GV Face: Alaa Abd El Fattah na Maryam Al Khawajah Wazungumzia Mgomo wa Kula, Kufungwa na Harakati zao Nchini Misri na Bahrain

Mpaka majuma machache yaliyopita,  Maryam Al Khawajah na Alaa Abd El Fattah walikuwa kwenye mgomo wa njaa gerezani. Alama ishara zinazodai kuachiliwa kwao huru kutoka kwenye magereza ya Bahrain na Misri zilitawala mtandao wa Twita. 

Wanaharakati hawa maarufu wanaungana nasi kwenye toleo la wiki hii la GV Face wakiwa huru, lakini mapambano yao hayana dalili ya kumalizika.
 
Maryam kwa sasa yuko Copenhagen, hana nafasi ya kumwona baba yake, ni mwanaharakati wa Bahrain aliyekuwa kifungoni akiongoza mgomo wa kula mara mbili tangu mwaka 2011.
 
Nchini Misri, Alaa alitolewa kwa dhamana muda mfupi baada ya kumaliza mgomo wake wa kula uliodumu kwa siku 40 na kumalizika majuma kadhaa yaliyopita. Kwa sasa anasubiri kushitakiwa na haruhusiwi kusafiri. Dada yake mdogo mwenye umri wa miaka 20 bado anaendelea na mgomo wake wa kula unaoingia siku ya 47 akiwa gerezani. nbsp; 
 
Mamia wa wafungwa wa kisiasa wanaendelea na mgomo wa kula nchini Misri na Bahrain. 
 
Maryam na Alaa wamekuwa waki-twiti mapambano yao ya kila siku kwa miaka mitatu, tangu ‘Mapinduzi ya Uarabuni’  yatawale fikra za mamia ya maelfu duniani kote. Alaa ana wafuasi zaidi ya laki 6.36 na  Maryam ana wafuasi wanaokaribia laki 1 kwenye mtandao wa twita.
 
Nchini Misri, baadhi ya wafungwa wanaofanya mgomo wa kula wamekuwa magereza tangu maandamanaji yanayopinga utawala wa nchi hiyo mnamo Januari 25, 2011. Bahrain, nchi ambayo imekuwa ikishuhudia maandamano ya kupinga utawala wa nchi hiyo tangu Februari 14, 2011, zaidi ya wafungwa 600 wameingia wenye mgomo kupinga mateso wanayoyapata wakiwa gerezani.
 
Katika toleo la wiki hii tunazungumza na Allan a Maryam kuhusiana na harakati zao, mapambano wanayokabiliana nchini  Bahrain na Misri pamoja na matumaini yao yanayowafanya wawe na moyo imara kuhusiana na mustakabali wa nchi yao.
 
Alaa alifungwa au kuchunguzwa kila awamu ya Urais wa nchi hiyo. Mwaka 2006, alikamatwa kwa kushiriki mandamano ya amani. Mwaka 2011, aliwekwa ndani kwa miezi miwili, akijikuta akikosa kuzaliwa kwa mwanae wa kwanza. Mwaka 2013, alikamatwa na kuwekwa ndani kwa siku 115 bila kufunguliwa mashitaka. Na sasa anakabiliana na hukumu ya miaka 15 jela. 
 
Maryam alikamatwa kwenye uwanja wa ndege mwishoni mwa mwezi Agosti, alipojaribu kuingia nchini Bahrain kukutana na baba wa mwanaharakati wa haki za binadamu alikuwa amefungwa tangu mwezi Aprili 2011. Baba yake alikuwa kwenye siku yake ya 27 ya mgomo wake wa pili wa kula. Zaidi ya wafungwa wa kisiasa wamekuwa kwenye mgomo wa kula nchini Bhrain kupinga kuteswa magerezani, tangu Februari 14, 2011, maandamano yalipoanza. Baada ya Maryam kukamatwa kwenye uwanja wa ndege, alituhumiwa kumpiga mmoja wa polisi. Maryam anakana mashtaka yake. Akiwa gerezani, alianza mgomo wa kutokula. Aliachiliwa huru mnamo  Septemba 19 na tangu wakati huo amehama nchi. Baba yake bado yuko gerezani. Maryam ni mkurugenzi mwenza waKituo cha Ghuba ya Arabuni cha Haki za Binadamu  

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.