Zaidi ya Habari za Kombe la Dunia: Machozi Brazil, Mabomu Bahrain na Majanga Qatar

A young woman stages a lone protest against FIFA in front of the Maracana stadium after Belgium played Russia in their group stage match on June 22, 2014, despite a large security cordon designed to block such demonstrations against the 2014 World Cup. Photo by Marcelo Fonseca. Copyright Demotix.

Binti akiandamana kivyake kuipinga FIFA mbele ya Uwanja wa Maracana baada ya Ubelgiji kucheza na urusi katika makundi yao yaliyoandamana tarehe 22 Juni, 2014, pamoja na kuandaliwa kwa vikosi vya usalama kuyazuia maandamano hayo kinyume cha mashindano ya kombe la dunia. Picha na Marcelo Fonseca. Haki Milki ya Demotix.

Posti hii awali ilionekana kwenye tovuti ya Pen American Center na imechapishwa kwa mara nyingine kwa ruhusa.

Kama ilivyo kwangu, unaweza kuwa unaweza kuwa ulihisi unaota baada ya kutazama kipigo cha kufedhehesha cha Brazili kuchapwa mabao 7-1 na Ujerumani katika mashindano ya nusu fainali ya kombe la Dunia. Lakini ndivyo ilivyotokea. Wanablogu kutoka Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini  walionyesha masikitiko yao, huku mtumiaji mmoja wa mtandao wa Twita wa Bahraini akibaini kuwa kikundi cha ‘wapiga mabomu’ kilikuwa kinaondoka kwa namna ‘yenye sura ya kashfa’. Alikuwa anamaanisha hatua ya serikali ya Bahrain kutumia  mabomu ya machozi ya ki-Brazili kuwanyamazisha waandamanaji kwa kutumia nguvu (tahadhari, kiungo kina maudhui yenye kutisha).

Brazili itapokea kitita kisichopungua dola milioni 20 kwa kufuzu kwake nusu fainali ya Kombe la Dunia, lakini timu hiyo bado ina fursa ya kushinda dola milioni 2 nyinginezo kama itaishinda Uholanzi, iliyopoteza mchezo wake dhidi ya Ajentina, katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wa mashindano hayo. Fedha hizo zinawezakutumika  kuleta mabadiliko kwenye chama cha mchezo wa mpira wa miguu cha nchi hiyo.

Maandamano yaliendelea kwenye nchi hiyo, lakini si kwa kiwango kile kile kilichofanyika kabla ya mashindano hayo. Baadhi ya waandamanaji 300 kwenye jiji la Sao Paulo waligeuka na kuanza kudai kuachiliwa huru kwa waandamanaji waliokamatwa kabla, lakini bado polisi ilijibu madai hayo kwa kuwakamatwa wengine sita zaidi. Mashabiki wengi wanasafiri kwenye Brazili watakuwa hawajasikia chochote kuhusu muziki wa baile funk (aina ya dansi) kwa sababu ilipigwa marufuku kwa umaarufu wake wa uchezaji na sauti, ambayo ‘alamu’ za kipolisi na milio ya risasi.

Mashabiki wa Ajentina, wakati huo huo, wanaweza kusherehekea kwa sababu watakuwana fursa ya kutazama timu yao ikicheza dhidi ya Ujerumani katika fainali kama Lionel Messi, mmoja wapo wa wachezaji maarufu zaidi kuwahi kuwepo, atakavyokuwa akicheza na Ezekiel Lavezzi pembeni mwake kwa kumkabili. Lavezzi amevutia mashabiki zaidi  baada ya kumvuta jezi yake katika kusherehekea ushindi.

Kuhusu ubaguzi wa rangi, inaonekana mambo hayakuwa shwari sana. Chombo kikuu cha kandanda duniani FIFA kimeonyesha migawanyiko ya ndani kwa ndani kuhusu kupambana na ubaguzi wa rangi kwenye mashindano haya. Kikosi kazi cha FIFA dhidi ya ubaguzi wa rangi  kilifika mahali pa kutokukubaliana na maamuzi ya kamati ya nidhamu  kuachana na adhabu dhidi ya mashirikisho ya mataifa kadhaa kwa maneno ya kushangilia yaliyokuwa na sura ya ubaguzi wa rangi na kimapenzi yaliyotolewa na mashabiki ambayo hayakuwa yakilengwa kwa wachezaji fulani fulani, bali kwa timu nzima.

Maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 huko Qatar tayari yameingia dosari kufuatia taarifa za kufa kwa wafanyakazi wa ujenzi 400 wa Nepal na 700 wa Kihindi katika hali ya hewa inayokaribia nyuzi 122 za Fahrenheit (nyuzi 50 Celsius).

Hata hivyo, profesa mmoja wa uandishi wa habari katika nchi hiyo anasihi kuwa maandamano hayolazima yaendelee kufanyika kwa sababu yataruhusu shinikizo zinaloendelea kuhusu Qatar kuboresha rekodi yake ya haki za binadamu. Pia alishiriki kuandika moja ya maandishi muhimu zaidi kuwahi kuandikwa kuhusu mitazamo ya kijamii kwa vyombo vya habari katika eneo la Mashariki ya Kati, ambalo unaweza kulisoma katikatovuti hii bora inayoshirikisha wasomaji wake. Utafiri wake uligharamiwa na Mfuko wa Qatar, shirika lile lile linalofadhili timu ya mpira ya Barcelona, anayoichezea Lionel Messi. Mfuko huo umefadhiliwa kwa sehemu na serikali ya Qatar. Bado unafuatilia? Kuwa refa.

Wafuatialiaji wa masuala ya michezo mara nyingi huzungumza kuhusu namna wanavyopenda kutazama kandanda lililo huru. Tutashangilia kutiririka kwa mawazo kwenye mchezo wa fainali. Tunaitakia timu bora kushinda.

Taarifa za nyongeza na Cassandra da Costa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.