Hakuna Usalama kwa Waandishi wa Kiraia Nchini Bahrain

Posti hii ni sehemu ya habari zetu maalumu za Maandamano ya Bahrain 2011.

Baada ya  video ya “kibao” cha polisi wa Bahrain kusambaa sana mtandaoni Waziri wa Mambo ya Ndani alitoa tamko akiomba kuwayeyote aliyepiga picha tukio hilo aliripoti haraka ” kwa mamlaka zinazohusika. Siku mbili baadae, na kinyume na kauli hiyo, watu wengi walishangazwa na kukamatwa kwa mpiga picha.

Picha ya Mpiga picha Ahmed Humaidan na uanachama wake wa chama cha wapiga picha wa MArenani. Ilichapishwa na @ahmedalfardan1

Shirika la Ulaya-Bahraini linaloshughulikia Haki za Binadamu lilitwiti:

@EBOHumanRights: Ahmed Humaidan kutoka Kituo cha Biashara cha Jiji la Bahrain amekamatwa na bado hajulikani aliko tangu jana usiku.

Mpiga picha Ahmed AlFardan aliongeza:

@AhmedAlFardan2: Zaidi ya polisi kanzu 15 walimkamata Humaidan kutoka katika Kituo cha biashara Jijini Bahrain  #freehumaidan #freebhphotographer #sitrapic.twitter.com/pSeM9YgJ

Sayed Hassan aliandika:

@WLEXT: Siku ya huzuni kwa wapigapicha & Journos nchini #Bahrain, Mshindi wa Tuzo ya Mwandishi wa kiraia wa picha #FreeHumaidan amekamatwa jana pic.twitter.com/c4ak9VFH

Picha ya Ahmed Humaidan akiwa na baadhi ya picha zake ziliozsababisha ashinde na tuzo alizopokea

Mwandishi wa Kuwaiti na mwanaharakati wa haki za binadamu Hadeel Buqrais alitwiti:

بعد افلات قتلة المصور أحمد اسماعيل يتم استهداف المصور احمد حميدان في البحرين بإعتقاله

@HadeeLBuQrais: Baada ya mauaji ya mpiga picha Ahmed Ismail mwingine aliyekimbia Ahmed Humaidan analengwa na amekamtwa.

Ahmed Ismail ni mpiga picha za video ambaye aliuawa mjini Salambad mwaka jana (2011) wakati alipiga picha za maandamano. Alipigwa risasi kutoka kwenye gari la kiraia.

Kituo cha Doha cha Uhuru wa Habari kilitoa tamko lililosema:

Kituo cha Doha cha Uhuru wa Habari kinaungana na utafutaji wa habari unaofanywa na Jamii ya Vijana wa Bahrain inayotetea Haki za Binadamu inayotoa wito wa kuachiliwa huru kwa Humaidan.

Humaidan ameshinda zaidi ya tuzo za kimataifa 140 katika tasnia ya uandishi wa habari picha, na anachukuliwa kuwa mpigapicha bora wa pili wa Nchi za Kiarabu kushinda katika mashindano ya upigaji picha.

 

Zainab Hashemi aliongeza:

دائماً يخافون ممن ينشر عنفهم و تعنجهم لذا إختطفوه ، غداً ستصفق سميرة رجب و تقول كعادتها : لدينا حرية في الصحافة في البحرین

@ZainaBHashemi: Siku zote wanamwogopa yeyote anachapisha picha kuonyesha matumizi yao ya nguvu na ujeuri ndio maana walimkamata. Kesho Sameera Rajab [waziri wa Nchi anayesughulikia Mambo ya Habari] atasema kama tulivyozoea: tunao uhuru wa habari nchini Bahrain

Posti hii ni sehemu ya habari zetu maalumu za Maandamano ya Bahrain 2011.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.