TAMKO: Global Voices Yatoa Wito wa Kuimarishwa kwa Usalama wa Wanablogu wa Bangladesh

"Who will be next?" Sketch of deceased Bangladesh bloggers by MadhuMondol.

“Nani atafuata?” michoro ya wanablogu wa Bangladesh waliouawa. Kwa hisani ya MadhuMondol.

Jumuia ya Global Voices yaitaka jamii ya kimataifa kutupia jicho hali tete ya usalama inayowakabili wanablogu wa Bangladeshi. Wanablogu wameshauawa, na wengine wengi wamesha shambuliwa, wakijikuta kwenye vitisho vya kuuawa na pia kutengwa na wahafidhina kutokana na mambao wanayoaandika. Kwa mwaka huu peke yake, wanablogu watatu waliuawa mbele ya hadhara.

Majina ya wanablogu hawa pamoja na wengine walio katika hatari hii yalionekana kwenye listi ya watu 84 iliyowasilishwa kwenye kamati maalum ya serikali na kikundi cha viongozi wa Kiislam kilichowatuhumu wanablogu hawa kwa kujihusisha na “upagani” pamoja na kuandika mambo yanayopingana na Uislam. Kufuatia tuhuma hizi kwa wanablogu hawa, Serikali iliamuru kufungwa kwa tovuti makini na kukamatwa kwa wanablogu pamoja na viongozi kwa kutumia sheria ya dini wakati ambapo maandamano ya #shahbag ya 2013 yalipokuwa wameshika hatamu. Baadhi ya vyombo vya habari, zikiwemo blogu maarufu za mrengo wa kulia, zimediriki hata kusambaza maneno kuwa wanablogu wote ni wapagani ambao “wamekuwa wakipotosha imani” ya waumini wa dini nchini Bangladesh.

Wapagani wana haki sawa na raia wengine wa nchini Bangladesh. Kwa mujibu wa sheria ya nchi, mtu yeyote aliye na madhumuni “thabiti” au “kushukiwa” “kudhuru hisia za kiimani” anaweza kuhukumiwa. Lakini machafuko yatokanayo na kujichukulia sheria mkononi pamoja na mauaji kunakotokana na tuhuma za kukashifu ni jambo lisilovumilika kabisa na ni dhahiri kuwa ni ukiukwaji wa sheria za Bangladesh. Hata hivyo, serikali ya kidini ya Bangladesh hadi sasa imeweka juhudi hafifu sana za kukemea mashambulizi haya au kuwafikisha wauaji kwenye vyombo vya sheria.

Wanablogu hawa hawakuwa wakiunga mkono au kujihusisha kwenye machafuko hayo. Walikuwa wakiandika kwa maoni yao kuhusiana na hali tete ya kisiasa ya Bangladesh pamoja na umuhimu wa kuweka kipau mbele haki za binadamu. Walikuwa wakitumia haki yao ya uhuru wa kujieleza, whuku wakilindwa na katiba ya taifa lao pamoja na Sheria ya kimataifa ya haki za binadamu ambayo Bangladesh ni mwanachama.

Global Voices ni jumuia ya wanablogu, wanaharakati, waandishi, na watafisi kutoka katika nchi 137. Haki ya binadamu ya kimataifa ya uhuru wa kujieleza ndiyo kipau mbele chetu katika dira yetu. Tunasambaza habari zisizopewa kipaumbele kutoka katika katika pande zote za dunia pamoja na kutetea haki ya kila mmoja ya kujieleza kwa uhuru bila ya hofu.

Miongoni mwa wanablogu hao, watu 84 katika listi hii ni marafiki na wachangiaji wa jumuia ya Global Voices. Pia, wapo wanablogu pamoja na wanaharakati wa mtandaoni ambao hawapo katika listi hiyo, lakini wapo katika hali hatarishi kutokana na uandishi na uanaharakati wao.

Kwa kila hali, tunahusika moja kwenye usalama wa wanablogu wa Bangladesh waliopo ndani na nje ya nchi hii. Tunawalaani waliofanya mauaji ya Ananta Bijoy Das, Ahmed Rajib Haider, Washiqur Rahman na Avijit Roy na pia tunazitaka mamlaka husika kuwachchukulia hatua za kisheria wale wote waliohusika kutimiza mauaji hayo. Na pia, tunawaomba washirika wetu wote wa jamii ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu kutuunga mkono ikiwa ni pamoja na kusaidia kuimarisha usalama wa watu wote walio katika mazingira hatarishi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.