Kumetokea Nini Kwenye Haki za Kidijitali kwa Miaka Saba Iliyopita? Toleo la 300 la Ripoti ya Raia Mtandaoni Litakueleza

waandamanaji katika Budapest, mwezi Oktoba 2014. Picha na Marietta Le na imetumika kwa ruhusa.

Taarifa ya raia mtandaoni ya Advox inatoa picha ya haraka kimataifa juu ya changamoto, ushindi na mienendo inayoibuka katika haki za kimtandao duniani.

Wiki hii katika kusherehekea toleo letu la 300, tunaangazia miaka saba iliyopita ya habari za haki ya kidijitali duniani!

Ripoti ya raia mtandaoni ilipoanzishwa mwaka 2011, tulianza kuweka rekodi ya kila wiki ya namna watu duniani wanavyotumia uhuru wa kutoa maoni kupitia teknolojia – na vikwazo na vitisho walivyokutana navyo.

Tumezungumzia kuongezeka kwa haki za kidijitali za harakati za kijamii kuanzia Hong Kong , Ukraine hadi Venezuela, mashambulizi juu ya mtandao uliotumiwa sana katika Cuba , Bahrain na Tanzania, lakini pia uandikishwaji wa mitandao katika zaidi ya nchi 100 kwenye kila bara.

‘Raia Mtandaoni si tu kiunganishi kizuri cha neno

Kwa mara ya kwanza neno hilo lilianza kutumika katika China ambapo jamii waliokuwa wanatumia mtandao nchini humo walianza wenyewe kujiita wǎngmín (yaani “raia -mtandaoni”) na wǎngyǒu (yaani “rafiki -mtandaoni”).

Zaidi ya neno hilo, jamii za kichina zilitoa nafasi ambapo watu waliweza kuzungumza, kukosoa na kujadili katika namna ambavyo haikuwa rahisi kwa jamii hizo. Raia mtandaoni walijitambua kabisa kama raia waliohai mtandaoni tofauti na wanavyoishi katika maisha halisi ya kila siku.

Katika nchi kama Ethiopia, Morocco na Syria timu yetu imefuatilia kesi na mihula ya vifungo vya mabloga na watumiaji wa mitandao ambao kazi zao zilileta mabadiliko katika jamii zao na kuongeza msukumo wa vitisho vya kisheria kutoka katika serikali zao wenyewe.

Hatuandiki kuhusu kanuni au nadharia ya haki za kidijitali— tunaandika namna zinavyosaidia watu halisi. Kila baada ya wiki, timu yetu ya kujitolea ilifanya kazi kuonesha namna utoaji maoni mtandaoni ulivyokuwa na nguvu ya ajabu katika maisha ya wananchi na namna inavyoweza kuinua jamii na harakati za kisiasa za taifa na asasi nyingine binafsi zenye nguvu.

Kwa muda mwingi ripoti zetu zilifuatilia namna tukio moja kubwa — kama janga la mazingira, migogoro ya wakimbizi, mashambulio mabaya— linavyoweza kuchochea majibizano ambayo yanasababisha vitisho kwa haki za mtandao duniani. Na tumefuatilia matukio makubwa duniani yanayokandamiza sheria ya uhuru wa kutoa maoni ambayo yameathiri watu wengi duniani, lakini mara nyingi hayachukuwi nafasi ya vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari.
Hapa kuna baadhi ya matoleo yetu ya ripoti ya raia mtandaoni ambayo yanaonesha ukubwa wa kazi yetu tangu 2011.
 

Unapokuwa unafanya kazi kwa maslahi ya umma unaweza kukamatwa: wanaharakati wa mtandao matatani

Haki za mtu anayesema ukweli kwa serikali ndiyo kiini cha kazi ya utetezi wa Global Voices. Kila baada ya wiki, tulihabarisha kuhusu vitisho dhidi ya uhuru wa kuongea kuanzia kukamatwa kwa wanaharakati 10 katika mji wa Istanbul, Ureno, kuteswa kwa mabloga 9 wa kanda katika Ethiopia na kuongezeka kwa mashambulizi ya kuwaua mabloga katika Bangladesh .

Waandamanaji wanaomba adhabu kali kwa watuhumiwa wa vita katika Bangladesh mwaka 2013. Picha na Mehdi Hasan Khan kupitia Wikimedia (CC BY-SA 3.0)

 

Ujumbe wa Charlie una matokeo ya kufadhaisha: Udhibiti kupitia kile kinachoitwa usalama wa taifa

Kuvamiwa kwa Charlie Hebdo katika mji wa Paris ulisababisha majadiliano makali juu ya umuhimu wa uhuru wa kutoa maoni , na ulipelekea serikali kadhaa katika umoja wa nchi za ulaya na kwingineko kuzuia uhuru wa kuongea na kuongeza vyombo vyao vya uangalizi . Hii ni moja ya mifano mingi ambapo serikali zilitumia vitisho vikali sana kama kuthibitisha kuzuia uhuru wa kuongea na haki nyingine za msingi– dhamira ya kudumu ya ripoti ya raia mtandaoni.

“Mimi ni Charlie… na mimi ni muislam.”

 

Katika ‘hali ya hatari’, mitandao inafungwa inawaacha wananchi wakihangaika kuunganisha

Mageuzi ya kisiasa na maandamano ya umma katika nchi nyingi yameongeza“hali ya hatari”, na kusababisha kuwekwa kando kwa haki za msingi na kuendelea kufungwa kwa mitandao. Toleo hili linazungumziaEthiopia na Venezuela, nchi mbili tu kati ya nchi nyingi ambapo kufungiwa kwa mitandao kulitokea. Pia tumezungumzia kufungwa kwa mitandao ya kijamii katika China, Syria, Pakistan, Cameroon, Iran, Togo, India, Iraq, Misri, Gabon, D. R. Congo, Somalia, na Sudan.

mwanafunzi mwandamanaji akiwambia walinzi wa Venezuela wakati wa maandamano mwaka 2014. Picha na Jamez 42 kupitia Wikimedia Commons (CC0)

 

Hatuwezi kuficha, lakini tunapeleza: Timu ya udukuaji yavuja

Kuvuja kwa hali ya juu kwa taarifa nyingi za ndani za timu ya kusimamia programu ya kudukua habari mtandaoni Italia zilithibitisha serikali zilikuwa zinawapeleleza waandishi wa habari, watetezi wa haki za bianadamu na vikundi vya upinzani kisiasa– hii ilithibitisha miaka ya mashaka na ushahidi wa programu hasidi ikilenga tulichoandika katika ripoti ya raia mtandaoni. Jumuia yetu iliandika matokeo ya matukio haya Bahrain, Ecuador, Misri, Lebanon, Mexico na Sebia.

Katuni na Doaa Eladl kupitia Flickr, mtandao tunaoutaka ( CC BY-SA 2.0)

 

Wanaharakati wanataka majibu kupitia Facebook

Kama jumuia ya waandishi na wanaharakati, tumekumbana na ukandamizaji, kunyanyaswa na vitisho hadharani kwa sababu ya uhusika wetu kupitia Facebook tangu siku za mwanzoni katika jukwaa hilo. Katika nyaraka za ripoti ya raia mtandaoni zinaonesha mifano mingi mno ya ubaguzi na unyanyasaji kwenye jukwaa hilo ambayo inaonesha utafiti wetu wa kina katika misingi ya uhuru (Mradi wa Facebook wa kutengeneza “taa mtandaoni” kwa watu wa nchi zinazoendelea), na imeandikwa vurugu kutoka kwa wanaharakati wakidai majibu kwenye jukwaa kufuatia kudhihirishwa kwa matukio ya Cambridge Analytica.

Mwandamanaji karibu na kituo cha walimu tarajali cha Chuo Kikuu cha Dhaka (TSC). Bango linasomeka “Udhuru kiasi gani zaidi? Fungua Viber, Messenger, WhatsApp na Facebook sasa.” Picha na Zaid Islam, imetumiwa kwa ruhusa.

Pamoja na timu ambayo iliyokuwa ikikuwa wakati wote ya waandishi, watafiti, wanaharakati na wataalamu wa haki za binadamu kutoka nchi 14(Orodha yao nzima ipo hapa chini) na wakiungwa mkono na wahariri wa Global Voices, tumezalisha toleo la 300 ya ripoti ya raia mtandaoni tangu mwaka 2011.
Wiki hii kwenye mtandao wa Twitter, ungana nasi ili kuinua kioo cha ukweli wa nguvu yetu ya pamoja. Kuna miaka mingi zaidi ya kunasa habari za haki za binadamu na mtandao duniani!

Wenu,

Timu ya ripoti ya mtandao
 

Abir Ghattas, Afef Abrougui, Alex Laverty, Alexey Kovalev, Amira Al Hussaini, Angel Carrión, Arzu Geybullayeva, Asteris Masouras, Bojan Perkov, Corey Abramson, Diego Casaes, Dragan Kucirov, Elaine Díaz, Elizabeth Rivera, Ellery Roberts Biddle, Endalk Chala, Filip Stojanovski, Firuzeh Shokooh Valle, Georgia Popplewell, Hae-in Lim, Hisham Almiraat, Inji Pennu, Ivan Sigal, J. Tadeo, James Losey, Janine Mendes-Franco, Jessica Dheere, Jillian York, Joey Ayoub, Juan Arellano, Juke Carolina, Karolle Rabarison, Kevin Rothrock, Kofi Yeboah, L. Finch, Laura Vidal, Leila Nachawati, Lisa Ferguson, Lova Rakotomalala, Don Le, Marietta Le, Mahsa Alimardani, Marianne Díaz, Mohamad Najem, Mohamed ElGohary, Mong Palatino, Nevin Thompson, Nwachukwu Egbunike, Oiwan Lam, Pauline Ratze, Rayna St, Rebecca MacKinnon, Renata Avila, Rezwan, Rohith Jyothish, Sadaf Khan, Sahar Habib Ghazi, Salma Essam, Sarah Myers West, Silvia Viñas, Solana Larsen, Suzanna Lehn, Taisa Sganzerla, Talal Raza, Tanya Lokot, Tetyana Bohdanova, Tom Risen, Torie Bosch, Weiping Li na Yuqi Chen wamechangia kwenye taarifa moja au nyingi ya ripoti za raia mtandaoni tangu.

Wachangiaji wa ripoti ya raia mtandaoni baadhi yao wanatokea nchi za Azerbaijan, Bahrain, Bangladesh, Brazil, Bulgaria, China, Misri, Ethiopia,Ufaransa, Ghana, Ugiriki, Guatemala, Hong Kong, Hungary, India, Indonesia, Japan, Iran, Kenya, Lebanon, Macedonia, Madagascar, Mexico, Morocco, Nigeria, Pakistan, Peru, Ufilipino, Puerto Rico, Urusi, Sebia, Korea kusini, Hispania, Uswisi , Siria, Tunisia, Ureno, Ukraini, Marekani, Venezuela na Vietnam.

 

Jiunge na ripoti ya raia mtandaoni

 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.