Uandishi wa Habari ni Kosa la Jinai Nchini Bahrain

American journalist Anna Therese Day was arrested in Bahrain for covering protests to mark the fifth anniversary of Arab Spring-like protests which still continue. Photograph shared on social media after Day's arrest

Mwanahabari wa Marekani, Anna Therese Day alitiwa nguvuni nchini Bahrain alipokuwa akiripoti maandamano ya kumbukumbu ya miaka mitano ya maandamano ya mageuzi ya Uarabu mpya yanayozidi kushamiri. Picha iliyopakiwa kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya Day kukamatwa(Chanzo cha picha: frontlinefreelance.org)

Mwanahabari wa Marekani aliyejizolea tuzo Anna Therese Day alishikiliwa nchini Bahrain akiwa na wenzake watatu ambao pia ni raia wa Marekani kwa sababu ya kuripoti maandamano ya kumbukumbu ya miaka mitano ya maandamano ya mageuzi ya Uarabu mpya nchini Bahrain.

Mapema tarehe 16 Februari, Day na wenzake walilazimishwa kurudi nchini mwao mara baada ya kushikiliwa kwa siku moja. Wanahabari hawa walishikiliwa wakati wa maandamano ya huko Sitra na kutuhumiwa kwa kushiriki maandamo yasiyo rasmi pamoja na kuingia nchini Bahrain kwa udanganyifu.

Mara kadhaa Bahrain imekuwa ikiwakataza wanahabari wa kigeni kuingia nchini humo(Shirika la Kufuatilia Kuminywa kwa Uhuru wa Kupata Taarifa limeweka taarifa ya kina hapa) ikiwa ni pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali na wanaharakati wa haki za binadamu— kimsingi ni pamoja na yeyote ambaye ataikosoa serikali kwa kitendo chake cha kuzuia maandamano, uhuru wa kiraia, uhuru wa kujieleza pamoja na haki za binadamu.

Kwa mfululizo wa jumbe za Twitter, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain inamtuhumu Day pamoja na wenzake kwa kushiriki kwenye maandamano “yasiyo halali”:

Raia wanne wa Marekani wanashikiliwa mara baada ya mmoja wao kukutwa akishiriki kwenye maandamano pamoja na waandamanaji na akiwa amejifunika uso wake huko Sitra

Waliobaki walikamatwa katika kituo cha uangalizi cha polisi katika eneo hilo la Sitra

Waliokamatwa waliingia nchini Bahrain kati ya Februari 11 na 12 na kutoa taarifa za uongo kwa mamlaka husika wakidai kuwa walifika nchini Bahrain kwa ajili ya kutalii

Walioshikiliwa walikuwa wakijihusisha na uandishi wa habari bila ya kibali na pia kufanya mambo ambayo ni kinyume na sheria. Taratibu za kisheria zimeshachukuliwa dhidi yao na wameshafikishwa kwa mwendesha mashtaka wa serikali.

Mashitaka dhidi ya waandishi wa habari ya kuvunja sheria kwa sababu ya kukusanya habari siyo jambo geni nchini Bahrain. Hivi karibuni, mwnahabari mpiga picha Ahmed Al Fardan alihukumiwa kwenda jela miezi mitatu kwa kupiga picha maandamano. Alituhumiwa kwa kosa la “kutaka” kuandamana. Kuwatuhumu waandishi wa habari kushiriki kwenye maandamano ni jambo ambalo halikuachwa nyuma na wanaharakati na marafiki waliopaza sauti zao mara baada ya kushikiliwa kwa Day.

Kupitia Twitter, mwandishi wa habari C. Robert Gibson aliwaomba marafiki wake wasikae kimya kuhusu tukio hili:

Wengine kama akina Sally Kohn, walishinikiza kuachiliwa kwa Day kupitia kiungo habari #JournalismIsNotACrime:

Uandishi wa habari nchini Bahrain ni kosa la jinai. Mwandishi wa habari wa Bahrain Nazeeha Saeed anafahamu. Siyo tu kwamba walimfanyia ukatili kutokana na kutimiza wajibu wake, lakini waliomfanyia ukatili walionekana hawakuwa na hatia. Hivyo tu.

Kwa mujibu wa Kamati ya kuwatetea Wanahabari , Bahrain ni “moja ya nchi inayokithiri kwa kuwafunga gerezani waandishi wa habari katika ukanda wa nchi za Kiarabu”:

Nchi ya Bahrain ambayo ni kisiwa kidogo chenye watu milioni 1.3 (ambao takribani nusu ya idadi hii wakiwa ni wafanyakazi wa kigeni) imeshashuhudia ukatili wa kupindukia wa kuzuia mapinduzi ya umma yaliyoanza mapema tarehe 14 Februari, 2011. Wanaharakati wameshateswa, uawa na hata kufungwa jela.

Amnesty International, shirika linaloongoza kwa kufuatilia haki za binadamu lilichapisha ripoti kadhaa wakati wa kuelekea kwenye maadhimisho ya tarehe 14 Februari kwa lengo la kuweka bayana hali ilivyo hatari kwa waaandamanaji nchini Bahrain. James Lynch, Naibu Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati na programu ya Afrika ya Kaskazini alisema:

Kwa hali ilivyo sasa nchini Bahrain, kwa yeyote anayejaribu kuikosoa serikali- ama iwe ni mwanaharakati wa haki za binadamu au mwanasiasa-anajitakia mateso […] Mbali na serikali kuahidi kuvishitaki vyombo vya dola vilivyohusika na vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu mwaka 2011, watu wa Bahrain bado wanatumaini kuwa haki itatendeka. Taasisi zinazojitokeza kutetea haki za binadamu siyo tu zimeshindwa kufanya uchunguzi huru, au hata kuwawajibisha wahusika, kwa sasa baadhi ya taasisi hizi zinaonekana kutumika kufunika maovu yanayoendelea kutendeka.

Miaka mitano sasa, maandamano yanaendelea, lakini ni ya wastani na ya ukimya . Kwa sasa, kuandamana, au “mikusanyiko” ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria na pia vijiji vipo chini ya ulinzi usiku na mchana.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.