Habari kuhusu Bangladesh
Kikundi cha ki-Islam Chadai Kuondolewa kwa Sanamu Mbele ya Mahakama Kuu Nchini Bangladesh
Mamlaka zimepewa chini ya juma moja kufanyia kazi madai ambayo wakuu wa serikali na watumiaji wa wanayaona kama hayana maana
Picha za Kale Zarejesha Kumbukumbu Nzuri za Mji Mkuu wa Dhaka nchini Bangladesh
"Hapo ndipo nilipokulia hadi nilipokuwa kijana na ninajaribu kupata hisia ya namna siku hizo zilivyokuwa nzuri. Hizo zilikuwa siku njema sana kwa jiji langu pendwa la Dacca na siyo Dhaka."
Matangazo ya Sauti ya ‘Wiki Ilivyokwenda’ Global Voices: Waliopotea
Wiki hii, tunakupeleka Ecuador, Uganda, Bangladesh, Ukraine na Pakistan.
TAMKO: Global Voices Yatoa Wito wa Kuimarishwa kwa Usalama wa Wanablogu wa Bangladesh
Tunalaani mauaji ya hivi karibuni ya wanablogu na kuzitaka mamlaka husika kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika kwenye mauaji haya wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Muandaaji wa Katuni ‘Meena’ Abadilisha Mitizamo ya Watu wa Asia ya Kusini Kuhusu Wasichana
"Since her inception 14 years ago she has shown millions of women and girls what can be achieved."
Bajeti ya Bangladesh: Maoni na Uchambuzi
“Bajeti ya kifahari lakini mpango duni?” Raia wa kawaida anatoa maoni na kuichambua bajeti ya hivi karibuni ya Bangladesh kwa mwaka wa fedha 2013-2014.
Mwanamke Aokolewa Kwenye Kifusi Baada ya Siku 17
Siku ifananayo na ile iliyogharimu maisha ya watu mara baada ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa tisa huko Savar pembezoni mwa mji mkuu wa Banglasesh, Dhaka, idadi ya watu waliofariki imeongezeka hadi 1,055 , idadi inayopelekea tukio hili kuwa tukio lililowahi kuua watu wengi zaidi tokea lile la tarehe 9/11 kulipotokea mashambulizi ya kigaidi, mfanyakazi mwanamke ajulikanaye kwa jina la Reshma Begum amekutwa akiwa hai mara baada ya kuzuiwa na kifusi cha jengo hilo kwa siku 17.
Bangladesh: Waislamu Wadai Wanawake Wabaki Majumbani
Wanachama wa kikundi chenye msimamo mkali cha Kiislamu nchini kimewashambulia wanahabari wa kike waliokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kiuandishi wakati kikundi hicho kilipokuwa kikifanya maandamano katika jiji la Dakar kudai kutumika kwa sheria kali za kiislamu, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku wanawake kuchanganyika na wanaume. Mpaka madai yao yatakapotekelezwa, chama hicho kimejiapiza kulitenga jiji la Dhaka na sehemu nyingine za nchi hiyo ifikapo Mei 5, 2013 kwa kuwaweka wanaharakati wake katika maeneo sita ya kuingilia jiji hilo.
Bangladesh: Jengo Laporomoka, Mamia Wauawa kwenye Vifusi
Janga jingine tena la kiwanda nchini Bangladesh, safari hii jengo la ghorofa tisa lilianguka na kuua zaidi ya watu 142 na watu wengine karibu elfu moja kujeruhiwa. Watu wengine wengi bado wamenaswa kwenye kifusi na harakati za kuwaokoa bado zinaendelea. tukio hili linatokana na uzembe wa baadhi ya watu kwani utawala wa kiwanda hiki uliwashinikiza watu kuendelea kufanya kazi katika jengo ambalo halikuwa salama.
Serikali ya Bangladeshi Yawafuatilia Wanablogu, Yawatuhumu Kuukashfu Uislam.
Kadri mapambano makali kati ya wanaharakati wa Kiislamu na serikali yanavyoendelea kusababisha migongano ya kidini nchini Bangladesh, Mamlaka ya Mawasiliano ya nchi hiyo imechukua hatua ya kuwanyamazisha wanablogu wanaoonekana wapinzani wa Uislamu na serikali. Asif mshindi wa tuzo ya mwanablogu bora amekuwa akilengwa na hatua hizo kwa siku za hivi karibuni.