Habari Kuu kuhusu Saudi Arabia
Habari kuhusu Saudi Arabia
Jinsi Viongozi Wa Saudia Wanavyotumia Dini Kujiimarisha na Kunyamazisha Sauti za Wakosoaji
''Unyanyasaji ni mfumo wenye mizizi mirefu, na [kwenye nchi yetu] unawezeshwa na dini.''
Mtumiaji wa Twita Nchini Saudi Arabia Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 10 na Viboko 2,000 kwa Kosa la “Kukufuru Dini”
Saudi Arabia imemhukumu mtumiaji wa mtandao wa Twita kifungo cha miaka 10 jela pamoja na viboko 2,000 kwa kosa la kuandika twi 600 "zinazoeneza imani ya ukana-Mungu" mtandaoni.
Polisi wa Kidini Thelathini Nchini Saudi Arabia Wahitimu Mafunzo ya Kukabiliana na Uchawi
Wajumbe thelathini wa Tume ya Kusimamia Maadili na Kukabiliana na Maovu wamemaliza mafunzo ya siku tano ya namna ya kukabiliana na uchawi, kuwatambua walozi na hata kuvunja laana zao.
ISIS Yashambulikia Kwa Mara Nyingine Msikiti wa Shia Nchini Saudi Arabia
kwenye dawati lakuthibitisha habari la Global Voices, mradi unaoendeshwa kwa ushirikiano kati ya Meedan Checkdesk, zana ya mtandaoni ya kufuatilia habari, na Global Voices Online, Joey Ayoub anaonesha miitikio ya awali kabisa kuhusu kupigwa bomu kwa msikiti wa pili wa Shia huko Dammam, Jimbo la Mashariki mwa Saudi Arabia, siku...
Je, Saudi Arabia Imelishambulia Bwawa la Kale la Marib Nchini Yemen?
Kuna taarifa zisizodhibitishwa zinazosema kwamba vikosi vya pamoja vya Kisaudi, ambavyo vimekuwa vikiishambulia Yemen kwa mabomu kwa zaidi ya miezi miwili sasa vimelilenga Bwawa la Marib, moja wapo ya maajabu makuu ya katika ulimwengu wa ubunifu wa kale wa kiufundi. Kwenye mtandao wa Twita, Hussain Albukhaiti anadai: Unconfirmed reports: #Saudi...
Magazeti Maarufu Iran Yataka Kusitishwa kwa Mashambulio ya Anga Nchini Yemen
Magazeti mawili yenye umaarufu mkubwa leo katika kurasa za mbele yalihanikizwa kwa habari za kushindwa kwa Saudi Arabia. Habari zili zimetokana na tangazo la Saudi Arabia la kusitisha mashambulizi ya anga dhidi ya Yemen mapema Jumanne hii. Kayhan, gazeti lililo na uhusiano na kiongozi mkuu wa Kidini, Ayatollah Khamenei, katika ukurasa wake...
Siku ya Wajinga: Waislamu Hawaruhusiwi Kudanganya Kamwe
Pamoja na maonyo, kwamba kufuata mkumbo wa Siku ya Wajinga Duniani kidini adhabu yake ni moto wa milele, watumiaji wa mitandao Uarabuni, waliitumia siku hii kuzikosoa serikali zao.
Saudi Arabia Inadhibiti Majina ya Watoto
Huruhusiwi kumwita mwanao wa kike majina kama Eman, au Sandy, au Yara. Na kama ni mvulana, majina kama Abdelnasser, Amir au Abdulmoeen hayaruhisiwi. Lakini hiyo si Saudi Arabia pekee. Kwenye mtandao wa twita, Iyad El Baghdadi anaorodhesha majina ya watoto yaliyopigwa marufuku kabisa kwenye ufalme huo: Orodha ya majina yaliyopigwa...
Pakistan, Usiingilie Vita vya Ndani ya Syria
Siku moja baada ya dondoo ndogo ya habari yenye kichwa cha habari, “Saudi Arabia ‘inatafuta uungwaji mkono kwa waasi wa” ilipoonekana kwenye magazeti ya Pakistani, mwanablogu wa siasa Ahsan Butt aliposti tahadhari kali kwa watunga sera ya mambo ya Kimataifa wa nchi ya Pakstani kuachana na mambo ya ndani ya...
GV Face: Wanawake Nchi Saudi Arabia Wanuia Kuendesha
Katika toleo la GV Face wiki hii, tunakutana na mwanablogu wa Jeddah na mwandishi Tamador Alyami anayeunga mkono kampeni ya #WanawakeWataendesha, Hadeel Mohammed, Mwandishi wetu wa Saudia anayeishi Dammam na Mhariri wetu wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Amira Al Hussaini