Jinsi Viongozi Wa Saudia Wanavyotumia Dini Kujiimarisha na Kunyamazisha Sauti za Wakosoaji

Msikiti Mkuu wa Mecca, inaaminiwa kuwa sehemu takatifu zaidi kwa Waislamu. Picha na Wikimedia mtumiaji Basil D Soufi [CC BY-SA 3.0].

Wakati mwanahabari wa Saudia na mwandishi wa makala katika Washington Post, Jamal Khashoggi alipouawa Oktoba katika ubalozi wa Saudia huko Instabul, kuleta giza totoro katika uhuru wa kujieleza kwa wanahabari kutoka Saudi Arabia na ukanda wote wa Arabuni.

Matokeo ya anguko hili la kisiasa limetikisa baadhi ya mamlaka zenye nguvu sana na sauti kubwa katika Uislamu.

Baada ya tukio la kupotea kwa Khashoggi na kifo chake kufahamika, viongozi mbakimbali wa duniani wamemtuhumu mwana wa mfalme wa Saudia Mohammad Bin Salman kuagiza mauaji ya mwanahabari huyo. Katika kile kilichoonekana kama majibu ya tuhuma hizo,  Imam Mkuu wa msikiti huko Mecca alitoa mawaidha ya Ijumaa ya Oktoba 19, ambapo alimsifia mtawala mkuu wa Ufalme Bin Salman.

Sheikh Abdulrahman al-Sudais katika mawaidha yake yaliyokuwa yamepitiwa kwanza na mamlaka za Saudia, alitaja “mabadiliko ya kisasa” aliyoyafanya Bin Salman na kukosoa mashambulizi dhidi ya “ardhi hizi zilizobarikiwa”. Alihitimisha kwa kusema kuwa “[lilikuwa] jukumu la waislamu wote kuunga mkono na kumtii Mfalme na Mrithi wa Kiti cha Ufalme Mtiifu, mlinzi na kiongozi wa maeneo matakatifu na Uislamu” 

Akijibu katika kipande kidogo cha maoni katika gazeti la New York Times, Profesa katika shule ya Sheria ya UCLA, profesa Khaled M. Abou El Fadl alisema mawaidha yale “yalinajisi na kuchafua” misingi ya Mtume.

“Kwa kutumia msikiti mkuu kusafisha vitendo vya unyanyasaji na udhalimu aliandika,” Mwana wa mfalme Mohammed ameweka misingi ya Uhalali ya Saudia kuongoza na kulinda maeneo matakatifu ya Mecca na Medina katika maswali.”

Historia ndefu ya Saudi Arabia katika Siasa na Dini

Kwa utaratibu wa kuongoza kwa kutumia sheria za dini, hili sio jambo la ajabu katika Ufalme huu wa kihafidhina uliokithiri. Kwa hiyo, viongozi wa Saudia wamekuwa wakiitumia dini kama zana ya nguvu kisiasa tangu kuanzishwa kwa ufalme huo.

Saudi Arabia ni nyumbani mwa maeneo mawili matakatifu ya Uislam, Mecca na Medina.

Kila mwaka, Mamilioni ya Waislamu kutoka kote ulimwenguni husafiri kuelekea Mecca kwa ajili ya kuhiji ambapo ni moja ya nguzo tano za Uislamu. Hili limeifanya serikali ya Saudia kudai uhalali maalum wa kidini katika Uislamu. Ufalme umekuwa ukiutumia uhalali huo kupata na kuendeleza mamlaka yake ya kisiasa.

Wakati mamlaka ya kwanza ya Saudia ilipoanzishwa mwaka 1744, Amiri wa mji mdogo wa vijito vya Diriya Muhammad ibn Saud, alifanya makubaliano na viongozi wa kidini na muumini wa dini ndugu Muhammad ibn Abd al-Wahhab. Abd al-Wahhab alianzisha mchakato wa uhafidhina wa kidini uliopitiliza (kwa sasa unafahamika kama Uwahhabi) ukilenga tafsiri yenye msimamo mkali wa Korani na desturi za Mtume.

Fanack, chombo huru cha habari na tovuti ya uchambuzi iliyojikita kwenye mji wa  MENA, inafafanua  kuwa muungano ulikusudiwa “kutengeneza mazingira ya Kiislamu yenye kuongozwa na tafsiri zenye msimamo mkali wa Uislam.”

Mamlaka hii ya kwanza ya Saudia ilianguka miongo kadhaa baadaye na mamlaka ya pili iliundwa mwaka 1824, na ilianguka tena mwaka 1891. Mwaka1924 na 1925, familia ya Ibn-Saud iliivamia Mecca na Medina (Miji mitakatifu ya Uislamu) wakisaidiwa kwa ukaribu na wapiganaji wa Wahhabi. Mwaka 1932, Ufalme wa Saudi Arabia ulianzishwa rasmi. Tangu hapo, viongozi wa Saudia wameendelea kuitumia dini kutumikia malengo yao ya kisiasa.

Sauti zinazotaka mjadala rasmi wa kidini zanyamazishwa.

Leo historia ya ufalme wa Saudia ipo juu kabisa katika vichwa cha Wasaudia wengi kwa jinsi wanavyokubaliana na ongezeko la viwango vya ukandamizwaji chini ya uongozi wa Mohammad Bin Salman. Watoa mihadhara ya kidini wameorodheshwa ili kuwaondosha wale wanaokemea uvunjaji wa haki au kupigania mabadiliko kwa kuwaita “maadui wa Uislamu” na mamlaka za nchi zimeendelea kupeleka na kutumia mijadala ya kidini kufikia malengo yao ya kisiasa.

Januari 2019, Waziri wa Masuala ya Uislamu Saudia ndugu Abdullatif Ibn Abdulaziz Al-Sheikh alikemea machafuko ya Waarabu ya 2011 na 2012, akiyaelezea kama “yenye sumu na uharibifu kwa Waarabu na binadamu wa Kiislamu.”

Katika rejea thabiti ya ukosoaji uliolenga Ufalme baada ya mauaji ya Khashoggi waziri alikemea kile alichokielezea kama ” mashambulizi yasiyo ya haki kutoka kwa maadui wa Uislamu” na akawatuhumu Waislamu wanaokosoa Ufalme na sera zake kwaa “kueneza uchochezi, kuleta mafarakano na uchochezi dhidi ya watawala na viongozi wao.”

Akiangazia kuhusu uhusiano baina ya Uwahhabi na ukandamizaji wa kisiasa, mwanaharakati wa haki za binadamu huko Saudia, Yahya Assiri, ambaye anaishi uhamishoni huko London, alitwiti hapo Januari 13

Ukandamizaji ni mfumo endelevu na (katika nchi yetu) unawezeshwa na dini Wakati Ibn Saud na Ibn Abd al-Wahhab walipoungana, Saudi Arabia na Uwahhabi waliongezeka na kuwa mapacha wakubwa sana. Nchi yetu haitaweza kuhimili labda tutokomeze ukandamizaji wa Saudia na Wahhabi. Kama ambavyo tulisema hili, wengine, wenye nia njema walishasema kwamba Uwahhabi ni harakati za kidini wakati kwa ukweli ni harakati za kisiasa.

Lakini sauti za watu kama vile Assiri zimenyamazishwa nchini Saudi Arabia.

Sauti nyingine kama hiyo ni ya Abdullah Al-Hamid ambaye yupo gerezani sasa na ni mmoja wa waanzilishi wa Chama Cha Haki za Kiraia na Kisiasa cha Saudia ambacho hakipo tena.

Al-Hamid anatumikia kifungo cha miaka kumi na moja gerezani kwa sababu ya harakati zake za kutetea haki za Binadamu, alihukumuwa kwa makosa ya ” kutokutii watawala” na uchochezi kwa kuitisha maandamano”. Alihukumiwa mwaka 2013 na mahakama Maarufu ya Makosa Maalumu ya Jinai, iliyoundwa kwa ajili ya makosa ya kigaidi lakini mara nyingi hutumika kuwahukumu wanaharakati wa haki za binadamu.

Vikundi vya Haki vimeripoti kuwa Al-Hamid alianza mgomo wa kula kuanzia Februari 17. Katika ujumbe uliokuwa umeandikwa naye na kuchapishwa na jukwaa la Haki za binadamu la MBS Mimi Pia, Al-Hamid alitamka kuwa anataka kachiliwa huru kwa wanaharakati wote wa Haki za binadamu na wafungwa wa kisiasa walio magerezani.

Abdullah Al-Hamid. Picha kutoka akaunti yake ya Goodreads.

Kwa kuongezea katika harakati zake za Haki za Binadamu, Al-Hamid pia ni mshairi na mwanazuoni. Katika maandiko yake, ametumia vitabu vya Kiislamu na vya kiutamaduni kuitisha mabadiliko ya kidemokrasia, akilenga haki za binadamu na akikosoa taasisi za kidini ambazo zinawezesha ukandamizaji Saudi Arabia kama vile Baraza la Mawalii Wakuu ambalo ni chombo kikuu cha kidini katika ufalme ambapo humshauri mfalme katika masuala ya kidini.

Mara moja alilituhumu Baraza hilo kutumika kuunga mkono ”Wale wanaoiba fedha za wananchi, utu wa watu na uhuru wao” na kuwajibika katika nafasi ya “kuwaumiza raia kwa pamoja na kuondoa uvumilivu” na kuzalisha vurugu na misimamo mikali.”

Pia alizungumza kuhusu “mijadala ya kisasa ya kidini ambayo inakumbatia utawala shirikishi” na alipinga alichokielezea kama “mijadala ya kawaida ya kidini” katika ufalme ambayo “hufanya sala nyuma ya Iman asiyetenda haki…hata kama anavunja haki, uhuru na usawa wa mtu mwingine.”

Ukandamizaji wa Wahubiri huru 

Wakati wakiwanyamazisha wale wanaoikosoa mijadala ya maafisa wa serikali, Saudi Arabia pia imechukua hatua kali dhidi ya Wahubiri ambao hawaungi mkono ipasavyo sera na vitendo vya Mwana Mfalme.

Wahubiri wa Saudi kama vile Sheikh Salman Al-Awda, Ali Al-Omari na Sheikh Awad Al-Qarni walikamatwa Septemba 2017 kwa makosa mbalimbali ambayo yaliwahusisha na kikundi cha Muslim Brotherhood. Vikundi vya Haki za binadamu vinasema kuwa mashitaka yao yaliletwa kwa sababu Wahubiri hao hawakuunga mkono kwa maneno  Saudi Arabia kuvunja ushirika wake wa kibiashara na wa kidiplomasia na Qatar na washirika wake. Na wote watatu wanaweza wakahukumiwa kifo.

Akiwa na miaka 62, Sheikh Salman Al-Awda ni muhubiri muhimu akiwa na wafuasi wengi katika majukwaa ya mitandao ya kijamii, sio Saudi Arabia Pekee bali ukanda wa Arabuni wote. Idadi ya wafuasi wake ikiunganishwa kutoka Instagram, Facebook, Twitter and YouTube ni zaidi ya milioni 22. Hapo mwanzo alishawahi kuunga mkono machafuko ya Waarabu mwaka 2011 na aliitisha mabadiliko ya kidemokrasia katika Ufalme na katika Ukanda wote.

Shirika la Haki za Binadamu na makundi mengine ya haki za Binadamu walihusianisha kukamatwa kwake na chapisho moja la 8 Septemba katika ukurasa wake wa twita, ambapo aligusia  habari kuhusu mapatano muhimu baina ya mataifa. Katika sehemu ya pili ya bandiko lake twita, aliandika: “Mungu alete amani katika mioyo yao kwa kile kilicho chema kwa watu wao”.

Ali Al-Omari ni mwanazuoni wa masuala ya dini na mwenyekiti wa 4Shbab, kituo cha runinga cha Kiislamu kinacholenga vijana. Tofauti na wenzake, sio mzungumzaji wa masuala ya kisiasa katika ufalme. Na mara moja alishawahi ku-tweet akiwaunga mkono viongozi wa ufalme na aliandika bandiko akiomba kwa ajili mafanikio ya Bin Salman alipoteuliwa kuwa mrithi wa kiti cha mfalme hapo Juni 2017.

Sheikh Awad Al-Qarni amekuwa akipokea tuhuma mbalimbali ikiwamo kuwaunga mkono kikundi cha Muslim Brotherhood, kukiuka sheria za Saudi Arabia, kuusingizia ufalme, kanuni zake na sheria zake na mfumo wake.

Wakutubi wengine kadhaa wako magerezani kwa sasa huko Saudi Arabia. Baadhi wameitisha mabadiliko ya kidemokrasia katika Ufalme kama vile Al-Awda, wakati wengine walipaza sauti wakimpinga Bin Salman na sera  zake au mabadiliko ya kijamii. Wengine kama vile al-Omari hapo nyuma alishawahi kuunga mkono watawala wa Saudi Arabia na Mrithi wa Kiti cha Mfalme.

Kinachothibitishwa na kesi hizi ni kuwa chini ya utawala wa Bin Salman, ukimya hautoshi tena. Zaidi ya muhuri wa mamlaka kunyamazisha “sauti huru” -maneno ya yeyote ambaye hayaandiki kwa ajili ya mamlaka ya ufalme au ajenda yake ya kisiasa- wahubiri lazima waende mbali zaidi na kumsifia hadharani mrithi wa kiti cha ufalme na uongozi wa Saudia.

Mitazamo na itikadi za wafungwa wa hisia kwa sasa ziko kifungoni huko Saudi Arabia, ikiwamo mpigania haki za wanawake, mpigania haki za binadamu, waandamanaji wa Kishia na wahutubu wa kidini, zinaweza kutofautiana. Lakini chini ya utawala wa Bin Salman ndugu wote hawa wamehukumiwa chini ya mkono dhalimu wa mamlaka za Saudia ikiwamo vizuizi holela, vifungo vya siri, mateso, and kupotea kwa kukusudia. Kuhalalisha na kusafisha matendo ya unyanyasaji, watawala wa Saudia hawakawii kutumia dini kama kinga.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.