Bangladeshi Yasherehekea Kurushwa Angani Kwa Setilaiti Yao Kwa Mara ya Kwanza

Mpango wa Setilaiti ya Bangabandhu-1 huko Cape Canaveral, Marekani. Picha kutoka Flickr kupitia picha rasmi za SpaceX. Public domain.

Saa 10:14. Mchana Saa za Mashariki (EDT) Mei 11, 2018, Bangabandhu-1, satelaiti ya kwanza ya mawasiliano nchini Bangladeshi ilirushwa angani kutokea Cape Canaveral, Florida nchini Marekani. Haya ni mafanikio makubwa kwa nchi na yalisherehekewa Bangladeshi nzima.

Bangabandhu-1, ilipewa jina hili ambalo ni jina la Sheikh Mujibur Rahman, ambaye ni baba wa Taifa la Bangladeshi, na ilirushwa katika mhimili wake wa nyuzi 119.1 longitudo ya Mashariki. Mpango huu wa setilaiti unategemewa kudumu angalau kwa miaka 15.

Ilipangwa chombo hicho kurushwa tangu Mei 10 lakini iliahirishwa na kufanyika siku iliyofuata baada ya kuonekana hitilafu dakika chache kabla ya kurushwa. Ujumbe wa maafisa wa Bangladesh uliongozwa na Waziri wa Mawasiliano ya Simu na Posta, Tarana Halim, waliwasili Florida siku ya Jumanne kushuhudia chombo hicho kikirushwa kwa mafanikio.

Peter B. de Selding, mhariri wa Space Intel Report aliandika:

Muundaji @Thales_Alenia amethibitisha kuwa hewani kwa Bangabandhu-1 yenye afya inayopeleka masafa kwa mionzi ya jua. Mpango umekamilika kwa kurushwa kwa mara ya kwanza kwa @SpaceX Falcon 9 Block 5 iliyoboreshwa. Bangladeshi sasa imejunga katika orodha ya nchi zinazomiliki setilaiti.

K. Scottt Piel, mhandisi wa software kutoka kituo cha Kenedy Space Center, alitwiti:

Muonekano wa 90 Magapixel kwenye  @SpaceX ikiwa imeibeba #Bangabandhu1

Kazi ilianza na setilaiti yenye uzito wa paundi 7,700 (kilo 3,700) kutoka kwenye kituo cha Kifaransa Thales Alenia Space by ilipoagizwa na Kamati ya Uratibu wa Mawasiliano ya Simu Bangladeshi (Bangladesh Telecommunication Regulatory Commission)

Kurushwa kwa chombo hicho ni mafanikio kwa kampuni SpaceX, iliyokuwa imechukuwa mkataba wa kukirusha chombo yenyewe. Ulikuwa mwanzo wa kupanda viwango kwa gari lao la kurushia linalojulikana kama Falcon 9 Block 5, ambalo ni la muundo ambao linaweza kutumika tena, na lenye msukumo mkubwa. SpaceX ni kampuni ya Kimarekani ambayo iliundwa mwaka 2002 na mjasiriamali Elon Musk. SpaceX ilitengeneza tovuti mubashara iliyoonesha chombo hicho kikirushwa na unaweza kuangalia mtandaoni:

Bangabandhu-1 itatoa huduma za runinga za setilaiti, mtandao wa intaneti, na huduma ya mawasiliano ya dharura kwa maeneo ya vijijini ya Bangladeshi na itaendeshwa na kampuni mpya iliyoundwa na inayomilikiwa na serikali inayoitwa Kampuni ya Mawasiliano ya Setilaiti Bangladeshi Ltd, baada ya kuwa imeongozwa mpaka sasa na Kamati ya Uratibu wa Mawasikiano ya Simu Bangladeshi mpaka sasa (Bangladesh Telecommunication Regulatory Committee – BTRC.)

Kulingana na the Dhaka Tribune, Bangladesh kwa mwaka hutumia kiasi cha dola milioni 14 kwa ajili ya kukodi mawasiliano ya setilaiti kutoka kwa makampuni ya kigeni. Inakisiwa kuwa kurushwa kwa Bangabandhu-1, itapunguza gharama hizo.

Setilaiti itatoa masafa ya Ku-band kwa Bangladesh yote na tawala zake zote za Pwani ya Bengal, India, Nepal, Bhutan, Sri Lanka, Ufilipino na Indonesia.

Masaa machache baada ya setilaiti hiyo kurushwa, Wananchi wa Bangladeshi wameonesha kuunga mkono mpango huo katika mtandao wa Twita.

Farhan Hossain aliandika:

Adnan Ahmed Khan aliandika:

Hata hivyo, baadhi ya watu kama vile Kazi Didar amesema kuwa matumizi makubwa kwa ajili ya Setilaiti ingependeza kama yangeelekezwa kwanza katika baadhi ya mahitaji muhimu ya waBangladeshi:

Haijalishi kuwa wengi wamechukulia hili kama mafanikio kwa Bangladesh:

Zenith a:

Raju aliandika:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.