Machapisho Katika Kurasa za Facebook Zachochea Ongezeko la Watu Kukamatwa Huko Bangladesh, Wavuti Waingiwa na Wasiwasi

Poet Henry Swaopon and Lawyer Imtiaz Mahmood.

Mshairi Henry Swapon na Mwanasheria Imtiaz Mahmood. Muunganiko huu ni wa picha zao zilizosambaa sana katika mitandao ya kijamii.

Watu wawili walikamatwa hapo Mei 14 na 15 kwa kuweka maoni yao katika kurasa zao za Facebook. Ukamataji huo umeleta maswali miongoni mwa jamii katika mitandao ya jamii.

Ukamataji wa Mshairi Henry Swapon

Mei 14, Mshairi na Mwanahabari Henry Swapon alikamatwa akiwa nyumbani kwake katika mji wa Barishal, ulio Kanda ya Kati Kusini mwa Bangladesh. Amekuwa akituhumiwa kwa kukiuka sheria ya Usalama wa Mitandaoni ya Bangladesh

Akiwa ni mshirika katika jumuiya ndogo ya Kikristo, hapo mwanzo Swapon alishawahi kushtakiwa yeye na kaka zake Alfred na Jewel Satkat kwa “kuumiza hisia za  kiimani za Waislam na Wakristo” katika mitandao ya jamii.

Kulingana na Dhaka Tribune, Swapon aliweka bandiko katika ukurasa wake wa Facebook akimkosoa Lawrence Subrata Howlader, ambaye ni Askofu Kanisa Katoliki katika Dayosisi ya Barishal. Askofu alichagua kufanya tukio la kiutamaduni katika moja ya makanisa ya Kikatoliki tarehe 22 Aprili 2019, ikiwa ni siku moja tu baada  shambulio la Kigaidi huko Sri Lanka. Swapon alidhani kuwa Askofu angeahirisha tamasha hilo kwa kuheshimu maisha ya mamia ya watu yaliyopotea katika shambulio hilo.

Wakristo wengine walikasirikia lugha aliyoitumia kwa Askofu na wengine walimtumia hata vitisho vya kumuua. Swapon amekuwa mzungumzaji sana mitandaoni akikemea kila aina ya uonevu na rushwa katika mji wao.

Mwanamtandao Swakrito Noman waliandika huko Facebook:

বাংলাদেশে ধর্মানুভূতিতে আঘাতের ব্যবসাটা একচেটিয়া মুসলমান মৌলবাদীদের ছিল। এখন দেখছি খ্রিষ্টান মৌলবাদীরাও এই ব্যবসা শুরু করে দিয়েছে। আমার তো মনে হয় এই অনুভূতি ব্যবসায়ীরা একেকজন মানসিক রোগী। রাষ্ট্রের উচিত তার অসুস্থ নাগরিকদের সুচিকিৎসার ব্যবস্থা করা। কবি হেনরি স্বপনকে গ্রেপ্তারের তীব্র নিন্দা জানাই। তাঁর নিঃশর্ত মুক্তি চাই।

Ndani ya Bangladesh, mkakati wa kushambulia wanaharakati kwa kuwatuhumu “kuumiza hisia za kiimani” umekuwa ni wa kawaida kwa viongozi wa Kiislamu. Sasa tunaona hata wale wa  Wakristo wasiobadilika nao wameanza kutumia mbinu hii. Nafikiria ambao wanachukia namna hii ya ukosoaji ni wagonjwa wa akili. Serikali iandae utaratibu wa kuwapa matibabu wagonjwa hawa. Tunakemea kwa nguvu zote ukamatwaji wa Mshairi Henry Swapon na tunataka aachiliwe haraka bila masharti yoyote.

Kukamatwa kwa Mwanasheria Imtiaz Mahmood

Asubuhi ya tarehe 15 Mei, polisi walimkamata Mwanasheria wa mahakama kuu  na mwandishi  Imtiaz Mahmud chini ya kifungu cha  sheria ya 2017 ambayo haitumika kwa sasa, sheria ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ambapo, raia mmoja, Shafiqul Islam, alilalamika kuwa mija ya machapisho ya Mahmood huko Facebook yameumiza hisia zake za kiimani na yalichochea uhalifu katika ukanda wa Kusini Mashariki mwa mkoa Chittagong, Bangladesh .

Imtiaz Mahmood alipata alipata dhamana kwa muda kesi ilipoletwa kwa mara ya kwanza lakini mahakama ya Khagrachhari ilitoa amri ya kukamatwa tena kinyume na ile ya Januari 2019.

Mahmood  alichangia maoni yake wakati wa  machafuko ya kikabila yaliyotokea baada ya mwendesha pikipiki wa  Bengali kuuwawa huko Khagrachhari, yakisababisha kikundi cha wa-Bengali kutia moto nyumba kadhaa na maduka ya wakazi wa eneo la Rangamati ndani ya Chittagong. Vyanzo vya huko viliiambia Dhaka Tribune kuwa polisi hawakuchukua hatua zozote kuzuia jambo hilo.

Mamia ya mashtaka ya aina hiyo yalifunguliwa  kuanzia mwaka  2013 mpaka 2018, wakati sheria ya Habari na Mawasiliano ilipobadilisha na sheria ya Usalama wa Mitandao.

Mwandishi Meher Afroz Shao aliandika  huko Facebook:

তিনি পাহাড় ভালোবাসেন- পাহাড়ের মানুষগুলোকে ভালেবাসেন। ফেসবুকে তাদের নিয়ে লেখেন। তার ফেসবুক লেখায় কখনও ‘জালাও পোড়াও’ তো দেখিনি!

কোথাও কোনো একটা ভুল হচ্ছে..! বেশ বড় একটা ভুল… ভুলগুলোর অবসান হোক।

বি.দ্র: আচ্ছা- ফেসবুকে অশালীন গালাগালি করে যারা পোস্ট করে তাদের নামে মামলা হলেই কি এ্যারেস্ট ওয়ারেন্ট বের হয়!

Anaipenda milima na watu ambao wanaishi pale. Huandika kuhusu haki zao. Sijawahi kuona “maneno ya uchochezi” katika uandishi wake.

Kuna jambo haliko sawa…Kuna makosa makubwa sana. Ninaamini  makosa yatarekebishwa haraka.

PS: Nimeshaona machapisho mengi sana huko Facebook ambayo yana lugha chafu na ubaguzi ndani yake. Ikiwa watu hao wakishtakiwa leo, je hati ya kuwakamata itatolewa papo hapo?

Wananchi wa Mitandaoni wengi wamekemea ukamatwaji huo wa wawili hao, wakitaka sheria ifutiliwe mbali.

Mhamiaji wa Bangladeshi Leesa Gazi alitwit:

Mwandishi wa Habari  Probhash Amin aliandika huko Facebook:

কবি হেনরী স্বপনের পর অ্যাডভোকেট ইমতিয়াজ মাহমুদ। একে একে রুদ্ধ হচ্ছে মুক্তমত। সকল কালাকানুন বাতিল চাই। মতপ্রকাশের স্বাধীনতা চাই। কবি হেনরী স্বপন ও আইনজীবী ইমতিয়াজ মাহমুদের মুক্তি চাই।

Baada ya Mshairi Henry Swapon, mwanasheria Imtiaz Mahmood (walikamatwa). Uhuru wa kujieleza umezuiwa. Ninataka sheria zote za kikatili zifutwe. Ninataka uhuru wa kujieleza. Ninataka Henry Swapon na Imtiaz Mahmood waachiliwe mara moja.

Pamoja na kuonesha kuwa sheria hiyo ingebana uhuru wa kujieleza, bunge la Bangladeshi  iliipitisha sheria ya Usalama wa Mitandaoni hapo Septemba 2018. Sheria hii ilichukua nafasi ya sheria nyingine kandamizi ya Habari na Teknolijia, ambayo pia ilikuwa ilitumika kama chombo cha  kuwanyamazisha wakosoaji Mitandaoni.

Sheria hii inahukumu baadhi ya mazungumzo mitandaoni kuanzia jumbe za kubeza mpaka  mazungumzo “yenye kuumiza hisia na maadili ya  kidini” ikiorodhesha pia faini kubwa. Pia inaruhusu vifungo vya muda mrefu kwa makosa ya  kutumia mitandao kusababisha vurugu katika jamii na kwa “kukusanya, kutuma na kuhifadhi” habari na nyaraka nyeti za serikali kupitia huduma za kidigitali. Baraza la Wahariri la Bangladeshi lilisema kuwa sheria hii ni “kinyume na uhuru uliotolewa kikatiba, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza.”

Sheria inatoa  mamlaka kubwa sana  kwa taasisi za kusimamia sheria kuanzisha upelelezi kwa yeyote ambaye shughuli zake zinahisiwa kuwa zina madhara na ni tishio kwa usalama.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.