Habari kuhusu Palestina
Miongo Minane Chuki Bado Ipo Kati ya Wajordani na Wapalestina
Ingawa kuishi pamoja kwa watu wawili huwafanya wawe na amani, ushirikiano mkamilifu bado haujawezekana kwenye baadhi ya maeneo ya maisha.
Msichana Achora Ramani ya Palestina kwa Kutumia Risasi za Israeli Alizokusanya Karibu na Nyumbani Kwao
Picha hii ya msichana wa ki-Palestina inazunguka kwenye mitandao ya kijamii. Taarifa zinasema msichana huyu alikusanya maganda ya risasi karibu na nyumbani kwao, akayatumia kuchorea ramani ya Palestina.
Katika Picha: Gaza Yaadhimisha Eid Al-Adha
Ikiwa na zaidi ya Wapalestina 2,000 waliojeruhiwa katika mashambulizi ya hivi karibuni yaliyofanywa na Isralei katika Ukanda wa Gaza, raia bado wanaona leo hii kuna kila sababu ya kusherehekea sikukuu ya Kiislam ya Eid Al-Adha.
PICHA: Wapelestina Wanatufundisha Namna ya Kuishi
Mpalestina Sayel anatwiti kwa wafuasi wake 1,800 kwenye mtandao wa Twita picha ifuatayo ya wakazi wa Gaza wakipanda maua kwenye maganda ya silaha za Israeli. Anasema: Palestinians from the Gaza...
Picha: Mwonekano wa Maroketi Yakiruka Kwenye Anga la Gaza Kutoka Angani
Kutoka kwenye anga la mbali, mwanaanga Alexander Gerst anatazama namna Gaza inavyowaka moto. Anatwiti: My saddest photo yet. From #ISS we can actually see explosions and rockets flying over #Gaza...
Israel Yaanza Operesheni ya Ardhini Gaza
Vikosi vya kijeshi vya Israeli vimeanza kuingia Gaza, baada ya siku kumi za mapigano yaliyogharimu maisha ya wa-Palestina 200. Hatua hiyo inafuatia Hamas kukataa pendekezo la kusitisha mapigano lililotolewa na Misri.
Madege ya Kijeshi ya ki-Palestina Yaruka kwenye Anga la Israel
Brigedi ya Palestina ya Al Qassam, tawi la kijeshi la Hamas, lilionyesha miundo mitatu ya madege ya kijeshi leo, ikisema kuwa yalirushwa kwenye anga la Israel. Mwandishi Dima Khatib anatwiti:...
Waandishi wa kimataifa Wakashifu Israeli kwa Kuendelea kwa Ujenzi wa Makazi
Waandishi kumi na sita wa kimataifa ambao walishiriki katika Tamasha la Wapalestina la Fasihi, lililofanyika katika miji kadhaa Palestina kuanzia Mei 31 hadi Juni 5, walitoa taarifa kukashifu Israeli kwa...
Ni Sikukuu ya Kuzaliwa Kristo (Noeli) Mjini Betlehemu
Ni sikukuu ya kuzaliwa Kristo mjini Betlehemu, katika ukanda wa Magharibi, Palestina, mahali alipozaliwa Yesu Kristo. Ni namna gani nzuri ya kusherehekea tukio hili zaidi ya kuwashirikisha picha na maoni mbalimbali ya watumiaji wa mtandao wa intaneti kuhusiana na tukio hili linalosherehekewa na mabilioni ya watu duniani kote.
Uarabuni: Sera ya Romney kwa Mashariki ya Kati Yaibua Mjadala
Hotuba ya Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Bw. Mitt Romney iliyoelezea sera yake ya nje imeibua mjadala mzito miongoni mwa raia wa mtandaoni leo hasa wale watokao katika nchi za ki-Arabuni. Twiti zinazohoji sera ya mambo ya nje ya Marekani kwa Mashariki ya Kati ziliendelea wakati ambao Romney, anayepeperusha bendera ya chama cha Republican, alipozungumza katika Chuo cha Jeshi cha Virginia. Endapo atachaguliwa, Romney ameahidi kuwa na sera rafiki za mambo ya nje, tofauti na mwelekeo usiotabirika wa sera za Obama wakati huu ambapo mabadiliko ya kisiasa yanaendelea kulikumba eneo la Mashariki ya Kati.