Siku ya Wajinga: Waislamu Hawaruhusiwi Kudanganya Kamwe

Muslims don't lie .. No to April Fool's. Photo credit: @al_tarb_al_a7mr

Waislamu hawadanganyi …Hatuna siku ya wajinga. Picha: @al_tarb_al_a7mr

Pamoja na maonyo, kufuata mkumbo wa Siku ya Wajinga kungesababisha hukumu ya moto wa milele kwa kuwa Waislamu hawapaswi kudanganya, watumiaji wengi wa mtandaoni Uarabuni kote, waliamua kuzikosoa serikali zao siku hii.

Kutoka Saudi Arabia, Abdelrahman Al Kanhal anatania:

King Abdulla amekubali mradi mpya wa kuendeleza mahakama na elimu

Na anaongeza:

Nchi hiyo ya kifalme imechukua hatua madhubuti kumaliza tatizo la msongamano wa magari barabarani

Na akikumbushia kuzuiwa kwa wanawake kuendesha magari nchini humo, anaendelea kuandika:

Jamii yenyewe ndiyo yenye kuamua ikiwa ni haki kwa wanawake kuendesha ama la. Na hatuwapingi wanawake kuendesha ila tu kuwapeleka jela kama wataendesha kitendo kilicho kinyume na matakwa ya jamii

Wakati huo huo, Mmsri Adham Morad anadanganya kuhusu kutudi kwa Rais Mohamed Morsi kiongozi wa Muslim Brotherhood aliyeng'olewa madarakani hivi karibuni:

Morsi amerudi!!

Na, bado nchini Misri, Adilovic ana matamanio yake ya kimawazo. Anatwiti:

Serikali ya Misri imeamua kuongeza mishahara, ruzuku, imeongeza bajeti ya huduma za elimu na afya na kuwapa wa-Misri maisha bora, uhuru na haki za kiraia

Kutoka Bahrain, Ammar Al Aradi, anawtiti mfululizo wa utani wa Siku ya Wajinga, ambao watu wengine walidhani ni kweli. Anabainisha:

Huu ni mmoja wa utani wake:

Kuwait imehalalisha mirungi kwa ajili ya matumizi ya kitabibu baada ya ushahidi kuonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya vijana nchini humo tayari wanaitumia

Tukirudi nchini Saudi Arabia, Ahmed Al Maani anahitimisha:

Siku ya wajinga Duniani itakuwa inachosha tu kwa Waarabu kwa sababu haina lolote lisilofanywa na Waarabu siku nyingine

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.