GV Face: Mazungumzo na Mwanaharakati wa Bahrain Ambaye Bahrain Isingependa Tumsikie

Familia ya Al Khawaja imejikuta ikiwa msitari wa mbele kwenye maandamano ya Bahrain, tangu wakati way ale yaliyoitwa Mapinduzi ya Uarabuni yalipoingia kwenye kisiwa hicho cha Ufalme mnamo Febrari 14, 2011.

Mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu Abdul Hadi Al Khawaja kwa sasa anatumikia kifungo cha maisha jela kwa kuhusika na maandamano hayo.

Wakitumia mitandao ya kijamii, mabinti zake Maryam, mwenye umri wa miaka 27, na Zainab Al Khawaja, mwenye miaka 31, wamepiga kelele kwenye mtandao wa Twita, wakisambaza habari za yale yanayoendelea nchini humo kwa maelfu ya wafuasi wao duniani kote. Maryam akiwa na wafuati elfu 10 na Zainabu akiwa na wafuasi 48.8 kwenye mtandao wa Twita, wamepata vitisho vya serikali kwa kitendo chao cha kusema.

Zainab kwa sasa yuko gerezani kwa kosa la kuchana picha rasmi ya Mfalme wa nchi hiyo akiwa mahakamani. Maryam kwa upande wake, ilimbidi kuondoka nchini humo baada ya kushikiliwa kwenye uwanja wa ndege alipojaribu kumtembelea baba yake. Baada ya Maryam kukamatwa uwanja wa ndege, alituhumiwa kumpiga polisi. Maryam anakana mashitaka hayo. Wakati amekamatwa, alifanya mgomo wa kula. Baadae aliachiliwa huru mnamo Septemba 19 na tangu wakati huo anaishi nje ya nchi. Baba yake yuko jela. Maryam ni Mkurugenzi mwenza wa Kituo cha Ghuba ya Arabuni cha Haki za Binadamu.

Katika toleo hili la GV Face, tunazungumza na Maryam Al Khawaja. 

Bahrain mpaka sasa imeingia mwaka wa tatu wa ghasia zaMapinduzi yaliyojipatia umaarufu. Taarifa za habari za vyombo vikuu vya kimataifa zinasema maandamano nchini Bahrain ni mapinduzi yanayoongozwa na waumini wa dini ya Shia dhidi ya utawala wa Sunni. Wakati wengi wanaweza kuona kwamba hakuna lolote la maana kwa maelezo haya, na ni maelezo mepesi yasiyoeleza kile kinachoendelea hasa nchini humo. Hayakubali ukweli kwamba wa-Bahrain wanaoinuka kinyume na utawala huo hawafanyi hivyo kwa sababu tu wao ni Shia na utawala huo ni Sunni. 

Tunazungumza na Maryam Al Khawaja kuhusu namna imani za kidini zinavyoathiri harakati hizo. Nani ni mwathirika na nani ni mwendelezaji wa hisia za kidini? Namna gani ukandamizaji wa kimfumo wa kidini unavyofanya kazi nchini Bahrain? Na kwa nini Mapinduzi ya Bahrain yanaonekana kuwa ya kidini?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.