‘Hakuna kupiga Kura Mpaka Barabara Ijengwe': Sababu ya Wanakijiji cha Goa Kususia Uchaguzi Mkuu wa India

Screenshot from YouTube video by VideoVolunteers.

Picha ya skrini kutoka katika video huko YouTube,  na VideoVolunteers.

Chapisho hili liliandikwa na Grace Jolliffe na mwanzoni and originally alilirushwa na Video Volunteers, kikundi cha kumtandao cha kimataifa kilichoshinda tuzo na makao yake makuu ni  India. Toleo lililohaririwa kidogo imechapishwa hapo chini kama sehemu ya makubaliano ya kushirikishana maudhuhi.

Wakati India ikipitia kipindi cha uchaguzi mkuu uliogawanyika katika awamu saba zinazoanzia 11 April mpaka 19 Mei 2019 ili kuchagua bunge lake la saba (Lok Sabha), baadhi ya wapiga kura wa India wamechukua hatia isiyo ya kawaida kwa kugomea shughuli za uchaguzi.

Huko Goa, jimbo la Kusini mwa India, wakazi wa kijiji kidogo kilichopo kitongoji  cha Cancona (sehemu ya wilaya), kijiji cha Marlem walikataa kupiga kura tarehe 23 Aprili katika awamu ya tatu ya uchaguzi mkuu wakiwa na madai kwamba serikali imekuwa ndio tatizo kuwa katika kijiji chao. Malalamiko yao makubwa ni kwamba mahitaji na huduma muhimu kama vile barabara nzuri na huduma ya maji safi na salama hazijawahi kutolewa na serikali.

Video ya Mtangazaji wa masuala ya kijamii  Devidas Gaonkar, mzaliwa wa kabila la wafugaji la waGoa inayoitwa Velip, ikionesha maandano ya wanakijiji hao:

Katika video hii, Pandurang Gaonkar, mkazi wa kijiji cha Marli alisema kwamba:

Tirwal to Marlem is a three-quilometres road stretch, which is incomplete. To date, no action has been taken by the authorities. They only make false promises, but no implementation. For this reason, we haven’t cast our votes.

Kuanzia Tirwal mpaka Marlem ni kilomita tatu tu za barabara lakini hazijakamilika. Mpaka leo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na mamlaka husika. Wanatupa ahadi za uongo tu hakuna utekelezaji. Na kwa sababu hiyo basi, hatujapiga kura.

Wakazi wa kijiji cha Marlem wamekuwa wakiishi katika kijiji hicho kwa zaidi ya miaka 20 sasa. Mwaka 1968, idara ya misitu ilitangaza kuwa kijiji cha Marlem kama  sehemu salama kwa wanyama wa mwituni. Hili linafanya ujenzi wa barabara au kazi yoyote ya maendeleo katika eneo hili kuwa na ugumu wa kutekeleza. Kulingana na taarifa,  ni kwamba mpango wa kupitisha mkongo wa umeme aridhini ili uweze kufika eneo hilo ulishapitishwa lakini ulizuiwa hivi karibuni kutokana na mapingamizi kutoka kwa Idara ya Misitu ya Taifa

Chanzo kingine cha mahangaiko ya wakazi wa hapa ni ukosefu wa barabara nzuri. Mtu anatakiwa kusafiri  kutoka barabara kuu umbali wa kilomita 2.8 katika barabara mbaya na ambayo haijasafishwa vizuri ili aweze kukuta nyumba ya kwanza katika kijiji cha Marlem. Mwisho kabisa, usambazaji wa umeme na maji safi na salama kwa wanakijiji vimebaki kuwa changamoto kwa wanakijiji.

Pamoja na kuweka malalamiko yao hadharani mara kwa mara, lakini wameshindwa kupata majibu ya mahitaji yao, wakazi wa Marlem pamoja na wakazi kutoka katika vijiji vingine viwili waliamua kutokupiga kura ili kuvuta masikio ya mamlaka dhidi ya masuala yao wanayoyalalamikia. “Wafanyakazi wa tume ya uchaguzi walikuja kuongea nasi kuhusu uamuzi wetu wa kutokupiga kura na msimamo wetu uko pale pale”, aliongeza Pandurang.

Isidore Fernandes, kiongozi wa upinzani kutoka chama cha (Indian National Congress) ambaye ni mbunge katika bunge la Cancona, pia alikutana na wakazi wa eneo hilo. Baada ya kusikiliza kero zao alieahakikishia kuwa atawasaidia kushughulikia jamjo hilo. ” Ni muhimu kwa serikali yoyote kutengeneza barabara, kusambaza umeme na maji kwa ajili ya watu wao. Mpaka sasa maafida wote wa serikali wamepuuza kutoa huduma hizi katika kijiji cha Marlem”, alisema   Fernandes.

Kususia uchaguzi sasa imekuwa kama njia mojawapo ya mgomo, ingawa kupiga kura sio lazima katika nchi ya India. Tofauti ya kijiji cha Goa, vijiji vilivyo katika jimbo la Kati Madhya Pradesh, Magharibi jimbo la Maharashtra, na Mashariki jimbo la Odisha wamekuwa wakitumia mbinu hii ili kuweza kufikisha mambo yao muhimu mbele ya viongozi wa mamlaka zinazohusika.

Hata hivyo, hakuna mgomo wowowte kati ya hii ambao umechukuliwa hatua na serikali. Wapiga kura wengi wameanza kuzoea kutumia mbinu hii kama ishara ya kuonesha hasira zao kwa wanasiasa na maofisa wa serikali ambao huzigeukia jamii walizozitelekeza katika kipindi cha uchaguzi wakiwa ma matumaini ya kupata kura zao, huku wakishindwa kutekeleza ahadi zao baada ya uchaguzi.

Lakini mwishowe, kama Kugomea chaguzi haitaleta mabadiliko katika jamii, je ni kitu gani wanajamii wataamua kufanya ili kuvuta masikio ya wenye mamlaka ambao wanapaswa kusikia sauti zao na kuchukua hatua za utekelezaji?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.