Kichwa hiki cha habari lazima kiwe moja ya mambo yasiyovutia kabisa anayoweza kuyaandika mwandishi wa habari, na mada hii lazima itakuwa kwenye kundi la mada zisizoandikwa mara nyingi, lakini kwa somo ninalotaka kuliandikia nilidhani ni lazima kuweka pembeni kila nilichowahi kufundishwa na hivyo nitaandika kwa kutumia ujuzi wa kijima.
Makala hii ilikuwa ihusu kukamatwa kwa Zainab Alkhawaja, mwanaharakati maarufu nchini Bahrain. Nilikuwa nianze na maelezo ya ufafanuzi, ambayo yangejikita kwenye kukamatwa kwake kufuatia twiti iliyokuwa na hotuba yake iliyoandikwa na dada yake Maryam:
Urgent: Zainab Alkhawaja walked into court, asked to speak. She said to judge: ” I'm the daughter of a proud & free man…” CONT'D #Bahrain
— Maryam Alkhawaja (@MARYAMALKHAWAJA) October 14, 2014
Dharura: Zainab Akhawaja ameingia mahakamani, ameombwa kuzungumza. Amemjibu jaji: “mimi ni binti wa mtu ajisikiye fahari na aliye huru…”
#PT ” my mother brought me into this world free and i will give birth to a free baby boy even if it is inside ur prisons.” CONT'D #Bahrain
— Maryam Alkhawaja (@MARYAMALKHAWAJA) October 14, 2014
Mama yangu alinileta duniani nikiwa huru na mimi kadhalika nitamzaa mtoto aliye huru hata kama nitakuwa gerezani
#PT ” It is my right… and my responsibility.. as a free person.. to protest against oppression and oppressors.” CONT'D # Bahrain
— Maryam Alkhawaja (@MARYAMALKHAWAJA) October 14, 2014
Ni haki yangu…ni wajibu wangu…kama mtu huru….kuandamana kupinga ukandamizaji na wakandamizaji
#PT She then ripped a picture of the king and placed it in front of the judge. Zainab is at risk of arrest now; 8 months pregnant #Bahrain
— Maryam Alkhawaja (@MARYAMALKHAWAJA) October 14, 2014
Na kisha alichana picha ya mfalme mbele ya Jaji. Zainab yuko kwenye hatari ya kifungo; ni mjamzito wa miezi nane
Ningegusia baadhi ya miitikio ya watu iliyotokana na kitendo hicho cha Maryam, mfano watu wangapi walianz akufanya jambo kama hilo la kuchana picha ya mfalme, kumwuunga mkono:
.@monakareem In solidarity with @angryarabiya I'm tweeting #ArrestMeWithZainab Join me! pic.twitter.com/2hArn15UFs
— Linda (@SE25A) October 14, 2014
@monakareem Ninamwuunga mkono @angryarabiya Ninatwiti kwa ajili ya #NifungePamojaNaZainab Ungana nami! pic.twitter.com/2hArn15UFs
Au video hii ya You Tube inayoonesha namna Hitler angeweza kuguswa na kitendo hicho:
Lakini hilo silo ninalodhani ni la maana. Ninadhani katika makala hii napaswa kumkabili Ibilisi na kukiri kwamba pamoja na kwamba ni kiasi gani mtindo wa kuandika unamsaidia mtu anayejaribu kukwepa zimwi na wahusika , wakati mwingine huwa ni njia ya kilaghai kujaribu kukuza mambo. Ninatumia neno ‘kukuza’ kwa sababu ninadhani kwamba mwandishi mzuri ni kama msanii: ijapokuwa mchoro waweza kufanana na msichana, bado unakuwa ni ubunifu wa mwonekano wa msichana huyo, tabia yake na tabasamu lake, na hayo ndiyo yanayotuambia zaidi na kutufanya tufikiri.
Sisi waandishi hatutarajiwi kuandika hisia zetu, isipokuwa kuripoti vile vinavyohusika na kitendo vinafanyaje na kusemaje. Lakini kile alichokifanya Zainab Alkhawaja hakikuwa kitendo cha kufanya kiandikwe kiasi kile kwenye vyombo vya habari—lengo lilikuwa kila mmoja wetu, kokote duniani na kwenye kazi yoyote aelewe. Tendo hilo lilikusudiwa kutukumbusha kwamba tabia za kikorofi si tu ni namna ya kukufanya uishi, lakini ndizo zinazotufanya tuwe wanadamu. Hiyo ndiyo dhambi ya asili ambayo kila mmoja wetu ameirithi. Ukorofi, uliofanywa na Zainab, haukuwa chambo cha kutaka kuonekana: kwa sababu hata uonekane namna gani bado haikusaidii unapokuwa gerezani, na wale wanaotaka kuonekana watatumia kuonekana huko wakiwa nje ya gereza. Zainab hakuwa anatafuta jukwaa, hakuwa anasaka kusimama mbele ya vipaza sauti na kupigwa picha akiwa na watu wa tabaka la juu miongoni mwa wanasiasa. Kwake, ukorofi ulikuwa ni mtindo wa maisha.
Sina maneno sahihi ya kueleza kile ninachotaka kukisema isipokuwa kwa kutumia shairi hili liloandikwa na Amal Dunqul:
يا اخوتي الذين يعبرون في الميدان مطرقين
منحدرين في نهاية المساء
في شارع الاسكندر الأكبر :
لا تخجلوا ..و لترفعوا عيونكم إليّ
لأنّكم معلقون جانبي .. على مشانق القيصر
فلترفعوا عيونكم إليّ
لربّما .. إذا التقت عيونكم بالموت في عينيّ
يبتسم الفناء داخلي .. لأنّكم رفعتم رأسكم .. مرّه !
” سيزيف ” لم تعد على أكتافه الصّخره
يحملها الذين يولدون في مخادع الرّقيق
و البحر .. كالصحراء .. لا يروى العطش
لأنّ من يقول ” لا ” لا يرتوي إلاّ من الدموع !
.. فلترفعوا عيونكم للثائر المشنوق
فسوف تنتهون مثله .. غدا
و قبّلوا زوجاتكم .. هنا .. على قارعة الطريق
فسوف تنتهون ها هنا .. غدا
فالانحناء مرّ ..
و العنكبوت فوق أعناق الرجال ينسج الردى
فقبّلوا زوجاتكم .. إنّي تركت زوجتي بلا وداع
و إن رأيتم طفلي الذي تركته على ذراعها بلا ذراع
فعلّموه الانحناء !
علّموه الانحناء !
Eh akina kaka mnaovuka uwanja wa mapambano huku mkiwa mmeinamisha vichwa
Mlioshindwa na machweo ya siku
Msione haya na niangalieni
kwa sababu mmesulubiwa pembeni mwangu na kitambaa cha Kaisari
Inueni macho yenu na mnitazame, kwa sababu macho yenu yamekutakana na kifo ndani yangu
Upekwe ndani yenu utageuka kuwa tabasamu kwa kunyanyua kichwa japo mara moja
Ramani imetupa mizigo yake
sasa imewaelemea waliozaliwa utumwani
Bahari ni kama jangwa, haisikii kiu
Kwa sababu kiu cha waasi hukatwa na machozi
Mtazameni mwasi aliyetundikwa
Kesho mtaishia kuwa kama yeye
‘mwabusu wake zenu hapa katikati ya barabara
kwa sababu hapo ndiko mtakakoishia
kwa kuwa kupiga magoti ni kuchungu
na buibui anatengeneza kiwambo chake kwenye mabega ya mwanadamu
Wabusuni wake zenu…nilimwacha mke wangu bila kumbusu
Na kama mtawaona wanangu niliowaacha mikononi mwake wakikosa kukumbatiwa
wafunzeni namna ya kupiga magoti
Mungu hakumsamehe Ibilisi aliposema hapana
Wapole
Watairithi nchi
Kwa sababu hawasulubiwi
Kwa hiyo wafunzeni namna ya kunyenyekea
Ningependa kuendelea kuandika makala hii yenye mrengo unaoonekana wazi, lakini orodha ya watu waliokufa na ndoto zilizouawa, ziliuawa kwa sababu zilisemwa ni ukorofi, na hazijai kwenye kizingiti cha maneno elfu moja. Kwa sasa nawaacha na jina moja: Abdulhadi, ambaye hajazaliwa bado, na ambaye atakuwa huru, iwe gerezani au kwingineko.