya nje ya Marekani kwa Mashariki ya Kati ziliendelea wakati ambao Romney, anayepeperusha bendera ya chama cha Republican, alipozungumza katika Chuo cha Jeshi cha Virginia. Endapo atachaguliwa, Romney ameahidi kuwa na sera rafiki za mambo ya nje, tofauti na mwelekeo usiotabirika wa sera za Obama wakati huu ambapo mabadiliko ya kisiasa yanaendelea kulikumba eneo la Mashariki ya Kati.
Makala za Global Voices Zilizosomwa Zaidi mwaka 2011
Global Voices haijabaki kuwa sauti pweke ya vyombo vya habari vya kiraia linapokuja suala la twita zinazotuma taarifa na posti za kwenye blogu. Bado, hata hivyo pale ambapo shauku kwa vyombo vikuu vya habari ikindelea kupungua, sisi ndio tunaojibidiisha kuendelea kuweka kumbukumbu ya kile ambacho wanablogu wadogo popote pale waliko wanahitaji dunia ikifahamu. Fahamu orodha ya makala zetu 20 zilizosomwa zaidi kwa mwaka 2011