Picha za Kale Zarejesha Kumbukumbu Nzuri za Mji Mkuu wa Dhaka nchini Bangladesh

Topkhana Road, Press Club Area, Dhaka (1965). Photographer- Roger Gwynn. Photo courtesy: Bangladesh Old Photo Archive.

Barabara ya Topkhana, Eneo la Press Club, Dhaka (1965). Picha na Roger Gwynn. Idhini ya picha: Hifadhi ya Picha za Kale ya Bangladesh.

Ni hali ya kustaajabisha kwa kiasi ambacho sehemu fulani inaweza kubadilika kwa miaka 50. kwa mfano, Dhaka, mji mkuu wa Bangladesh, ni moja ya majiji maarufu kabisa duniani lakini huwezi kuamini kwa namna unavyoonekana kwenye picha zilizopigwa miaka mingi iliyopita.

Kwenye miak ya 1960, mpiga picha wa Kiingereza Roger Gwynn alifika Bangladesh kama mtu wa kujitolea na kufanya kazi na shirika lisilo la kiserikali la  Service Civil International. Aliweza kutembelea maeneo mbalimbali ya Bangladesh, ambayo kwa wakati huo ilijulikana kama Pakistani ya Mashariki na kuweza kupiga picha mbalimbali. Hivi karibuni, picha zake zilichapishwa kwenye ukurasa wa Facebook ulijulikan kama  Hifadhi ya Picha za Zamani ya Bangladesh na kisha kusambaa sana miongoni mwa watumiaji wa matandao nchini Bangladesh.

Ukurasa huu uliofunguliwa mnamo Agosti 24, 2011, una wafuatiliaji zaidi ya 171, 000. Kwa miaka kadhaa, jumuia hii imeshachapisha picha nyingi za eneo ambalo kwa sasa ndio Bangladesh — tangu kipindi cha ukoloni wa mwingereza hadi miaka ya 1990. Pindi unapoangalia hifadhi ya picha hizi, unapata kidokezo cha historia, tamaduni na maisha ya raia wa Bangladesh kwa kipindi cha karne moja iliyopita.

Picha za Roger Gwynn ziliwafanya watu wengi wahisi kuwa kuna kitu wanachokikosa. Walivuta kumbukumbu za zamani kuhusu mambo mazuri ya wakati huo na baadhi yao kuonesha nia ya kutaka kurudia nyakati hizo.

Victoria Park area. Sadarghat, Dhaka (1967). Photographer- Roger Gwynn. Photo courtesy- Bangladesh Old Photo Archive.

Eneo la Victoria Park. Sadarghat, Dhaka (1967).Picha na Roger Gwynn. Idhini ya picha: Hifadhi ya Picha za Kale ya Bangladesh.

Salim Omer Sher alivuta  kumbukumbu ya eneo la Victoria Park kwenye miaka ya 1960:

Inanikubmusha mbali sana. Nilikuwa mwanafunzi kwenye shule kongwe ya Dhaka na nilikuwa nikitembelea eneo hili kwenye miaka ya 60. Mwaka 1960 nilikuwa na umri wa miaka 17 wakati ambao picha hii ilipigwa. Kumbukumbu halisi ya eneo la Victoria Park.

Handcart porters at New Market area. Dhaka (1965). Photographer- Roger Gwynn. Photo courtesy- Bangladesh Old Photo Archive.

Wabeba mizigo wanaotumia mikokoteni ya mkono wakiwa katika eneo la soko Jipya. Dhaka (1965). Picha na Roger Gwynn. Idhini ya picha: Hifadhi ya Picha za Kale ya Bangladesh.

Mtaalamu wa masuala ya mawasiliano Wazir Satter alikumbuka nyakati za chakula cha bei rahisi mara baada ya kuona picha ya mtaa wa eneo la soko Jipya:

Moja ya mgahawa ulikuwa ukiuza malai cha (chai maalum ya viungo). Wanafunzi kutoka chuo cha Dacca tulikuwa na utarayibu wa kufika kwenye mgahawa huu kwenye miaka ya 1967-69 kwa ajili ya chai hiyo pamoja na makate maalum wa Kiasia wa nyama (gosht-porota). Jin la mgahawa huo lilikuwa ni Chittagong. Kikombe kimoja cha chai ya vioungo maalum ilikuwa ni poisha 25 za Bangladesh (4 anas).

Street scene of Mirpur Road, New Market. Dhaka (1965). Photographer- Roger Gwynn. Photo courtesy- Bangladesh Old Photo Archive.

Muonekano wa Barabara ya mtaa wa Mirpur, Soko Jipya. Dhaka (1965). Picha na Roger Gwynn. Idhini ya picha: Hifadhi ya Picha za Kale ya Bangladesh.

Moja ya picha iliibua kumbukumbu za utotoni za Babor Huq:

Nilikuwa nikitembea na baba yangu huku nikiwa nimemshika mkono alipokuwa akienda kuchukua nguo zake huko Lifa na nilikuwa na Kalojam (aina ya pipi) kutoka Moron Chand, kipindi hicho nikiwa mdogo sana. Hata ninazikumbuka nyakazi hizi kwa kiasi chake. Ninamkumbuka sana baba yangu na kila wakati ninamuombea.

Demra Road by Hardeo glass factory, Dhaka (1965). Photographer- Roger Gwynn. Photo courtesy- Bangladesh Old Photo Archive.

Barabara ya Demra na kiwanda cha glasi cha Hardeo, Dhaka (1965). Picha na Roger Gwynn. Idhini ya picha: Hifadhi ya Picha za Kale ya Bangladesh.

Ranajay Gupta pale alipoona kiwanda cha glasi cha Hardeo:

Interesting. Kiwanda cha glasi cha Hardeo kwa mara ya kwanza kabisa kilikuwa kinamilikiwa na familia yangu huko Tikatuli. Ninaamini kulikuwa na kaburi la kumbukumbu (‘samadhimandir’) kwa ajili ya nyanya wangu (memorial shrine) for my great-grandparents Sarat Chandra Gupta (ambaye barabara ya Sarat Gupta ilipewa jina lake) na Manorama Gupta kwenye kona ya eneo hilo. Ninaambiwa kuwa baadae lilikuja kuka kubwa la Rajdhani; kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa samadhimandir bado ipo kwenye kona ya soko.

Children are enjoying Bioscope show. Old Dhaka, Bangladesh (1960s). Photographer- Roger Gwynn. Photo courtesy- Bangladesh Old Photo Archive.

Watoto wakifurahia onesho la sinema. Dhaka ya Kale, Bangladesh (1960). Picha na Roger Gwynn. Idhini ya picha: Hifadhi ya Picha za Kale ya Bangladesh.

Nyakati hizo, sinema , aina ya tamthilia zinazojongea, ilikuwa ni burudani maarufu. Syed Harun Rashid aliandika:

Wakati usiosahaulika wa miaka mingi iliyopita! … Ningeliweza sana kujifananisha na vijana hawa. Kutazama na fikra za kuweza kufurahia, ni miujiza, hii iliitwa sinema. Ninawaza kuhusu hali ya hisia kali ya furaha isiyo na kifani ya kitu hiki kilichosahauliwa ambacho hakitakaa kiondoke kwenye kumbukumbu zetu…..

Jiji la Dhaka linafahamika kwa kuwa na msongamano mkubwa wa magari. Lakini mika ya 1960 ulikuwa ni mji uliokuwa umepangika vizuri. Rumi Aftab aliandika:

Kipindi hicho kilikuwa kizuri sana. Kwa sasa jiji limesongamana na pia kuwepo na msongamano mkubwa wa magari unaleta hali ya kukosa utulivu, hali hii pia inatupoteza muda!

Street scene of Dhanmondi Road No 2. Dhaka (1965) Photographer- Roger Gwynn

Mwonekano wa mtaa wa Dhanmondi Road No 2. Dhaka (1965). Picha na Roger Gwynn. Idhini ya picha: Hifadhi ya Picha za Kale ya Bangladesh.

Mwonekano wa jiji umebadilika sana kiasi kwamba ni vigumu sana kufananisha mwonekano wa picha za Gwynn na Dhaka ya sasa. Mtumiaji wa Facebook Swargiyo Jiban aliandika:

Ni vigumu kuamini laini kulikuwemo na sehemu kubwa ya mwonekano wa mtu. Nilikulia kwenye maeneo ya rayer Bazar na mohammadpur. Maeneo ya Saw rayer Bazar hadi Mohammadpur yalizungukwa na mto mrefu uliojulikana kwa jina la burigongha. Kulikuwa na kijiji tulichozoea kukiita bochila, na ilikuwa raha sana kwenda huko kwa kutumia boti. Ni kumbukumbu ambayo ingekuwa vigumu sana kuikumbuka tangu miaka ya 1982-86, ambapo niliondoka eneo hilo mwaka 1987 na baada ya miaka 15 kupita nilitembelea tena maeneo hayo na hali ilikuwa ya kushangaza sana.. mabadiliko ya miaka 15 yalikuwa makubwa sana, minara ilibadilishwa na kuchukua maumbo mengine kabisa, hata sikuamini, kulikuwa na mto tuliokuwa tukicheza, kuogelea.. hata kutokea hazaribugh hadi kamrangir chor iliwezekana kwenda kwa gari.. siamini…

Syed Rahman haupendi mwonekano wa sasa wa jiji la Dhaka:

Hapo ndipo nilipokulia hadi nilipokuwa kijana na ninajaribu kupata hisia ya namna siku hizo zilivyokuwa nzuri. Hizo zilikuwa siku njema sana kwa jiji langu pendwa la Dacca na siyo Dhaka.

Picha zaidi za Dhaka:

Water carrier, Wari, Dhaka (1965). Photographer- Roger Gwynn. Photo courtesy- Bangladesh Old Photo Archive.

Mbeba maji, Wari, Dhaka (1965). Picha na Roger Gwynn. Idhini ya picha: Hifadhi ya Picha za Kale ya Bangladesh.

Morning street market - fresh fish on sale. Dhaka (1960s). Photographer- Roger Gwynn. Photo courtesy- Bangladesh Old Photo Archive.

Morning street market – Samaki wabichi wakiwa wanauzwa. Dhaka (1960s). Picha na Roger Gwynn. Idhini ya picha: Hifadhi ya Picha za Kale ya Bangladesh.

A guy reading newspaper in a tea stall. Dhaka, Bangladesh (1965). Photographer- Roger Gwynn. Photo courtesy- Bangladesh Old Photo Archive.

Mtu akisoma gazeti kwanye kibanda cha kuuzia chai. Dhaka, Bangladesh (1965).
Picha na Roger Gwynn. Idhini ya picha: Hifadhi ya Picha za Kale ya Bangladesh.

Girls studying the Quran in a maktab. Dhaka (1960s). Photographer- Roger Gwynn. Photo courtesy- Bangladesh Old Photo Archive.

Wasichana wakijifunza Kuran kwenye maktaba. Dhaka (1960s). Picha na Roger Gwynn. Idhini ya picha: Hifadhi ya Picha za Kale ya Bangladesh.

Unaweza kupitia kitabu chote cha picha hapa .

Picha zimetumiwa kwa ruhusa ya Roger Gwynn.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.