Uarabuni: Sera ya Romney kwa Mashariki ya Kati Yaibua Mjadala

Hotuba ya Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Bw. Mitt Romney iliyoelezea sera yake ya nje imeibua mjadala mzito miongoni mwa raia wa mtandaoni leo hasa wale watokao katika nchi za ki-Arabuni.

Twiti zinazohoji sera ya mambo ya nje ya Marekani kwa Mashariki ya Kati ziliendelea wakati ambao Romney, anayepeperusha bendera ya chama cha Republican, alipozungumza katika Chuo cha Jeshi cha Virginia. Endapo atachaguliwa, Romney ameahidi kuwa na sera rafiki za mambo ya nje, tofauti na mwelekeo usiotabirika wa sera za Obama wakati huu ambapo mabadiliko ya kisiasa yanaendelea kulikumba eneo la Mashariki ya Kati. Alisema piaangewapa mafunzo ya kijeshi waasi wa Kisyria, angalau wale wenye mtazamo unaofanana na wake.

Akiandika kutoka Venezuela, mwandishi Dima Khatib hakupendezwa na maneno hayo. Alituma twiti[ar]:

ما كان ناقص غير مرشح رئاسي أمريكي كمان يستخدم سوريا في حملته الانتخابية للترويج لنفسه.. عأساس هو أحسن من أوباما !! كملت والله


@Dima_Khatib
: Tulichokikosa kwa muda sasa ni mgombea Urais wa Marekani kuitumia Syria katika kampeni zake za uchaguzi kwa lengo la kujitafutia umaarufu wa kisiasa kwa madai kwamba yeye ni bora kuliko Obama!!! Mkakati umekamilika

Anauliza:

لسا في حدا بهالعالم ما مص دم الثورة السورية مشان مصلحة ما ؟


@Dima_Khatib
: Kuna aliyebaki ambaye hajanyonya damu ya mapinduzi ya Syria kwa maslahi yake mwenyewe?

Raia wa Algeria Imad Mesdoua anasema:

@ImadMesdoua: #Romney anaifahamu vizuri Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Aliiona #Libya na akapata wazo hilo alilonalo, kuwapa waasi wa #Syria mafunzo ya kijeshi! #letmeknowhowthatworksoutforyou (naomba kujua namna inavyowezekana kwako)

Shadi Hamid, kutoka Kituo cha Brooking Doha, nchini Qatar, anaandika:

@shadihamid: Hotuba ya Romney kuhusu Mashariki ya Kati inaweza kuwa muhimu. Angalau sasa tunaweza kutazamia hotuba hiyo imsukume Obama kufafanua sera yake, ambayo kwa kweli imekuwa haieleweki sawa sawa

Anaongeza:

@shadihamid: Suala la Marekeni “kuongoza” au “kuongoza kutokea nyuma” ni halisi na halipaswi kupuuzwa. Mashaka halisi kuhusu nguvu ya Marekani kutatua na kukaa katika nchi za ki-Arabu.

Mwanaharakati wa haki za binadamu wa Bahraini Maryam Al Khawaja anasema:

@MARYAMALKHAWAJA: Kwa kupima matamshi yake tu, #Romney atakuwa janga kubwa kwa masuala ya haki za binadamu katika Baraza la Ushirikiano la Ghuba [Gulf Cooperation Council], zaidi sana kuliko #Obama… #bahrain

Na Mhariri Mtendaji wa Sera za Nje Blake Hounshell anakubaliana na hayo:


@blakehounshell
: Kitu kimoja ambacho Romney na Obama wanaonekana kukubaliana: Kuindoa Bahrain katika orodha ya mapinduzi ambayo Marekani inayaunga mkono.

Wakati raia wa Qatar Shayma Al-Naimi, anayesoma nchini Marekani, alitwiti:

@iShayma: #Romney anataka kweli kuzungumzia “rekodi ya Marekani” katika historia ya amani????

Na anaongeza:


@iShayma
: Kwa dhati kabisa siwezi kuamini kile anachokisema #Romney kwa sasa! Inakera kwa kweli. Inasikitisha kujua kwamba watu wenye mtazamo kama wake nao wapo.

Mpalestina Iyad El-Baghdadi, anayetwiti akiwa Dubai, anaangaliza:

@iyad_elbaghdadi: Mara ya mwisho Marekani imeonyesha “Uongozi katika Mshariki ya Kati”, wa-Iraq wapatao 600,000 walipoteza maisha yao.

Na anapendekeza suluhu:


@iyad_elbaghdadi
: Nusu ya yaliyoandikwa kwenye ukurasa wangu inasema Obama hafai, na nusu nyingi inasema Romney hafai. Jamani, ninakubaliana na ninyi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.