Bangladesh: Jengo Laporomoka, Mamia Wauawa kwenye Vifusi

Jengo la ghorofa tisa lililokuwa na idadi kubwa ya watu wanaotengeneza nguo liliporomoka huko Savar, nje kidogo ya mji mkuu Dhaka na kuua watu 142 na kujeruhi takribani watu elfu moja, hali iliyopelekea kuibua umakini wa hali ya usalama kwa sekta ya viwanda nchini Bangladesh.

Zaidi ya watu elfu moja inaaminiwa bado wamenaswa kwenye kifusi cha jengo hilo.

Watengenezaji sita wa nguo walikuwa wakiendelea na kazi katika ghorofa ya tatu hadi ya nane ya jengo hilo huko Savar na watu wasiopungua elfu tano walikuwa ndani ya jengo lililokuwa na msongamano mkubwa wa watu wakati lilipoanguka asubuhi ya tarehe 24, Aprili 2013.

Tukio hili linakuja miezi mitano baada ya tukio jingine la moto ambalo liliua zaidi ya watu 100, wengi wao wakiwa ni wanawake katika kiwanda kingine cha nguo kilichokuwa na msongamano mkubwa wa watu kijulikanacho kama “Mitindo ya Tazreen”.

Tangu kutokea kwa tukio hilo, kumekuwa na ongezeko kubwa la umakini wa usalama wa wafanyakazi pamoja na kutokuwa na muitikio usioridhisha itokeapo dharura katika viwanda. Wafanyakazi wa kiwanda cha nguo wamekuwa wakinung’unika dhidi ya ujira mdogo wanaopewa.

Bangladesh ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa nguo zilizo tayari kuvaliwa baada ya China. Wauzaji wa rejareja wa kimataifa kama vile Walmart, H&M, Sears, GAP, Tommy Hilfiger na mitindo mingine maarufu huagiza nguo zao kutoka Bangladesh zikiwa na kibandiko cha”Imetengenezwa Bangladesh”, ambayo ni sifa kubwa kwa nchi hii. Mwanablogu na mwandishi Arafatul Islam anafikiri kuwa, sifa ya aina hii ipo hatarini:

পোশাক কারখানায় আগুন লেগে পুড়ে মরে শ্রমিক, পোশাক কারখানার ভবন ধসে চাপা পড়ে মরে শ্রমিক… লাশের মিছিল এভাবেই বেড়ে চলে। আগে ‘মেইড ইন বাংলাদেশ’ দেখলে আগ্রহ ভরে কিনতাম। এখন কেমন যেন সেই লেখার মধ্যে রক্তের দাগ দেখতে পাই, মৃত্যুর আর্তনাদ শুনি।

Wafanyakazi wanakufa kwa moto wa viwanda, wafanyakazu wanakufa kwa kuangukiwa na majengo… wimbi la watu kufa linaongezeka. Nilizoea kununua nguo zenye kibandiko “Imetengenezwa Bangladesh” kwa kujivunia. Kwa sasa ninaona damu kwenye kibandiko hicho, ninasikia kilio cha wafu.

the scene after a nine-storey building collapsed in Savar

muonekano wa jengo la ghorofa tisa lililo anguka huko Savar, nje ya jiji la Dhaka. Picha na Firoz Ahmed. Haki miliki na Demotix (24/4/2013)

Watumiaji wa mtandao wameonesha katika mitandao ya kijamii hali ya kufedheheshwa kufuatia matukio haya yanayojirudiarudia katika viwanda vya nguo. Katika sekta hii, wanawake ndio wengi zaidi. Mwanablogu Vashkar Abedin katika ukurasa wa Facebook anaandika:

আহা বোন!
সুঁচ-সুতো দিয়ে কেবল নিজেদের মৃত্যু বুনে যাচ্ছো…

Ah dada!
Washona kifo chako tu…

Joydeep Dey Shaplu hawezi kutawala hasira yake katika ukurasa wa Facebook:

এতো লাশের ভিড়ে কেউ জীবিত থাকতে পারে না। আমি আপনি সব শালা লাশ… নইলে এতো লাশ পড়তো না এ দেশে…

hakuna atakayekuwa hai miongoni mwa miili hii ya watu waliokufa. Sisi ni mizimu.. vinginevyo tusingeweza kuacha idadi kubwa hivi ya watu wafariki..

Ushahidi unaonesha kuwa, kulikuwa na ufa kwenye jengo hilo siku moja kabla ya tukio. viwanda vilifungwa haraka sana. [bn]. Lakini dalili za kuanza kuanguka hazikutiliwa maanani na mmiliki wa jengo hilo kwani alilifungua kw ajili ya biashara mnamo tarehe 24 Aprili na wafanyakazi walilazimishwa kurudi kazini. Sumeema Yasmin Sumi hawezi kukubaliana na maamuzi haya yasiyokuwa makini kutoka kwa wamiliki:

এতোগুলো মানুষকে মৃত্যুর দিকে ঠেলে দেয়া হলো! এরকম দায়িত্বহীনতা কোনোভাবেই মেনে নিতে পারছি না।

Watu wengi sana walisabishiwa kifo. Siwezi kukubalian na hali hii ya kutokuwajibika kulikooneshwa na wamiliki wa jengo hili.

Lucky Akter, mmoja wa wanaharakati waandamizi wa #maandamano ya Shahbag aliandika kwenye Somehwhereinblog katika makala iliyokuwa na kichwa cha habari”Hakuna maombolezo, bali maandamano”:

দাসপ্রথা নাকি বিলোপ হয়েছে বহু আগে কিন্তু আমরা তো দেখি দাস প্রথা নতুন ভাবে ফিরে এসেছে খুব ভয়ালভাবে, তা না হলে মৃত্যু নিশ্চিত-জেনেও শ্রমিকদেরকে পিটিয়ে পিটিয়ে কেন মৃত্যুকূপে পাঠানো হল? কেন মিথ্যা বেতনের আশ্বাস দিয়ে শ্রমিকদেরকে কারখানায় আনা হল?

Utumwa ulishasitishwa miaka mingi iliyopita. Lakini tunaona kuwa, utumwa umerudi tena kwa namna mpya. Vinginevyo, kama ilifahamika kuwa kulikuw na hatari ya watu kutopoteza maisha, iliwezekanaje hadi watu hawa wakalazimishwa kuingia kwenye hatari ya kifo?Slavery has been abolished long ago. But we see that slavery has returned in a new form. Otherwise knowing that there is a death-risk, how come these laborers were forced to enter the death-zone? Je, walirubuniwa kurudi kazini kwa kuahidiwa kifuta jasho?

 Kazi ya uokoaji imeshakuwa ngumu

Wanajeshi na raia wa kujitolea wanafanya kazi pamoja katika kuwaokoa watu walionasa kwenye kifusi cha jengo hilo. Picha na Firoz Ahmed. Haki miliki na Demotix (24/4/2013)

Sehemu kubwa ya fedha za kigeni za Bangladesh zinatokana na viwanda vya nguo zilizo tayari kutumiwa moja kwa moja. Tamanna Sultana anaandika katika ukurasa wa Facebook:

আমি লজ্জিত! একটা দেশের অর্থনীতির মূল চালিকাশক্তি যারা, তারা শয়ে শয়ে মরে গেলেও তেমন কিছু যায় আসে না। এই ঘটনা বার বার ঘটতে থাকে। বড় বড় ব্যক্তিগুলো সুখে শান্তিতে বসবাস করতে পারলেই হলো…

Ninajionea aibu! Hao walio uti wa mgongo wa nchi wanakufa kwa mamia, na hakuna anayejali. Na hili linarudiwa mara kwa mara. Inaonekana kama vile tunawajali sana matajiri na wenye nguvu tu.

Wamiliki wa viwanda au hao wanaohusika ni nadra sana kuhukumiwa kwa kushindwa kutoa huduma stahiki kulikopelekea uharibifu mkubwa kiasi hiki. Apurbo Shohag anaonesha ghadhabu yake katika Facebook:

এই দেশে মৃত্যু কোনো ব্যাপার না। এই দেশে সবচে’ সস্তা জিনিস হলো মানুষের প্রাণ! শুধু আজকে সাভারেই নয়, এর আগেও যখন গার্মেন্টস কারখানাগুলোতে অসংখ্য প্রাণ শেষ হয়েছে বা ভবন ধসে মানুষ মরেছে আমরা তখন শুধুই শুনে গেছি মালিকদের শাস্তি হবে। শাস্তি হয় কি না সেটা আর জানা হয় না। তবে একের পর এক সাভারের মতো ঘটনা ঘটছেই। দীর্ঘ থেকে দীর্ঘ হয় লাশের লাইন।

Katika nchi hii, kifo kinaweza kumkuta mtu kirahisi sana. Kwa kuwa jambo rahisi kabisa ni uhai wa mtu. Siyo tu uharibifu huu wa leo wa Savar, tumeshasikia mara nyingi sana ukiachia maafa haya ya kuporomoka kwa viwanda kwani hao wanaohusika ikiwa ni pamoja na wamiliki watafikishwa mahakamani. Lakini hatuoni wakiadhabiwa. Kwa hiyo majanga haya yanajitokeza mara kwa mara. Miili ya watu waliokufa inajirundika kwa idadi kubwa kabisaThe bodies pile up in greater numbers.

ধ্বংসস্কুপের ভেতরে চাপা পড়ে আছে এখনও অনেকে। ছবি ফিরোজ আহমেদের। সর্বস্বত্ব ডেমোটিক্স (২৪/৪/২০১৩)

Watu wengi bado wanazikwa kwenye vifusi vya zege. Picha na Firoz Ahmed. Haki miliki na Demotix (24/4/2013)

Serikali imetangaza Siku ya maombolezo [bn] kufuatia idadi kubwa ya watu kupoteza maisha. Kulikuwa na maombi kupitia Facebook ya kuchangia damu, na wengi walijitokeza kuchangia damu huko Savar na kwingineko.

Blood donation in Shahbag Square for the injured people of Savar building collapse. Image courtesy Shahbag Movement Facebook page

uchangiaji wa damu unaendelea katika eneo la wazi lililozungukwa na majengo la Shahbag kwa ajili ya kuwasaidia watu waliojeruhiwa kufuatia jengo lililoporomoka huko Savar. Picha kwa hisani ya Ukurasa wa Facebook wa Harakati za Shahbag.

Taarifa zaidi zilikuwa zinatumwa katika mtandao wa Twita:

@ShahbagInfo: damu yenye Rh hasi inahitajika #Shahbag; Mifuko 700 ya damu imekusanywa hapa, 500 imetumwa katika hospitali ya chuo cha Dhaka na kwenye kambi; Hospitali ya chuo cha Enam. #Savar

Wanaojitolea kwa ajili ya Bangladesh crowdsourced volunteers kupitia mtandao wa Facebook kwa ajili ya kusaidia michakato ya uokoaji. Picha zaidi kuhusian na janaga hili zinapatikana katika makala hii iliyoandaliwa na Mwanablogu Bishkhoy.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.