Gazeti laBangladesh Daily Star siku ya August 4, 2016 liliripoti kuwa Tume ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Simu ya Bangladeshi iliamuru waendeshaji wa mitambo ya mitandao ya Internet ya kimataifa kufungia tovuti za habari zipatazo 35.
Hakuna maelezo zaidi yaliyojitokeza kuhusu kufungiwa huko mpaka sasa, lakini orodha ya tovuti hizo ni ndefu na inajumuisha tovuti zinazowakilisha maeneo muhimu ndani ya nchi hasa katika hali ya kisiasa ya sasa ya nchini. Orodha nzima ya tovuti hizo zilizoamriwa kufungiwa iko hapa chini kama ilivyoripotiwa na Daily Star.
Tovuti zilizoamriwa kufungiwa:
rtnews24.com
haquekotha.com
amrabnp.com
real-timenews.com
bnation24.com
nationnewsbd.com
bhoreralap.com
banglapost24.com
dailytimes24.com
mynewsbd.com
livekhobor.com
rikhan.com
sheershanewsbd.com
natunerdak.com
sylhetvoice24.com
somoybangla.com
prothom-news.com
banglalatestnews.com
bdmonitor.net
bdupdatenews24.net
newsdaily24bd.com
amardeshonline.com
doinikamardesh.com
onnojogot24.com
amarbangladesh-online.com
desh-bd.net
crimebdnews24.com
natunsokal.com
sheershakhobor.com
onb24.com
dinkalonline.net
sarabangla.com
parstoday.com
weeklysonarbangla.net
24banglanewsblog.wordpress.com
Hili linajitokeza katika mkanganyiko wa kufungiwa kwa mtandao wa internet kulikofanyika asubuhi ya tarehe 2 Agosti, wakati mtandao wa internet ulipokatwa katika mji wa kibiashara wa Dhaka kwa masaa matatu na nusu kama sehemu ya serikali kutekeleza mpango wa kujaribu uwezo wa mashirika ya simu nchini. Shirika la mawasiliano ya simu nchini lilionesha kuwa ilikuwa sehem ya mlolongo wa majaribio ya kuzima ambayo yatafanyika hivi karibuni nchini pote.
Mpango wa kuzima internet ulitangazwa Agosti 1 na kuwasilishwa kama mkakati wa kiusalama. Hili linafanyika kufuatia uvamizi wa kikatili uliofanyika mapema Julai katika enei la kuokea mikate la Holey Artisan, ambapo mateka wapatao 20 waliuawakama sehemu ya shambulio la kigaidi lililokuja katika kipindi ambacho vurugu zinaongezeka nchini .
Pamoja na mtandao wa intaneti huduma nyingine pia zilikatwa. Makampuni ya uendeshaji wa simu za mikononi yaliripotiwa kupimwa uwezo wao kuzima miito ya sauti na ISPs pia waliambiwa wafungie baadhi ya tovuti. Haijaeleweka vizuri kama tovuti hizi ndio zile zile zilizoamriwa kufungiwa hapo Agosti 4.
Mwenyekiti wa Tume ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Simu nchini Bangladeshi (BTRC), Shahjahan Mahmood, kuwa hili zoezi lilikuwa la kwanza kati ya mfululizo wa kuzima kwa muda kwa mitandao ya internet, anasema “Kama sehemu ya zoezi linaloendelea, aina zote za mitandao ya internet itasimamishwa kwa kipindi kifupi kwa muda wowote na mahali popote hapa nchini,”
Ahsan Habib Khan, makamu mwenyekiti wa BTRC aliongezea kuzimwa huko kwa mitandao hiyo mara nyingi itakuwa inafanyika wakati wa usiku na siku za mapumziko.
Wananchi wanapambana kuona jinsi kuzimwa huko kwa mitandao kutakavyokuwa na matokeo chanya katika usalama wao, lakini changamoto zimeonesha kukwama kwa mkakati huo. Wananchi wa Bangladeshi wameeleza masikitiko yao na hasira zao kupitia mitandao ya kijamii kwa mtumiaji mmoja wa mtandao wa Facebook kuandika:
Na hiki ni nini?? Bila hata ya taarifa kabla au kwa taarifa ya muda mfupi hivyo?? Wanajua jinsi watu wqnavyofanya kazi kweli au kujua jinsi jambo hilo linavyoweza kuathiri kazi zao?? Fikiria kuhusu hali hiyo-mtandao unazimika katika eneo ghafla tena katika nyakati muhimu ambapo watu karibia wote hawajui kuhusu hilo na huwezi kutumia mtandao katika simu yako ya kiganjani kufanya mawasiliano na mtu mwingine kumpa taarifa kuhusu hali mbaya iliyosababishwa katika eneo zima.
Huko Twitter, kundi la haki za kiteknolojia Access Now ziliita vitendo hivi kuwa “potofu” kama sehemu ya kampeni yao ya kimataifa kupinga kuzimwa kwa huduma ya internet, #ziwasheni.
YA KUSHTUKIZA: Leo Bangladesh imetangaza “mpango” wa kuzimwa kwa mtandao wa internet. Huu ndio mtazamo wetu. #Usizimwe pic.twitter.com/0gVp1ndX8I
— Access Now (@accessnow) Agosti 1, 2016
Hii sio mara ya kwanza mitandao kuzimwa kwa makusudi nchini Bangladeshi. Novemba 2015, serikali ya Bangladeshi ilifungia kurasa za mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, Viber na Whatsapp kwa kipindi cha karibu wiki nne. .
Siku ya kwanza ya marufuku hiyo, huduma za internet zilikatwa nchi nzima kwa muda unaokadiriwa ni dakika 75. Mara moja baadaye, Mahmood alisema kuwa kuna makosa yalijitokeza na kuzimwa kwa mitandao hiyo ilikuwa ni matokeo ya “kutokuelewana”
Msukumo huu mpya wa kuwaondoshea wananchi mtandao wa interneti unatia hofu sana, hasa kwa Bangladesh ambapo uhuru wa kujieleza unaendelea kuwa chini ya vitisho , kote mitandaoni na katika maisha ya kila siku.
Mwaka 2011, Umoja wa mataifa ulitangaza kuwa upatikanaji wa huduma za Internet kuwa haki ya msingi katika haki za binadamu. . Ni wiki nne tu zimepita, Baraza la Umoja wa Mataifa linalosimamia Haki za Binadamu ijumaa lilipitisha azimio lisilo la kisheria likilaani nchi zinazozuia au kukwamisha upatikanaji wa huduma za Interneti.
Licha ya kujirudia kwa ukiukwaji huu wa haki za kiteknolojia, madai ya serikali kuwa inasonga mbele kuelekea ” Bangladeshi ya Kitenolojia” yameendelea.