Habari kutoka 29 Aprili 2013
Bangladesh: Jengo Laporomoka, Mamia Wauawa kwenye Vifusi
Janga jingine tena la kiwanda nchini Bangladesh, safari hii jengo la ghorofa tisa lilianguka na kuua zaidi ya watu 142 na watu wengine karibu elfu moja kujeruhiwa. Watu wengine wengi bado wamenaswa kwenye kifusi na harakati za kuwaokoa bado zinaendelea. tukio hili linatokana na uzembe wa baadhi ya watu kwani utawala wa kiwanda hiki uliwashinikiza watu kuendelea kufanya kazi katika jengo ambalo halikuwa salama.
Ujasiriamali,Utamaduni na Mshikamano katika Afrika
Pamoja na ukuaji mkubwa wa kiuchumi, bara la Afrika bado linahangaika kukuza kada ya wajasiriamali wazawa watakaoweza kudhibiti viwanda vya kimkakati. Wasomi na watafiti wengi wa ki-Afrika wanajaribu kuelewa atahri za tabia za kimila katika ujasiriamali barani humo.