Mwanamke Aokolewa Kwenye Kifusi Baada ya Siku 17

Siku ifananayo na ile iliyogharimu maisha ya watu mara baada ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa tisa huko Savar pembezoni mwa mji mkuu wa Banglasesh, Dhaka idadi ya vifo imeongezeka hadi 1,055, hadi sasa hili ndilo jingo lililowahi kuporomoka na kuua idadi kubwa zaidi ya watu tangu lilipotokea shambulizi la kigaidi mnamo tarehe 9/11, mfanyakazi mmoja mwanamke ajulikanaye kwa jina la Reshma Begum amekutwa akiwa hai baada ya kuzuiwa na vifusi vya jengo hilo kwa siku 17.

Begum alikuwa akifanya kazi ya ushonaji katika ghorofa ya pili ya jengo hilo. Jingo lilipoporomoka, mwanamke huyo wa miaka 24 alizuiwa ndani ya msikiti uliokuwa sakafu ya ardhi na aliweza kustahimili kwa masaa 416 kwenye vifusi kwa kupumua kupitia kwenye bomba pamoja na kutafuta biskuti kwenyee vibegi vido vya mgongoni vya wenzake waliokuwa wameshapoteza maisha.

Katika siku chache za kwanza mara baada ya jingo hilo kuporomoka mnamo Aprili 24, 2013, watu 2,428 wameshaokolewa kutoka katika vifusi vya jengo hilo. Tumaini la kuwapata watu wengine wakiwa hai katika vifusi vya jengo hilo linazidi kufifia.

Bangladeshi rescuers retrieve garment worker Reshma from the rubble of a collapsed building in Savar after seventeen days. Image by Rehman Asad. opyright Demotix (10/5/2013)

Waokoaji wa Bangladeshi wakimuokoa mfanyakazi wa kiwanda cha kutengenezea nguo ajulikaye kwa jina la Reshma kutoka kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka baada ya kufunikwa kwa vifusi vya jengo hilo kwa siku 17. picha na Rehman Asad. Copyright Demotix (10/5/2013).

Begum aliwaambia mawakala wa habari :

আমি ১৭ দিন পানি খেয়ে বেঁচেছিলাম। ভবন ধসের পরপরই আমি ভবনের নিচে আটকা পড়ি। পরে বাঁচার জন্য ভবনে অবস্থিত নামাজ ঘরে চলে যাই। উদ্ধারকারীরা ওপর থেকে নানা সময়ে বোতলজাত পানি পাঠান। আমি সেখান থেকে দুই বোতল পানি সংরক্ষণ করে রাখি। সেই বোতলের পানি আমি প্রতিদিন অল্প অল্প খেয়ে জীবন বাঁচাই।

kwa kiasi kikubwa niliweza kuishi kwa kunywa maji. Nilibanwa mara tu baada ya jengo kuporomoka. Haraka nilielekea kwenye chumba kwa ajili ya maombi kama mkimbizi. Waokoaji walikuwa wakitupa chupa za maji ndani ya chumba hicho mara kwa mara. Niliweza kupata chupa mbili za maji ambazo ndizo zilizonifanya nikawa hai kwa siku zote hizi.

Kuepuka kifo huku kwa miujiza kwa Begum kuliibua hisia kali miongoni mwa wtu wengi. Baada ya kusikia habari hizi nzuri, mwanablogu Ashraf Shishir (@ashrafshishir) aliandika:

@ashrafshishir: অনেকদিন পর বাচ্চা ছেলের মতো কাঁদলাম। এইমাত্র রেশমী অথবা রেশমাকে জীবন্ত উদ্ধার করা সম্ভব হয়েছে!…

@ashrafshishir (Ashraf Shishir): Nililia kama mtoto kwa muda mrefu. Reshmi au Reshma ni hivi punde tu ameokolewa akiwa hai!..

Muundaji wa nguo, Shahana Siddiqui (@shahanasiddiqui) alijitahidi kutoililia furaha. Alitwiti:

@shahanasiddiqui: Niliacha kutoa machozi yangu mara baada ya kusikia kuokoka kimiujiza kwa Reshma! Ni wakati wa furaha, ni muda wa kujisikia fahari.

Army and rescuers look through the pocket point in the rubble of Rana Plaza where they found Reshma located alive under the rubble after 17 days of the worst-ever building collapse tragedy. Image by Firoz Ahmed. Copyright Demotix (10/5/2013)

Wanajeshi na waokoaji wakiangalia sehemu Rishma alipokuwa amezuiwa na kifusi cha jengo la Rana Plaza, mahali walipompata akiwa hai. Picha na Firoz Ahmed. Copyright Demotix (10/5/2013)

Baroness Sayeeda Hussain Warsi (@SayeedaWarsi), waziri mwandamizi wa Uingerezera anayehusika na mambo ya nje na ushirikiano wa makoloni ya Uingereza alitoa maoni yake mara baada ya kusikia habari za kuokolewa kwa Reshma:

@SayeedaWarsi: ni zaidi ya ajabu; tukiio la kutia moyo kwa mwanamke mdogo kuokolewa baada ya siku 17 kupita tokea jengo la Savar kuporomoka. Mwale wa matumaini katikati ya janga.

Asif Touhid, mtaalamu wa mauzo, aliandika katika Facebook:

Reshma … dada mpendwa,Dear sister, ushupavu wako wa kuishi kwenye vifusi kwa siku zote hizo kumenipa hamasa na kurejesha imani kwa watu wangu. blockquote>
Mwandishi wa habari Kamrul Hasan (@_Kamrul_Hasan_) aliwashukuru waokoji wote kwa juhudi zao walizozionesha kwa kumuokoa Begum akiwa hai:

@Kamrul_Hasan: এভাবেও ফিরে আসা যায়! অভিনন্দন বেশমা, আপনি বেঁচে থাকুন। অনেক অনেক ধন্যবাদ বাংলাদেশ সেনাবাহিনীসহ সকল উদ্ধারকারীদের।

@Kamrul_Hasan: kumbe hili linawezekana! Hongera sana reshma, uishi maisha marefu na mazuri. Shukrani za pekee kwa jopo la waokoaji wa kijeshi kwa juhudi walizoweka.

Jukumu la vyombo vya habari lilihojiwa pale walipohamia kwa Begum na kujaribu kumhoji. Mwandishi wa habari Tanvir Ahmed aliwahoji waandishi wenzake katika ukurasa wa Facebook:

আপাতত উদ্ধারকর্মী আর চিকিৎসকদের সাক্ষাতকার নিয়ে তৃপ্ত থাকুন। এতদিন রেশমা কি খেয়ে বেঁচে ছিলো, তার জামা কাপড় এতো পরিস্কার কেন? এসকল প্রশ্নের চেয়ে মেয়েটির এখন শুধুই প্রয়োজন চিকিৎসা সেবা।

Tafadhali mridhike na mahojiano na waokoaji pamoja na jopo la madaktari. Msijisumbue kuuliza jinsi alivyoweza kuishi kwenye vifusi kwa siku zote hizo. Kwa nini nguo zake hazikutatuka? Badala ya kujibu maswali yote haya, anahitaji huduma ya haraka ya matibabu. blockquote>

Relatives of missing or dead garment workers optimistic 17 days after the incident. Image by Shafiur Rahman. Copyright Demotix (10/5/2013)

Ndugu wa waliokuwa fanyakazi katika kiwanda cha nguo waliopotea au kufariki wameendelea kuwa na matumaini ya kuwapata ndugu zao siku 17 baada ya tukio hili. Picha na Shafiur Rahman. Copyright Demotix (10/5/2013)

Biashara ya nguo zilizokuwa tayari ndio chanzo kikubwa kabisa cha pato la nje kwa nchi ya Bangladesh, kwa hiyo, kwa mtazamo wa wengi, kuanguka kwa jengo hilo kunachorwa kuwa ni taswira hasi ya nchi ya Bangladesh. Kwa kulizingatia hili, Abu Maksud alimchukulia Begum kama taswira ya Bangladesh katika makala aliyoiweka katika ukurasa wa Facebook:

১৭ দিন ধরে ধ্বংসস্তুপে বেঁচে ছিল বাংলাদেশ। রেশমা- বোন আমার অন্ধকূপ থেকে তুমি ফিরে এসেছ, তুমি দেখিয়েছ বাংলাদেশ বেঁচে থাকে, ধ্বংসস্তুপেও বাংলাদেশ বেঁচে থাকে।

Bangladesh iliweza kuishi kwenye kifusi kwa siku 17. Dada Rishma- umenusurika na kifo. Umeonesha kuwa hata Bangladesh inaweza kuishi kwenye vifusi.

Zafar Sobhan, mhariri wa Jukwaa la Dhaka, alitoa mjumuisho katika mahojiano na mtandao wa habari wa News.com.au:

Reshma anawakilisha ubora wa Bangladesh, ustawi wa nchi ya Bangladesh unaambatana na magumu yasiyoelezeka, utiaji moyo wake, uimara wake, uthabiti wake wa kutokukata tamaa pamoja na changamoto nyingi. blockquote>

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.